Mojawapo ya Changamoto kubwa kwa wafugaji wa nguruwe imekuwa ukosefu wa mbegu bora na yenye tija hapa nchini. Mbegu nzuri zilizoletwa na wakoloni miaka ile zimepoteza ubora wake kwa sababu ya inbreeding.
Wafugaji wachache wenye nia ya kuboresha ufugaji wa nguruwe waliungana pamoja na kuunda chama cha wafugaji nguruwe Tanzania(Tanzania Association OF Pig Farmers -TAPIFA). Kwa kupitia TAPIFA watanzania wengi wataweza kupata aina mpya ya mbegu ya nguruwe iitwayo
Camborough.
Mbegu hii ina sifa zifuatazo:
- Hukua haraka-inaweza kuongezeka 0.7-0.9kg kwa siku.Camborough wa miezi 6 anazaidi ya 100kg
- Hutumia vizuri chakula kuzalisha nyama(feed conversion)
- Huzaa watoto wengi(watoto 10-23)
- Huwa na nyama nzuri isiyo na mafuta
Tayari kuna wafugaji wanafuga mbegu hizi hapa Tanzania wale ambao waliagiza mwanzo lakini pia TAPIFA yaweza kukusaidia kuagiza mbegu hii.Waweza tembelea
www.tapifa.or.tz kupata taarifa zaidi kuhusu chama hiki mkombozi wa wafugaji nguruwe Tanzania au waweza wasiliana nami pia kwa 0789412904(simu,msg,whatasap). Waweza pitia threads mbalimbali za ufugaji nilizoandika jamii forums kuhusu tasnia hii ya ufugaji(search MalafyaleP).
Angalia pia attachment inayoonyesha growth performance ya camborough.
..........................................
Baada ya kupokea simu nyingi na meseji ni vema nikaweka sawa zaidi:
Hii mbegu ni ngeni nchini hivyo wafugaji wachache tayari wamezalisha watoto na wengi hawauzi kwa sasa. Kuna njia mbili za kuipata kwa wingi
1.Ngoja wenye nazo wazalishe ununue kwao.Itakuwa March to April 2017 kwa sababu wanyama wengi wana mimba sasa.
2.Kuagiza kutoka nje kwa kupitia TAPIFA na hii ni kwa wanachama tu!
Chaguo ni lako.
Sio rahisi mm kuwepo jf muda wote.Nipigie kama una maswali zaidi na usiponipata kwa simu andika msg nitakupigia.
Upatikanaji wa hii mbegu kwa sasa ni gharama,hivyo hii mbegu ni kwa wale tu wanaotaka kufanya ufugaji kibiashara na wapo tayari kuwekeza.ahsanten
Kuna maelezo kwa undani kuhusu hii mbegu hapa
www.picrsa.co.za