Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Jamani mimi ni mfugaji pia ila naomba kaushauri..nilikua napata oda ya bata mzinga. ikabidi niwaanze sasa wamefika 12 wakubwa bado bado wengine wataanguliwa karibuni sasa suala la bei ndo linanichanganya kwani nikijaribu kuuliza kwa wanaofuga wananichanganya madaktar nao vilevile kila mtu ananiambia bei yake sasa nimepata oda hapa shoprite Arusha bata mzinga 4 kuna anaefika kg 25 niuze vip maana wao wananiambia elf 70??
 
Naombeni msaada wa kujua gharama za chakula , madawa kwa kuku wa mayai 200 toka vifarnga hadi kutaga na wastani wa trei
Nina Imani,
Kuku wa mayai ni kuku maalum aliyetokana na kuku wazazi.Kuku hawa kazi yao kubwa ni kutaga mayai.

Hebu sasa tuangalie gharama za chakula,madawa nk ambazo mfugaji ataingia kwa kumfuga kuku wa mayai mmoja toka kifaranga hadi anaanza kutaga na mpaka atakapochoka kutaga.

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 375"]
[TR]
[TD] MAHITAJI
[/TD]
[TD] GHARAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Chakula
[/TD]
[TD] 39860/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Madawa
[/TD]
[TD] 16800/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Box za kutagia
[/TD]
[TD] 3160/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Kifaranga 1
[/TD]
[TD] 2500/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Mshahara wa mfanyakazi kwa kuku
[/TD]
[TD] 2000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Vilishio
[/TD]
[TD] 400/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Vinywesheo
[/TD]
[TD] 250/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Gharama ya Vifo inayobebwa na kuku mmoja
[/TD]
[TD] 150/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Jumla ya kumfuga kuku 1 wa Mayai
[/TD]
[TD] 65120/=
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 375"]
[TR]
[TD] FAIDA
[/TD]
[TD] IDADI
[/TD]
[TD] TSHS
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Mayai
[/TD]
[TD] 435
[/TD]
[TD] 108750/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Kuku aliyechoka kutaga
[/TD]
[TD] 1
[/TD]
[TD] 8000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Samadi
[/TD]
[TD] 70kg
[/TD]
[TD] 5000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Jumla ya Faida
[/TD]
[TD][/TD]
[TD] 121750/=
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

FAIDA KAMILI=120750-65120= 56630/=
Hii ni kwa kifupi tu, kwa kirefu inahitaji kuandika mchanganua wa mradi kamili uanaoanisha pesa zinazoingia na kutoka nk.
 
  • Thanks
Reactions: YJS
Mkuu Zantsan nimependa sana shule uliyoitoa, nimefuatilia kwa umakini. Tafadhali naomba uni pm contact zenu kwa maulizo zaidi.
 
Asante sana kwa taarifa nzuri sana , nimejifunza kuwa kumbe kwa kuku 200 naweza kupata faida kubwa sana , Ubarikiwe.
 
Mahitaji ya kuku wa mayai 1000
  1. Hapa utahitaji uwe na mfanyakazi mmoja ambaye utamlipa mshahara wa shilingi 100 kwa kuku mmoja kwa mwezi.
  2. Vilishio (Feeders) za mzunguko 50
  3. Vinyesheo (Drikers) 15
  4. Boksi za kutagia (Nest Box) 20
  5. Bembea(Perches) 25
  6. Ardhi eneo la 150mx 120m,

  • 15m x 8m Nyumba ya kuku inayotosha kuku 1000
  • 8m x 4m kwa ajili ya ujenzi wa nyumba Mfanyakazi au maneja wa Mradi.
  • 3.5m x 3m kwa ajili ya ujenzi wa choo
  • 4m x 4m kwa ajili ya ujenzi wa stoo ya kuhifadhia chakula, madawa, mayai, trai za mayai, nk

Nimependa sana na nimekuwa nafatilia sana toka mwanzo sasa nadhani niulize swali na mie.
Napenda fuga kuku wa kienyeji na kisasa ( mayai na nyama).
Eneo lipo kama 1500sqmt.
Maji yapo, umeme swali langu kubwa ni je kwa kuku wa kienyeji 200 kuwafuga hadi kuwauza naweza tumia shilingi ngapi.
Kuhusu wa mayai tayari nimesoma uzi wako na nimeelewa
 
jaman samahan napend kuulza,nna kuk wang wa mayai wana miez 5 na wik 3 lakn hawajaanz kutaga bali wanatetea tu,tatzo linawez kuwa nn?!
 
samahanini wadau napenda kupata ushauri hivi nnao kuku wa kisasa wa mayai miambili hamsini je polo la chakula cha kg 50 nilishie kwa siku ngapi

Kuku wako wana umri gani? Kiasi cha ulishaji hutofautiana kulingana na umri wa kuku...
(Polo) nafikiri unazungumzia mfuko wa chakula wa kg 50?
 
