Hongera kwa kuchukua hatua
1. Si vema kuweka taka za wanyama hapo katikati sababu ammonia na harufu kutoka hapo itasambaa kwenye mabanda yote.Weka hizo taka pembeni ya mabanda huku ukizingatia uelekeo wa upepo.
Pia waweza hamishia corridor ndani na kuongeza U-shaped banda lingine kwa ndani na hivyo kuongeza namba ya vyumba
2.Hayo mabomba ya nn?Ips pipes ni nzuri na cheap.Pia nakushauri kuweka autodrinkers kila chumba ili nguruwe waweze kunywa maji kwa kiwango wanachotaka bila kuchafua na kumwaga
3. Kila chumba katika banda lako waweza weka nguruwe 4 wakubwa au wa 2 wenye watoto au 10 wadogo hadi miezi 3. Unataka kufuga wa umri gani?kama lengo lako ni kununua wadogo na kuwakuza then ok.Lakini kama unataka kuzalisha pia unahitaji ku design zaidi ili uwe na mabanda ya wakubwa,wenye watoto na grower-finisher.Kuna design very economical ya banda la grower-finisher isiyo na concrete ila mapumba/malanda.5mx5m yaweza kukaa nguruwe 15-20.Tembelea wafugaji kupata uzoefu
4.kuhusu piglets ni muhimu sana ukajua nn kinahitajika kwa jike na dume.Jike anatakiwa awe mwenye uwezo wa kuzaa wengi(at least 10) na kulea vizuri.Dume atoke mbegu inayokuwa haraka na nyama nzuri isiyo na mafuta mengi.Kutegemea na idadi mm naweza kukuuzia piglets though sipo dar.Nipo a 2 hrs drive kuelekea morogoro
5.Muhimu pia kupanga utawalisha nn!