Nina Imani,Naombeni msaada wa kujua gharama za chakula , madawa kwa kuku wa mayai 200 toka vifarnga hadi kutaga na wastani wa trei
Ya kanga?
samahanini wadau napenda kupata ushauri hivi nnao kuku wa kisasa wa mayai miambili hamsini je polo la chakula cha kg 50 nilishie kwa siku ngapi
Nimependa sana na nimekuwa nafatilia sana toka mwanzo sasa nadhani niulize swali na mie.
Napenda fuga kuku wa kienyeji na kisasa ( mayai na nyama).
Eneo lipo kama 1500sqmt.
Maji yapo, umeme swali langu kubwa ni je kwa kuku wa kienyeji 200 kuwafuga hadi kuwauza naweza tumia shilingi ngapi.
Kuhusu wa mayai tayari nimesoma uzi wako na nimeelewa
Nimerudi tena na sasa naanda majibu ya Selmah,Kama kuna mtu still ana swali tutalijadili kwa pamoja.
Msaada plz, nikitaka kupima gram moja, kwa mazingira ya nyumbani natumia kipimo gani?
Nazungumzia chakula.Englishlady,
Kupata kipimo cha gram moja kama gram moja ni ngumu ila kwa dawa nyingi za kuku tunaanza na kipimo cha gram tano ambacho ni sawa na kijiko kidogo kimoja cha chai. Kile kijiko kikubwa cha chakula ni gram 10 ikiwa kimejaa dawa.
Englishlady,Nazungumzia chakula.
Ndugu Aman,
Nimefuatilia mjadala kwa ukaribu sana, naomba niulize maswali machache kama ifuatavyo,
Nampango nianze kufuga kuku 1000 wa mayai, shamba lipo sehemu ambayo haina umeme. Unanishauri nitumie nini ili waweze kupata joto wanalostahili?
Wakianza kutaga nitegemee mayai mangapi kwa siku?
Wapi naweza kupata vifaranga bora?
Naomba unitumie contacts zako kwenye PM, tuwezekuongea zaidi
Ndugu yangu emma250,
Umeme si kikwazo katika ufugaji wa kuku wa mayai. Kwa ajili ya joto unaweza kutumia majiko ya mkaa. Kwa vifaranga wa mayai wao huitaji joto na mwanga zaidi katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo baada ya hapo hawahitaji tena. Kwa ajili ya mwanga utatumia taa za kandili.
Baada ya wiki tatu usiwashie taa wala majiko hadi watakapochoka kutaga.
Kuku wa mayai 1000 wakianza kutaga,wakiwa kwenye kilele cha utagaji hufikia asilimia hadi 94 ya kuku wote itategemea na utunzaji.
Vifaranga bora wanapatikana Njombe kuna kampuni moja inaitwa matembwe village co Ltd.
Asante
Kwa wale wafugaji ambao tayari wamekwisha kuanza ufugaji wa kuku,leteni changamoto zenu tutawasadia kusudi msonge mbele.Sisi ni mkusanyiko wa wataalam wa mifugo by professional lkn pia ni wazoefu wa muda mrefu kwenye hii kada.Pia tuna watu waliobobea kwenye maandiko ya uanzishwaji wa mradi(Project write up) na mpango wa biashara yaani Business plan
Kwa wafugaji waliojikusanya pamoja wanaweza kuwasiliana nasi tukawapa mafunzo ya namna ya ufugaji bora,si tu wa kuku ni kwa mifugo yote.Tutawaeleza kwa uwazi na ufasaha mkubwa wa namna ya kutengeza pesa kupitia ufugaji.Watanzania bila umasikini inawezekana.
Sisi tuko Morogoro,chuo kikuu cha kilimo Sua,but tuko movable kulingana na mahitaji ya anayetaka kuanzishiwA MRADI.
Kumbuka kuanzisha mradi bila kuwa na elimu yake ni sawa na kutembea huku ukiwa umefumba macho.
Aman,
Asante kwa majibu yako,naomba niulize maswali mengi,
Kwa ujuzi wako ule moshi wa majiko ya mkaa hauwadhuru vifaranga?
Kwa kukadiria kuku 1000, wataitaji majiko mangapi na taa ngapi?
Kuna mabanda special kwa ajili ya kutunza vifaranga au wanaweza wakakaa kwenye banda la kawaida?
Kwa experience yako nikianza na kuku 1000 naeza nikaexpect vifo yaani normal loss ya vifaranga wangapi kama vifaranga vikifugwa kiutaalam?
Siku hizi trei moja ya mayai inauzwa kwa shs ngapi?
Asante kwa ushirikiano wako.