Wafugaji wengi wamekuwa wakinywesha maji nguruwe wao kwa kuweka kwenye masebeni au sehemu zilizojengewa chini, unyweshaji maji nguruwe wa aina hii imekuwa ni moja ya sababu ya nguruwe kupata magonjwa kutokana na uchafu kuingia katika maji wakati mwingine nguruwe halalia na kukanyaga maji hayo au kujisaidia hupelekea kupata minyoo na hivyo inaathiri ukuaji wa nguruwe hatimae kudumaa endapo hawatatibiwa kwa wakati.
Mbali na magonjwa, vijana wengi ni wavivu kufanya kazi hivyo unaweza kukuta nguruwe amewekewa maji mara moja tu toka asubuhi. Vyombo vimeisha maji lakini hakuna anayejishughulisha kuwawekea maji nguruwe, nguruwe akikosa maji ukuaji wake huwa wa mashaka. Nguruwe anahitaji maji sana, si tu maji bali maji safi na salama.
Katika ukuaji wa teknolojia, kuna kifaa kinaitwa pig nipple drinker. Kifaa hiki ni maalumu kwaajili ya kunywea maji nguruwe wako, uwepo wa maji bandani mwako utakuwa wa uhakika kwasaa 24 na maji yanakuwa masafi muda wote.
JINSI YA KUFUNGA DRINKERS
- Unakuwa na tank lako la maji ambalo una connect bomba toka kwenye tank kuja kwenye banda la nguruwe
- Bomba ikifika kwenye la nguruwe mbele ya bomba ndipo unafunga hicho kifaa (drinker) ili nguruwe aweze kunywa maji
- Kifaa hicho kipo kama chuchu hivyo nguruwe akihitaji maji anaenda kunyonya na maji yanatoka. Na huo ndio ufugaji wa kisasa katika nchi zilizoendelea
Angalia video hapo chini nimeattach video uone nguruwe anavyokuja masafi kwa starehe, ukiwa na swali lolote kuhusu drinkers za nguruwe tupigie kwa namba 0625 504 952