Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Amoeba mwenyewe sijui kama yupo hai kitambo sana hajaingia, since 2013
 
Amoeba mwenyewe sijui kama yupo hai kitambo sana hajaingia, since 2013
Duh muda sana ila anaweza kuwa hai labda kapumzika tu JF. By then project yake kwa mujibu wa maelezo yake ilikuwa iko njema sana. Jaribu kumpm tumsikie kama bado anaendelea ama lah.
 
Nguruwe anaeweza kuzaa watoto 10 hadi 30 kwa mwaka mmoja unasema n hasara?? Pole sana
 
Hongera sana mkuu kwa hatua , ukienda vizuri kwenye kizazi cha tatu tayar utakua na hao 100 kwa mwez .. na ambayo sio safari ndefu sana, miaka miwil na nusu mitatu
 
Habarini za mwaka mpya wana Jf!
Baada ya muda mrefu kuto post makala humu (nimekuwa busy kwenye media zingine kama instagram, utube,whatsap,telegram..),acha leo nichangie kidogo maana nimeona post nyingi kuhusu ufugaji nguruwe zenye mapungufu. Wakongwe wa Jf watanikumbuka maana nime post sana makala za ufugaji humu miaka hadi kumi iliyopita.
Ufugaji nguruwe kibiashara sio rahisi ila unawezekana.Ugumu unakuja kwa sababu ni biashara na biashara zote zina kanuni ili kujipa uwezekano wa kufanikiwa. Ili uweze kufanikiwa katika ufugaji nguruwe kuna maeneo makubwa mawili:
A.Uzalishaji
Uzalishaji wenye tija unategemea mbegu na matunzo. Matunzo ni mambo yanayohusisha mazingira ya kuishi wanyama, lishe sahihi, chanjo/tiba na utarartibu wa kuzuia magonjwa kuingia kwenye mradi.
B. Masoko
Hakuna namna mradi wako utadumu bila kuuza bidhaa zako. Biashara yoyote haiwezi kudumu kama hakuna mauzo. Wafugaji wengi huanza ufugaji bila kufanya utafiti wa soko na miradi yao hukwama

Hivyo kama unataka kufanya biashara kwenye ufugaji nguruwe chukua hatua hizi
1. Tafiti kuhusu ufugaji nguruwe kupitia machapisho mbalimbali kam vitabu,makala mitandanoni kama google,instagram na utube.
Hii itakusaidia kuuelewa ufugaji na changamoto/fursa zilizopo.

2. Pata ushauri toka kwa wafugaji wazoefu. Kuna faida kukutana ana kwa ana na mtu mwenye uzoefu kwenye ufugaji ukaweza kujadili nae na kujifunza mambo muhimu. Hata kama utahitajika kulipia huduma hiyo fanya.Ni muhimu sana kwako

3. Tafiti kuhusu soko la bidhaa za nguruwe. Hapa fanya utafiti wewe binafsi ndugu,usitegemee maneno ya kuambiwa. Soko la bidhaa za nguruwe lipo ila haina maana soko la bidhaa zako wewe lipo linakungoja!!

4. Amua bidhaa utakazozalisha na weka malengo kulingana na soko la bidhaa zako

5.Anza mradi kwa kuongozwa na mshauri mzoefu. Kila kitu kinategemea malengo yako:aina ya mbegu,ukubwa wa mradi,soko......

#Malafyale Farms tuna makala mbalimbali pia kwenye ukurasa wetu wa instagram: https://instagram.com/malafyalepigfarms?igshid=4koq1jc1dabp

Ni waandishi pia wa kitabu cha ufugaji nguruwe cha kiswahili rahisi kwa kila mtanzania 'Kanuni za Ufugaji Nguruwe wenye tija'

Waweza wasiliana nasi kwa 0789412904/0754393838 kwa simu au whatsap. Tusipopokea andika ujumbe tutakupigia.
 
Majike 25 gharama za kuwalisha zikoje hapa mkuu?
 
Kuna kupiga mswaki nguruwe,Mkuu?
 
Leteni mrejesho wadau
Biashara hii ni ngumu sana. Mnunuzi akija bandani kuangalia nguruwe wako bei anayokutajia utachoka. Nguruwe likubwa na ni hybrid anakwambia anakupa laki 4. Natamani ningekua na kijiwe changu mwenyewe niwe nachinja na kuuza mwenyewe kuliko unafuga halafu mwisho wa siku unamsubiria mnunuzi aje na bei za kikolo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…