Nimependa sana na nimekuwa nafatilia sana toka mwanzo sasa nadhani niulize swali na mie.
Napenda fuga kuku wa kienyeji na kisasa ( mayai na nyama).
Eneo lipo kama 1500sqmt.
Maji yapo, umeme swali langu kubwa ni je kwa kuku wa kienyeji 200 kuwafuga hadi kuwauza naweza tumia shilingi ngapi.
Kuhusu wa mayai tayari nimesoma uzi wako na nimeelewa

Mara nyingi gharama za kufuga kuku wa kienyeji hutegemea na mfumo wa ufugaji utakaotumia kama ni wa ndani tu,nusu ndani nusu nje au nje tu. Pia itategemea idadi hiyo ya kuku wa kienyeji utataka kuwauza wakiwa na umri gani?
 
Wana JF
Nmepata ushauri kutoka kwa wafuatiliaji wa mada zangu kuwa nitumie jina langu halisi ili kuwarahisishia kulitamka na kunifahamu hivyo nimesikia ushauri wao na nimetekeleza hivyo jina langu halisi ni Aman Ng'oma ndio jina langu halisi ambalo nitakuwa nilitumia kuanzia leo na kuendelea.Asante kwa ushirikiano wenu. Nakumbuka hii ni mara yangu ya tatu kubadilisha jina mwanzo nilitumia Kichwa mbovu,nikashauriwa nibadilishe, nikaja na Zantsan pia nimeshauriwa nibadilishe na sasa nimekuja kwa jina langu halisi.
Maada inaendelea, karibu sana.
 
Msaada plz, nikitaka kupima gram moja, kwa mazingira ya nyumbani natumia kipimo gani?

Englishlady,
Kupata kipimo cha gram moja kama gram moja ni ngumu ila kwa dawa nyingi za kuku tunaanza na kipimo cha gram tano ambacho ni sawa na kijiko kidogo kimoja cha chai. Kile kijiko kikubwa cha chakula ni gram 10 ikiwa kimejaa dawa.
 
Nazungumzia chakula.
 
Nazungumzia chakula.
Englishlady,
Ok nimekupata bibie, kwa chakula hupaswi kupima kwa gram moja moja isipokuwa inatakiwa kujua kwamba kuku mmoja anakula gram ngapi kwa siku kisha unazidisha mara idadi ya kuku utapata jumla ya gram ambazo kuku atakula kwa siku then utabadilisha gram kwenda kwenye kilogram.

Kwa mfano kifaranga mmoja wiki ya kwanza kwa siku atahitaji grm 12.Ukiwa na vifaranga 100 ile wiki ya kwanza kila siku watahitaji gram 1200 sawa na kilo 1.2. Kilo 1.2 ni rahisi kuipima. Sijui kama nitakuwa nimekuridhisha.
 
Ndugu Aman,
Nimefuatilia mjadala kwa ukaribu sana, naomba niulize maswali machache kama ifuatavyo,

Nampango nianze kufuga kuku 1000 wa mayai, shamba lipo sehemu ambayo haina umeme. Unanishauri nitumie nini ili waweze kupata joto wanalostahili?

Wakianza kutaga nitegemee mayai mangapi kwa siku?

Wapi naweza kupata vifaranga bora?

Naomba unitumie contacts zako kwenye PM, tuwezekuongea zaidi
 
Ndugu yangu emma250,
Umeme si kikwazo katika ufugaji wa kuku wa mayai. Kwa ajili ya joto unaweza kutumia majiko ya mkaa. Kwa vifaranga wa mayai wao huitaji joto na mwanga zaidi katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo baada ya hapo hawahitaji tena. Kwa ajili ya mwanga utatumia taa za kandili.

Baada ya wiki tatu usiwashie taa wala majiko hadi watakapochoka kutaga.

Kuku wa mayai 1000 wakianza kutaga,wakiwa kwenye kilele cha utagaji hufikia asilimia hadi 94 ya kuku wote itategemea na utunzaji.

Vifaranga bora wanapatikana Njombe kuna kampuni moja inaitwa matembwe village co Ltd.
Asante
 
Aman,
Asante kwa majibu yako,naomba niulize maswali mengi,

Kwa ujuzi wako ule moshi wa majiko ya mkaa hauwadhuru vifaranga?

Kwa kukadiria kuku 1000, wataitaji majiko mangapi na taa ngapi?

Kuna mabanda special kwa ajili ya kutunza vifaranga au wanaweza wakakaa kwenye banda la kawaida?

