Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Nguruwe kuwa mkubwa na kilo nyingi lakini ndani ana mafuta kuliko Steak inasababishwa na nini?

Je ni Chakula anachokula kila siku au ni aina ya Nguruwe(Breed) ndio inafanya wawe hivyo.

Kwa wale ambao mnakula nguruwe mtakubaliana na Mimi kwamba Nguruwe mzuri ni yule mwenyewe mafuta kidogo na nyama nyingi naamini hata wachinjaji inawapa faida zaidi akichinja nguruwe mwenye nyama nyingi na mafuta kidogo

Sasa Je mfugaji afanye nini ili Nguruwe wake wawe na Kilo nyingi lakini zenye nyama pamoja na mafuta machache maana unaweza kumuona Nguruwe mkubwa kwa mwili na kilo nyingi lakini akichinjwa unakuta mafuta ni mengi mno kuliko nyama kitu ambacho walaji hawapendi.

Naamini hata wachinjaji wanapenda zaidi Nguruwe wa aina hii maana anawapatia faida zaidi,

Naombeni majibu wadau,sikumoja napenda nifuge hawa wanyama

Ahsante
 
navyojua ni ratio ya chakula unachompa inawezekana anakula (protein+carbs+fats)kwa wingi sana .
hapa inabid upunguze ratio ya chakula.wengi hawajui mnyama ni kama binadamu kwaiyo kwa kutaka kujua ni kwann nguruwe anamafuta mengi kuliko stake bac at the same time jiulize kwann pia binadamu ana kuwa mnene kupindukia,nadhani ukiweza kujua ni kwa nn bac utakuwa umepata majibu mazuri zaidi.
 
Mkuu sijaanza kufuga bado ila najaribu kujiuliza mambo ya msingi ili wafugaji waelewa wanipe somo maana hiki kitu nimeshakutana nacho,nashukuru kwa mchango wako
 
Post inatamanisha sana ushauri wangu: Kama umeamuakufuga kama hivyo basi jitahidi angalau 90% ya muda wako upo hapo na ukubali kupigika hasa kutokana na changamoto utakazokutana nazo. Kadri unavyopambana na hizo changamoto ndivyo utakavyokua unaelekea kwenye mafanikio
 
Hivi inafaa kwaogesha kwa dawa ya kuua kupe(maarufu..dipu) kama ng'ombe,mbuzi nk ili kuua viroboto..wanajisugua ukutani
 
Hakika jukwaa hili ni SULUHISHO,, mimi ni ufugaji wa nguruwe nimeanza mwaka huu mwezi wa 5 na nimeanza na majike 25 tayari 10 wana mimba ,, nategemea kuuza nguruwe 100 kila mwezi wadogo kwa wakubwa,, nina eneo la hekari mbili maeneo ya kerege bagamoyo,, nimelima migomba, maboga kwa ajili ya chakula cha ziada, nawapa mchanganyiko wa Pumba za mchele, pumba za mshindi, mashudu ya alizeti, chumvi,pig mix,, nawaona wakiwa na afya njema sanaa.Wale wenzangu tujuzane masoko serious!!
 
Yan tz sjui tunafeli wap yan hakuna daraja kati wa wataalamu na wafugaji au wakulima matokeo yake ndo kama haya mfugaji anaweza kua anatumia expenses nyingi kwenye ufugaji na faida anapata ndogo ufagaji mzuri ni ule wenye tija production cost ndogo na kupata faida kubwa

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Habari wakuu, mimi ni mfugaji nipo Mwanza, nauza nguruwe watoto na wakubwa kwa ajili ya kufugwa, napatikana Mwanza nitafute kwa namba hizi 0719832015
Karibuni sana
 
Mkuu unamia chakula kiasi gani kuwalisha hao nguruwe 25 kwa mwezi (kilogramu ngapi) na je ni wakubwa kabisa?
 
Nimeanza na majike mawili mwezi huu tar 10 /8/2021 mungu akilijalia ntanunua wengine wa 3 ili jumla wawe 5,nilikuwa naangalia YouTube kuna shamba LA nguruwe linaitwa DAIICHI FARM jinsi anavyo ongeza thaman ya nyama yake kutoka shambaa mpaka kuwa na kakiwanda ka kupack na kutengeneza sausage ............. Nikifika level za kuwa na nguruwe 50 nadhan ntapata moyo zaidi na hii SIDE HUSTLE
 
Ili kupunguza mafuta mengi kwa nguruwe jitahidi kumpa majani mengi na pia tumia kiasi kikubwa cha pumba za mpunga katika mchanganyiko wa chakula chao kuliko pumba za mahindi
Hapa utapata nyama nyingii mafuta kidogo
 
Je kuharisha kwa piglets kunaweza sababishwa na maziwa ya sow kama hakupata matibabu na chanjo stahiki kabla ya kubeba mimba?
Mama akiwa anatoa maziwa yenye vimelea vya ugonjwa ndio watoto huharisha .........hapa Fanya kutumia dawa zenye sulphur kuwatibu au changanya kiasi cha chakula chao ( creep feeds na antibiotic za unga zenye sulphur ) lakin muhimi kuzingatia usafi pia
 
Ili kupunguza mafuta mengi kwa nguruwe jitahidi kumpa majani mengi na pia tumia kiasi kikubwa cha pumba za mpunga katika mchanganyiko wa chakula chao kuliko pumba za mahindi
Hapa utapata nyama nyingii mafuta kidogo
Asante
 
Nimekuwa interested sana na ushauri wako nami ningependa kujaribu hilo deal. Jambo moja linanisumbua ni jinsi ya kupata sehemu ya kufugia, kama kuna mtu ana idea mashamba ya bei nafuu pembezoni mwa Dar es salaam naomba msaada.
Mimi nina eneo kubwa tu Vigwaza pale, tuingie ubia au kama utataka kununua
 
Mimi nina wazo hili miaka mingi, nina mtaji wa eneo kama eka moja na ushee kule Vigwaza, linatosha kabisa kuhifadhi nguruwe hata mia
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ulifanikiwa kumtembelea?
 
Ulifanikiwa kumtembelea?
Ni muda umepita mkuu hata sikumbuki vzr hii thread. Ila ni Amoeba ndiyo alikuwa ana mpango wa kumtembelea mfugaji mkubwa wa nguruwe Iringa ninadhani. Na mm ndiyo nilisema nikipata mrejesho toka kwake ndiyo ningepanga hiyo safari pia. Sikumbuki kama nilipata huyo mrejesho toka kwa mkuu Amoeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…