1. Usipoanza kuwa mjasiriamali utabaki kusema "sijawahi kuwa mjasiriamali". Una wazo zuri sana, kuku wa kienyeji wana soko kubwa ukilinganisha na wa kisasa.
2. Jibu la swali hili linapatikana kwenye jibu la swali la kwanza hapo juu.
3. Kuna watu wengi wanafanya biashara ya kununua kuku mikoani na kusafirisha kupeleka Dar Es Salaam kwahiyo kama utakua unazalisha kwa wingi utakua umewarahisishia wao kupunguza gharama za kukusanya mzigo huko minadani na kwa wafugaji wadogo wadogo watakua wanakua wanachukua kwako. Consistency yako katika kuzalisha na reliability yako ndio itakua silaha yako kuwafanya wafanye biashara nawewe.
4. Ili kujibu ni sahihi au sio sahihi kumuweka nduguyo au kuajiri mtu, ni lazima ujiridhishe na uaminifu, uchapa kazi pamoja na maslahi yake pia ndugu au mwajiriwa. Yeyote anaye meet hayo hapo juu muweke na utakua uko sahihi.
5. Hii itategemea na kiasi ulichokitenga kwa ajili ya huu mradi wako wa ufugaji (umeeleza tu kipato chako cha mwezi).
6. (Hii kwako haipo), Mimi binafsi ninatamani sana ufanikiwe katika mradi wako, Mungu akubariki na akufanyie wepesi katika kukabiliana na changamoto zozote zinazojitokeza katika ufugaji.
Kila lililo jema.