Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ni muda umepita mkuu hata sikumbuki vzr hii thread. Ila ni Amoeba ndiyo alikuwa ana mpango wa kumtembelea mfugaji mkubwa wa nguruwe Iringa ninadhani. Na mm ndiyo nilisema nikipata mrejesho toka kwake ndiyo ningepanga hiyo safari pia. Sikumbuki kama nilipata huyo mrejesho toka kwa mkuu Amoeba.
Amoeba mwenyewe sijui kama yupo hai kitambo sana hajaingia, since 2013
 
Amoeba mwenyewe sijui kama yupo hai kitambo sana hajaingia, since 2013
Duh muda sana ila anaweza kuwa hai labda kapumzika tu JF. By then project yake kwa mujibu wa maelezo yake ilikuwa iko njema sana. Jaribu kumpm tumsikie kama bado anaendelea ama lah.
 
Mimi ni mfugaji kwa miaka minne sasa Avatar yangu inanitambulisha pia. Sijaona faida ya mnyama huyo isipokuwa hasara. Ana gharama za malisho na rahisi sana kudumaa...Kwa ufupi hachelewi kukosewa katika ukuaji.

Unaweza kujaribu ukajionea mwenyewe ingawa wengi humu ambao hawafugi watakuja kukupa ushauri wa kwenye vitabu.
Mimi kwa sasa nafuga kama huduma si faida tena kwakuwa mabanda nilishayajenga ya kisasa hayawezi kukaa hivi hivi.
Nguruwe anaeweza kuzaa watoto 10 hadi 30 kwa mwaka mmoja unasema n hasara?? Pole sana
 
Hakika jukwaa hili ni SULUHISHO,, mimi ni ufugaji wa nguruwe nimeanza mwaka huu mwezi wa 5 na nimeanza na majike 25 tayari 10 wana mimba ,, nategemea kuuza nguruwe 100 kila mwezi wadogo kwa wakubwa,, nina eneo la hekari mbili maeneo ya kerege bagamoyo,, nimelima migomba, maboga kwa ajili ya chakula cha ziada, nawapa mchanganyiko wa Pumba za mchele, pumba za mshindi, mashudu ya alizeti, chumvi,pig mix,, nawaona wakiwa na afya njema sanaa.Wale wenzangu tujuzane masoko serious!!
Hongera sana mkuu kwa hatua , ukienda vizuri kwenye kizazi cha tatu tayar utakua na hao 100 kwa mwez .. na ambayo sio safari ndefu sana, miaka miwil na nusu mitatu
 
Habarini za mwaka mpya wana Jf!
Baada ya muda mrefu kuto post makala humu (nimekuwa busy kwenye media zingine kama instagram, utube,whatsap,telegram..),acha leo nichangie kidogo maana nimeona post nyingi kuhusu ufugaji nguruwe zenye mapungufu. Wakongwe wa Jf watanikumbuka maana nime post sana makala za ufugaji humu miaka hadi kumi iliyopita.
Ufugaji nguruwe kibiashara sio rahisi ila unawezekana.Ugumu unakuja kwa sababu ni biashara na biashara zote zina kanuni ili kujipa uwezekano wa kufanikiwa. Ili uweze kufanikiwa katika ufugaji nguruwe kuna maeneo makubwa mawili:
A.Uzalishaji
Uzalishaji wenye tija unategemea mbegu na matunzo. Matunzo ni mambo yanayohusisha mazingira ya kuishi wanyama, lishe sahihi, chanjo/tiba na utarartibu wa kuzuia magonjwa kuingia kwenye mradi.
B. Masoko
Hakuna namna mradi wako utadumu bila kuuza bidhaa zako. Biashara yoyote haiwezi kudumu kama hakuna mauzo. Wafugaji wengi huanza ufugaji bila kufanya utafiti wa soko na miradi yao hukwama

Hivyo kama unataka kufanya biashara kwenye ufugaji nguruwe chukua hatua hizi
1. Tafiti kuhusu ufugaji nguruwe kupitia machapisho mbalimbali kam vitabu,makala mitandanoni kama google,instagram na utube.
Hii itakusaidia kuuelewa ufugaji na changamoto/fursa zilizopo.

2. Pata ushauri toka kwa wafugaji wazoefu. Kuna faida kukutana ana kwa ana na mtu mwenye uzoefu kwenye ufugaji ukaweza kujadili nae na kujifunza mambo muhimu. Hata kama utahitajika kulipia huduma hiyo fanya.Ni muhimu sana kwako

3. Tafiti kuhusu soko la bidhaa za nguruwe. Hapa fanya utafiti wewe binafsi ndugu,usitegemee maneno ya kuambiwa. Soko la bidhaa za nguruwe lipo ila haina maana soko la bidhaa zako wewe lipo linakungoja!!

4. Amua bidhaa utakazozalisha na weka malengo kulingana na soko la bidhaa zako

5.Anza mradi kwa kuongozwa na mshauri mzoefu. Kila kitu kinategemea malengo yako:aina ya mbegu,ukubwa wa mradi,soko......

#Malafyale Farms tuna makala mbalimbali pia kwenye ukurasa wetu wa instagram: https://instagram.com/malafyalepigfarms?igshid=4koq1jc1dabp

Ni waandishi pia wa kitabu cha ufugaji nguruwe cha kiswahili rahisi kwa kila mtanzania 'Kanuni za Ufugaji Nguruwe wenye tija'

Waweza wasiliana nasi kwa 0789412904/0754393838 kwa simu au whatsap. Tusipopokea andika ujumbe tutakupigia.
 
Hakika jukwaa hili ni SULUHISHO,, mimi ni ufugaji wa nguruwe nimeanza mwaka huu mwezi wa 5 na nimeanza na majike 25 tayari 10 wana mimba ,, nategemea kuuza nguruwe 100 kila mwezi wadogo kwa wakubwa,, nina eneo la hekari mbili maeneo ya kerege bagamoyo,, nimelima migomba, maboga kwa ajili ya chakula cha ziada, nawapa mchanganyiko wa Pumba za mchele, pumba za mshindi, mashudu ya alizeti, chumvi,pig mix,, nawaona wakiwa na afya njema sanaa.Wale wenzangu tujuzane masoko serious!!
Majike 25 gharama za kuwalisha zikoje hapa mkuu?
 
Hii system ya mabanda na ulishaji inapatikana wapi
Screenshot_20220218-220031.jpeg
 
Uko sahihi sana Mkuu, hii ni kwa wale walio committed tu, kwa less committed sijajua biashara wanayoweza kufanya kilelemama n a ukapata pesa!..hii ni kutokana na uzoefu wangu, ukiwaachia wafanyakazi kufanya kila kitu utakuta wameuza madawa na nguruwe wote wanakufa, hii ni ngumu kwa vijana wa sasa hamuwezi kupiga mswaki nguruwe!
Kuna kupiga mswaki nguruwe,Mkuu?
 
Leteni mrejesho wadau
Biashara hii ni ngumu sana. Mnunuzi akija bandani kuangalia nguruwe wako bei anayokutajia utachoka. Nguruwe likubwa na ni hybrid anakwambia anakupa laki 4. Natamani ningekua na kijiwe changu mwenyewe niwe nachinja na kuuza mwenyewe kuliko unafuga halafu mwisho wa siku unamsubiria mnunuzi aje na bei za kikolo..
 
Back
Top Bottom