Kwa experience yako nikianza na kuku 1000 naeza nikaexpect vifo yaani normal loss ya vifaranga wangapi kama vifaranga vikifugwa kiutaalam?

Siku hizi trei moja ya mayai inauzwa kwa shs ngapi?

Asante kwa ushirikiano wako.
 
Kwa wale wafugaji ambao tayari wamekwisha kuanza ufugaji wa kuku,leteni changamoto zenu tutawasadia kusudi msonge mbele.Sisi ni mkusanyiko wa wataalam wa mifugo by professional lkn pia ni wazoefu wa muda mrefu kwenye hii kada.Pia tuna watu waliobobea kwenye maandiko ya uanzishwaji wa mradi(Project write up) na mpango wa biashara yaani Business plan
Kwa wafugaji waliojikusanya pamoja wanaweza kuwasiliana nasi tukawapa mafunzo ya namna ya ufugaji bora,si tu wa kuku ni kwa mifugo yote.Tutawaeleza kwa uwazi na ufasaha mkubwa wa namna ya kutengeza pesa kupitia ufugaji.Watanzania bila umasikini inawezekana.

Sisi tuko Morogoro,chuo kikuu cha kilimo Sua,but tuko movable kulingana na mahitaji ya anayetaka kuanzishiwA MRADI.
Kumbuka kuanzisha mradi bila kuwa na elimu yake ni sawa na kutembea huku ukiwa umefumba macho.

mimi nauliza ni sahihi kuwapa Kuku chotara dagaa na pumba za mahindi tu
 
Aman,
Asante kwa majibu yako,naomba niulize maswali mengi,

Kwa ujuzi wako ule moshi wa majiko ya mkaa hauwadhuru vifaranga?

Kwa kukadiria kuku 1000, wataitaji majiko mangapi na taa ngapi?

Kuna mabanda special kwa ajili ya kutunza vifaranga au wanaweza wakakaa kwenye banda la kawaida?

Kwa experience yako nikianza na kuku 1000 naeza nikaexpect vifo yaani normal loss ya vifaranga wangapi kama vifaranga vikifugwa kiutaalam?

Siku hizi trei moja ya mayai inauzwa kwa shs ngapi?

Asante kwa ushirikiano wako.

emma250,
Asante kwa maswali yako mazuri. Kwakifupi ni kwamba, moshi unawaathiri vifaranga kama ambayo huwaathiri binaadamu
kitu cha msingi unapaswa kuhakikisha kuwa yale majiko yanakolezwa nje ya chumba cha vifaranga yakishakolea vyema yanayaingizwa ndani hivyo yanakuwa hayana tena moshi lakini pia ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata mkaa mzuri maana mikaa mingine inakuwa na matatizo ya kutoa moshi.

Majiko 4 yanatosha kwa kuku hao 1000. Vilevile unapaswa uwe na vyumba viwili tofauti vya kuwalelea vifaranga hao kila chaumba kibebe vifaranga 500 na baada ya mwezi mmoja wawekwe kwenye vyumba 4 tofauti kila chumba kikibeba kuku 250. Nyumba itakayotosha kuku hao 1000 inatakiwa iwe yenye ukubwa wa 15m kwa 8m, kisha utaigawa katika vyumba vinne vilivyo sawa.

Ukifuga kwa kufuata kanuni na misingi ya ufugaji bora vifo vinakuwa ni 5%. Ingawa bado inalipa kibiashara hata vifo vikifika 10% ya kuku wote walioagizwa. Vifo zaidi ya asilimia kumi ni ishara ya kukosa umakini katika uleaji na utunzaji wa vifaranga na hivyo kupunguza faida. Kama utafuata ushauri kutoka kwa mtaam aliyesomea taaluma ya mifugo bila shaka utafanya vizuri katika ufugaji wako wa kuku na hata faida ufugaji itaonekana.

Katika uleaji wa vifaranga huwa tunatengeneza chumba maalum kwa ajili ya kulelea vifaranga hasa katika zile wiki tatu za mwanzo ambapo vifaranga wanahitaji joto kwa kiasi kikubwa ili kuwakinga dhidi ya baridi. Chumba hicho huitwa brooder. Brooder inaweza kutengenezwa kwa sealing board inayojikunja au chumba cha kawaida kinaweza kutumika kama brooder isipokuwa zile kona za chumba zitapaswa kuondolewe kwa kutengeneza vibao maalum ambavyo vitaondoa kona, ukiwasiliana na mafundi selemala watakusaidia.

Bei ya trai moja ya mayai kwa sasa ni tsh 7500 kwa jumla na tsh 9000 kwa bei ya rejareja, itategemea pia na mahali ulipo.

Asante.
 
Back
Top Bottom