Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Amina.Mungu akubariki pia......Asigwa nashukuru sana kwa kunipa taarifa hii.hapa nina bata mzinga na kanga wachache nitawatenga ili kuepusha hayo matatizo.ubarikiwe ndugu yangu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amina.Mungu akubariki pia......Asigwa nashukuru sana kwa kunipa taarifa hii.hapa nina bata mzinga na kanga wachache nitawatenga ili kuepusha hayo matatizo.ubarikiwe ndugu yangu
Haujachelewa hata kidogo,mara ulipogundua hii fursa ya kuwa tajiri ni mwanzo wa utajiri wako.chukua hatua na usiogope changamoto utakazokutana nazo.karibu darasani kwa mwalimu Kubota.Jaman najutia kutofuatlia kwa mada hii nw ningeshakuwa tajiri.
Niko na mitetea kama kumi ivi ndo wanataga wakitotoa vitoto tuu ,vifaranga ntavitenga na mama zao na kuanza wafeed kama vifaranga wa kisasa ili mama zao waanze maandalizi ya kutaga tena.
Hii mbinu ikitick nitawapa feedbak.
Ugumu wa maisha unakufanya uwe creative hope 2015 kutakuwa na ahueni maan wananchi tumetelekzwa bei hakushikiki akina pride na finca nao wanabana vimkopo vidgo vidogo sana
hyo njia ni nzuri sana ila wape chanjo ya newcastle baada ya siku 7. Then viangalie vsiloane. M talking through my litle experience na nilifanikiwa. In addition kwa hlo kuku aliyetoka kuatamia huwa namtenga na majogo for 3 day. Ninapomchanganya na majogoo humchangamkia kisawasawa na baada ya siiku chache huanza kurudia mzunguko wake wa kutaga
Wazo zuri sana hili mkuu....Mkuu Asigwa asante sana kudokezea juu ya athari za kuchanganya hawa kuku, bata na kanga, sasa tahadhari itachukuliwa ipasavyo! Kuhusu hayo madawa uliyosema kwa kweli nayo ni changamoto kubwa! Mimi ninachoshauri ni hivi, kila jambo la kitaalamu hutokea baada ya mkereketwa mmoja kufanya ubunifu au utafiti fulani! Inawezekana hakuna anaejua jinsi ya kuchanganya ratio hizo, tuombe Mola muungwana ajitokeze asaidie jambo hili! Vinginevyo fanya hivi Mkuu Asigwa, kwa kila dawa pima dozi yake kama unavyopima inapokuwa peke yake, kisha zichanganye dawa zote kila moja ikiwa imepimwa kwa kipimo cha dose yake, tibia kwa kuku au bata wachache ili usikilizie mziki wake kwanza!! Infact nikuhakikishie kuwa, madawa ya mitishamba (botanicals) inasemwa kwamba ni vigumu sana kuoverdose kama ilivyokwa madawa ya kemikali za viwandani! Inasemwa kwamba inapokuwa overdose kuna-tabia ya mnywaji awe mtu au mnyama yoyote, hutapika na kuepusha dhahama!! Kwahiyo utakapokuwa unafanya jaribio usifanye kwa hofu kabisa hii nakupa ni uzoefu wa kutoka kwa wajuaji wa madawa ya mitishamba.
Jaman najutia kutofuatlia kwa mada hii nw ningeshakuwa tajiri.
Tunakusubili,tunataka kujua na haina kuku nataka kuanza na 30 ila nataka mbegu kubwa kubwa,si unaujuwa kusini kuna maombi ya wawekezaji 40
CC KUBOTA
Safi sana mkuu hii nondo yako ya leo nimeipenda na imenikuna haswaaaaWapendwa wadau wa ujasiliamali JF, nawasilisha kwenu ramani ya ufugaji kuku huria kwenye eneo kubwa. Kwa mfugaji ambaye alieanza kidogo kidogo kisha kundi likapanuka, au kwa mfugaji anayeanza mwenye mtaji mkubwa anaweza kuitumia dizaini hii ili mradi eneo la kutosha lipo! Hapa nimeambatanisha mchoro ambao unaonyesha shamba la kufugia kuku likiwa limezungushiwa fensi inayozuia kuku kutoka nje na kuzuia viumbe maadui wasiingie ndani ya shamba! Inaweza kuwa ni fensi yoyote ya kudumu ambayo ni wavu mpana wa chuma. Ndani ya shamba katikati kuna banda kubwa la kufugia ambalo lina milango minne kama mchoro ulivyoonyesha rangi nyekundu.
