Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

najihusisha na ushauri pamoja ufugaji wa samaki aina ya sato na kambare kwa ujumla tuwasiliane zaid kwa atakayehitaji ushauri npo dar. mawasiliano maisha_magumu@yahoo.co.uk,0687136037
 
Kwa Ardhi ya kigamboni nahitaji kuweka karatasi ngumu au nachimba tu bwawa na kuanza kazi?
 
wakuu naomba kujua mahala pa kupata karatasi za nailoni ngumu za kuzuia maji yasipenye

Unahitaji dam liners za kucover bwawa la ukubwa gani? Nipe vipimo HxWxL nikupe bei. Au tuwasiliane kwa simu namba 0714881500
 

Mkuu Malila na wadau wengine wa ufugaji wa samaki ... tunaomba feedback

nina mashine ya kutengeneza pellet feeds ... nakusudia kuanza kutengeneza fish pellet meal ... naomba ushauri wa market trends na feed formulars .... ILA you seem technically informed or a professional in fisheries please help
 
 

Hv kumbe ule mradi ni wa mzungu,,nlishaenda hadi kwa wale jamaa nkapiga nao stori mbili tatu na nkajua ishu ni ya kwao,,doh!
 
Ufugaji wa samaki kwenye bwawa

January 29th, 2014


"Nina shamba maeneo ya Bunju Dar es salaam. Ningependa kufuga samaki kibiashara. Maji ya uhakika ni ya kisima na yana chumvi kiasi. Napenda kupata maelezo zaidi yatakayoniwezesha kuanza ufugaji huu."-Angela,Dar es Salaam




Wakulima wanaweza kuongeza kipato kutokana na ufugaji wa samaki katika maeneo yao

Ufugaji wa samaki kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Mbali na hilo, mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla ya kuanza ufugaji. Moja ya vigezo hivyo ni soko. Si jambo la busara kuanza shughuli yoyote kabla haujafanya uchunguzi na kujua kama kuna mahitaji ya bidhaa unayokusudia kuzalisha. Wafugaji wengi wameanzisha ufugaji wa samaki lakini wakaishia kupata hasara kutokana na ukosefu wa soko. Na wengine wameanguka kutokana na utunzaji mbovu wa mabwawa ya samaki.

Maji
Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki. Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji. Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki. Wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatika yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Kwa wakazi wa Dar es
Salaam, inawezekana pia kufuga samaki kwenye bwawa, endapo maji yana chumvi ya wastani, na kwa kiwango kinachoshauriwa kitaalamu, basi samaki wanaweza kustahimili, na kukua vizuri.

Bwawa

Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.

Utengenezaji wa bwawa la samaki kwa maeneo yenye udongo wa kichanga kama Dar es Salaam, mfugaji atalazimika kuchimba na kuweka karatasi ya nailoni. Hii, itasaidia kuzuia upotevu wa maji pamoja na kuzuia bwawa kuporomoka.

Ni vyema upande mmoja wa bwawa ukawa na kina kirefu kuliko mwingine. Upande mmoja unaweza kuwa na kina cha mita moja na nusu, na mwingine mita moja. Hii itamsaidia mfugaji kuweza kulihudumia bwawa vizuri, hata kama ni kuingia na kufanya usafi.

Utunzaji wa bwawa



Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara, hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.

Ulishaji

Wafugaji walio wengi, wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishaji wa samaki. Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha samaki mara mbili hadi mara tatu kwa siku.

Aina ya chakula

Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa. Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi, bali kiwe mabonge madogo madogo, kwa wastani wa tambi.

Magonjwa

Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia, ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu (fangasi), magonjwa yatokanayo na virusi, pamoja na minyoo.

Samaki wanaposhambuliwa na fangasi, huonekana kwa macho kwa kuwa huwa na madoa madoa. Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege.

Pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwa kuwa huzubaa sehemu moja kwa muda mrefu. Magonjwa kwa samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano kwenye bwawa. Hivyo, ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.

Tiba

Tiba iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji, kasha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa, kisha kuwatoa na
kuwarudisha bwawani.

Upatikanaji

Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki Kingolwira Morogoro. Bei ya kifaranga cha Perege ni shilingi 50, na Kambale ni shilingi 150.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Bwana Kalinga kwa simu namba 0757891 761, 0787 596 798

 
Mkuu kwanini usiiweke hapahapa kila mtu akasoma?

Tangu nijiunge JF leo ndo kwa mara ya kwanza nmekuona ukipost kwenye jukwaa tofauti na lile la Kikubwa. karibu sana mkuu. mia
 
teh teh teh

Safari_ni_Safari umemaliza kila kitu katika thread hii

machapisho yangu yana kurasa zaidi ya mia moja kila moja na yanaeleza kwa kina ufugaji mfano mpk namna ya kuchimba bwawa kusafisha bwawa na vitu vingi sana sishindani na mtu na wala siyauzi natoa bure siwezi kuyaweka hapa kwa kuwa yana hati miliki na mimi nilipewa na watu wa kituo cha utafiti kwa kuwa nachimba mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Nikiyaweka hapa nitawa-dissapoint sana
 

Sasa wakisikia kuwa unayauza kwa email ndio watafurahi?
 
Sasa wakisikia kuwa unayauza kwa email ndio watafurahi?
siwezi kuyauza ninatoa bure kusaidia watu wenye interest, sina tatizo la kuuza vitu kama hivyo ninafanya hivyo kama kuwasaidia wenye nia ya kubadilisha maisha yao. Kuna baadhi ya watu nimeshawatumia bure ila kwa mwenye kuhitaji serious tu. Kwani tuna ugomvi kaka mbona kama hutaki nifanye wema mmenizoea jukwaa lile tu mnaona kila kitu ni naniliu
 
hapo juu nilielezea kuwa nachimba mabwawa sio kwamba ni kazi yangu ila nataka nifuge samaki kwa majaribio ndio fundi ananichimbia mabwawa. Sifanyi biashara ya kuchimba mabwawa na sijuhisishi na biashara yoyote humu JF nina reputation kubwa sana ndani na nje ya nchi hii sema jina langua la humu na matendo yangu ndio siyaelewi elewi. Kwa wale wote niliowatumia machapisho naomba myafanyie kazi ili tuone matokeo yake. Kwa pamoja tunaweza kujenga uchumi ya Tanzania
 
Mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri yamenifungua macho,mi nina bwawa lenye ukubwa wa mita 35 kwa 40 nililitengeneza mwaka jana nashangaa nimekuta kuna samaki nadhani watakuwa samaki pori wale wana ndevu , konokono.na vyura. niataka kufuga samaski wa mwanza nitalisafishaje bwawe lisiwe.na hao wadudu na samaski pori au samaski.ni samaki!!!! jamani tusikatishane tamaa kunawatu wameumbwa kuwa na mioyo milaini.yauwoga na hofu
 

Asante kwa hivi vitabu
 

Mkuu kazi inaendelea, majaribio ya kambale nimefaulu kwa 75% na mwaka huu nimeanza perege, mpaka september naweza kusema kitu. Vijana watu walivua kambale wakubwa baada ya kuwafuga kwa miezi nane.

Kuna mdau mmoja rafiki yangu, anaingia ubia na kampuni moja ya kichina kwa ajili ya shughuli hii, hasa vyakula, water kits na masoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…