Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Naomba kuelekezwa namna ya kufuga nguruwe kisasa na kibiashara

Kuna nyuzi kibao kwenye jukwaa hili hili zinaelezea kila kitu kuhusu ufugaji wa nguruwe kisasa na kibiashara. Endapo utataka kufanya ubia katika hii biashara ya ufugaji wa nguruwe karibu tuzungumze.
 
Habari wakuu.. mimi ni miongoni mwa wafugaji wachanga wa nguruwe .. tatizo langu ni kuwa nilinunua vitoto vya nguruwe sehemu moja yaani wote ni tumbo moja madume 2 na majike 6.. tatizo kuna wafugaji wachache huku kijijini wanasema hawa nguruwe dada na kaka wakipandiana vitoto vitakavyozaliwa vitakufa nitafute dume sehemu nyingine.. je kisayansi kuna ukweli wowote hapo?
 
Jaman naomben niulize swali nna imam wenye elimu nalo watanijibu kiufasaha



Jaman nasikia kuwa nguruwe anaingia ktk hedhi kama binadam eti hii Habar ina ukweli? Na kunawanaosema nguruwe wana tabia ya kuingiliana kinyume na maumbile hii nayo imekaaje
 
Hii mimi ni field yangu kabisaaa na imenigusa sana,kwa kuwa mimi hii elimu niliipata bure kwa msaada wa serikali iliyoko madarakani acha nami niwasaidie watanzania wenzangu.

Kwa kawaida nguruwe hubeba mimba kwa muda wa miezi mitatu, wiki tatu na siku tatu,hii ni sawasawa na siku 114. Hiyo ndiyo gestation period ya nguruwe. Kuhusu idadi ya watoto ambao nguruwe anaweza akazaa itategemea na idadi ya titi/nyonyo ambazo mama alizokuwanazo,zikiwa kumi na mbili basi atazaa kumi na mbili zikiwa nane pia atazaa nane nk, lakini kwa ujumla nguruwe huzaa watoto kuanzia 8-12.
Tahadhari,fuga mbali na maeneo ya waislam na wazabato.
Kwani mkuu kati ya hizi Dini mbili na nguruwe kipi kilianza kuwepo Duniani?
 
Nahitaji kufuga nguruwe ila natatizwa sana na aina ya mbegu kuna mkulima mmoja aliniambia kuna nguruwe wanaoweza kufika hadi kilo mia tatu na ni wa kisasa. Lakin huku nilipo sijawaona kabisa. Naombeni kama kuna mtu yeyote mwenye udhoefu na hili anisaidie.
 
Back
Top Bottom