Hilo shamba limegawanywa kwenye plots (paddocks) nne yaani A, B, C na D. Hizo plot zenye rangi ya kijani ndiyo malisho yenyewe ambamo kuku huachiwa na kuingia kuchunga kwa mzunguko kama mishale myeupe inavyoonesha. Yaani kuku wanoachiwa ili wachunge kwenye plot A inabidi mlango unaoelekea kwenye ploti A ufunguliwe na ile milango mingine yote inakuwa imefungwa, kwa hiyo kuku wote wataingia na kuchunga ndani ya plot hiyo tu, kunakuwa na fensi ndogo inayohamishika inayowazuia kuku wabaki ndani ya hiyo plot A. Fensi hii inaweza kutengenezwa kwa vifaa mbalimbali ikiwamo, nyasi, matete, mianzi, fito au chicken wire mesh! Baada ya kuwemo eneo hilo kwa siku 10 kuku hutakiwa kuhamishiwa eneo jipya yaani plot B. Ili kufanikisha hilo inabidi ile fensi inayotenganisha Plot A na plot C ihamishiwe na kwenda kutenga Plot B na Plot D kama mchoro unavyoonesha, kisha mlango unaoelekea Plot B ndiyo hutumika kufungulia kuku wakati milango mingine yote iliyobaki inakuwa imefungwa. Baada ya siku 10 tena uhamishaji wa fensi na kuku kwenda plot D hufanyika kwa jinsi ilivyofanyika kama ilivyohamishwa awali.
Banda kubwa hilo lililoko katikati ya shamba linakona nne, kwa ndani kona ya kwanza tengeneza sehemu ya viota vya kutosha kulingana na idadi ya kuku, kona ya pili tengeneza sehemu ya nursery ya kukuzia vifaranga, kona ya tatu tengeneza sehemu ya kuatamisha vifaranga kama mfugaji atakuwa bado hatumiii mashine ya kutotolesha vifaranga na mwisho kona ya nne tengeneza sehemu ya store na JELA. Ukubwa wa hivyo vijisehemu uwe wa kutosha huduma inayotarajiwa na pia iweze kuacha eneo la kutosha kulaza kuku waliopo shambani.
Kwenye mchoro upande wa kushoto kuna lango la kuingilia shambani na barabara (njia) inayopita kando kando mwa fensi ya ndani (mstari wa kahawia)! Kwa vile shambani ni muhimu kuwepo msimamizi au mlinzi au makazi ya mwenye shamba, nyumba yake imeonyeshwa kwa rangi bluu au zambarau, myumba yapaswa ikae langoni ambako wageni wanaweza kuingia na kutoka bila kusumbua kuku kwenye malisho, makazi pia yanapaswa kuwa mbali na mabanda ya kuku kwa sababu za kiafya kwa kuku na binadamu pia.
Eneo la shamba hili linaweza kuwa kuanzia ekari moja na zaidi kulingana na uwezo wa mfugaji! Kadri kuku wanavyozidi kuongezeka mfugaji anaweza kuwa na mabanda mengine yaliyozungukwa na malisho kwa mfano huo na ukubwa wa eneo utaamuliwa na mfugaji husika. Idadi ya kuku kwa ekari moja inaweza kufikia hadi kuku 400 kwa hiyo kama unahitaji kufuga kuku 1000 utahitaji kuwa na eneo la ekari mbili na nusu (Hekta 1).
Mtindo huu unaweza kutumika si kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji pekee bali pia kwa ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai. Ni ufugaji unaopunguza gharama kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo pamoja na kuku kuchunga unapaswa kuweka pia chakula cha ziada na kuna kipindi baadhi ya maeneo wakati wa kiangazi majani yote hukauka wakati huo kwa kiasi kikubwa kuku hutegemea chakula watakacholetewa tu. Vyombo vya kuwawekea vyakula ni vema vikatawanywa sehemu tofauti na kuwekwa chini ya kivuli.
Wadau nawasilisha kwenu dizaini ya eneo la ufugaji mkubwa huria, nakaribisha maswali kwa mwenye kutaka ufafanuzi wowote.
Asigwa ndugu yangu vp umeshapima upepo?naomba mrejeshoWazo zuri sana hili mkuu....
Ngoja nika-mix kwa hiyo ratio ila nahakikisha kwanza na dilute na maji mengi huo mchanganyiko kabla ya kuwapa kuku wangu ili nipime upepo kwanza, ila baada ya muda nakua napunguza ratio ya maji kidogo kidogo mpaka kiwango cha maji ntakachoona kinafaa...
Thaks a lot kwa hili wazo hasa kunifumbua macho kuhusu kutapika...
Thanx Kobota, ubarikiwe zaidi. Mama anakaribia kustaafu ananiambia nimshauri mradi wa kufanya kila unaokuja kichwani naona hatauweza kwa mikiki mikiki yeye kashaziea kushika chaki na kelele za watoto wa primary, lakini hapa naona ni penyewe.
Yaani asubuhi ili litakuwa somolake la kwanza kwani nimeona anao mitetea miwili na vifaranga vitano mayai 11 yaliharibika. Sasa ngoja nimshikie hapa hapa. Asante JF na members wote.
You are highly welcome...JF ni kisima cha elimuThanx Kobota, ubarikiwe zaidi. Mama anakaribia kustaafu ananiambia nimshauri mradi wa kufanya kila unaokuja kichwani naona hatauweza kwa mikiki mikiki yeye kashaziea kushika chaki na kelele za watoto wa primary, lakini hapa naona ni penyewe.
Yaani asubuhi ili litakuwa somolake la kwanza kwani nimeona anao mitetea miwili na vifaranga vitano mayai 11 yaliharibika. Sasa ngoja nimshikie hapa hapa. Asante JF na members wote.