Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa watalaamu na wafugaji wazoefu.
Nini kuku wale weusi (black Australorp) . wako wiki ya 5, nilianza nao 130 na sasa wamebaki 90 maana wanakufa karibu kila siku lazima afe mmoja au wawili. wanaanza kuvimba macho na hatimaye kufa. Daktari alisema ni ukosefu wa vitamini. nimewapa vitamin aina ya Introvit A pamoja na dawa ya typhoid lakini wapi. wanaendelea kufa tu!!
Hebu nipeni maoni, huo unaweza kuwa ugonjwa gani maana naona sijapata dawa muafaka. naambatanisha picha!!
Digna thanks kwa ushauri wako. nimeenda kwa mtaalamu mmoja kanipa antibiotic Tylosin 75% ndo nawapa pamoja na Oligovit.
thanks a lot kwa ushauri wa kuwasafisha macho. nitafanya hivyo then nitatoa feedback.
Mambo yalikwendaje Kanyagio?


Haya let me share with you some graphs of my poultry project. hii ni project iliyoanza mwezi wa August 2011 kwa kuku 630 layers. mnano mwezi wa 9 mwishoni tuliongeza kuku wengine 450. kuku wa awamu ya kwanza walianza kutaga tarehe 1 December 2011 na hawa wa phase 2 walianza kutaga tarehe 1 February 2012. kwa ujumbla walikufa kuku kama 80 na hivyo tumebakiwa na kuku 1000.
Kumbuka mabanda nimeyakodisha na nalipa hela kidogo kidogo. ila mabanda haya niliyafanyia renovations. ufugaji unafanyikia Dar es salaam. December na january mwanzoni soko lilikuwa zuri maana tuliuza tray kwa 6500 hadi 7000/= ila sasa limeshuka kwa sababu trei ni Tsh 5500. Chakula (layers mash) kimepanda kutoka 32500/= kwa mfuko wa 50kg hadi 34500/=. ila hatukati tamaa.
View attachment 50000
View attachment 50001
mwenye utaalamu wa kukuza image anisaidie
Mpaka sasa umepata faida au vipi? Umeeleza kwamba mradi mpaka ulipofikia umegharimu milioni ishirini, total revenue milioni saba, na net revenue milioni kumi na tatu. Je, faida kiasi gani?
Nipo Dar nataka nianze biashara hii ya kuku wa mayai ila nataka kijana mtaalam mwenye uzoefu naweza mpata wap? na maeneo mazuri ya kuweka banda ni wap nina plot bagamoyo kma heka 2 na plot ya "20 kwa 30" Goba panafaa kujenga banda la kuku 2000?
Ujenzi wa banda la kuku wa mayai (kuku 2000) linagarimu kiasi gani cha fedha? mchoro stracture yake naweza ipata wap la kisasa na economical! ntashukuru kwa majibu yenu