Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.

nadhani anachokifanya Malila ndio muafaka zaidi, hata sie wengine tunajifunza kupitia hapa.
 
Last edited by a moderator:
Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.
Hapana mkuu ku Pm hapa sio sawa cos hii ni jamii tuko wengi tunaobenefi kwenye haya maelezo na uchangiaji wa hawa ndugu huku kama mimi nilikua nafikiria kuanza ila nilikua sijui maeneo ya kununua lakni hapa kidogo nimeanzakupata msaada kwahio nashauri waendelee kujibizana live ile na sisis wengine tuelewe, ku PM ni confidencial info tu please
 
Naomba nichangie mawili matatu,
Kabla hujaenda huko kwa watalaam, je eneo lako lina maji ya namna gani? Yanatiririka, yatakuwa ya kutuama, au ya kuleta kwa pampu/mfereji, je yamewahi kutokea mafuriko/au huwa yapo, ardhi ni mali ya nani/.Aina ya udongo uliopo ktk eneo lako.

Haya maswali lazima utaulizwa huko kwa watalaam. Nimeweka red kama tahadhali, nina rafiki yangu Isele Mkuranga, alipata mkondo mzuri wa maji bure, akafanya vitu vyake kitalaam,mavuno ya kwanza yakawaamsha waliolala,hawataki jamaa apanue biashara yake,kuuza hawataki, na wao kufuga hawawezi.

watu wana roooooho fulani za ajabuuuuu... Majanga
 
nipm nikupe contact za afisa uvuvi mtaalam sana ye nimstaafu kwa sasa wengi anawafanyia hizo kazi but yupo Iringa town

iv sry kupm... Wht is pm... Yaani natapa taabu kweli na hii lugha naunga unga ila haiji maana aisee...any help?? Murakokoze... Xiexie
 
Habari Wadau,

Naomba kujuzwa au anae dili na kuuza samaki yaani mbegu kwa ajili ya kufuga. naitaji sato.
au aina nyingine yoyote iliyo nzuri kufuga kwenye mabwawa hapa dar.
 
Mkuu pale moshi gereza la karanga wanauza mbegu ya samaki perege na wakubwa wake jamii ya sato (Nile perch)

okay ningekushauri fuga kambale (cat fish) ufugaji wake ni rahisi, wanazaana sans na mavuno ni ndani ya muda mfupi
 
  • Thanks
Reactions: OTL

hivi mjini kuna watu wanakula hao samaki?
 
Kuna kampuni kibaha nimesahau jina fuatilia tena na soko wanakupa wao.
 
hivi mjini kuna watu wanakula hao samaki?

Hebu acha kujishauwa wewe unaishi mji gani? Ni stockholm au London?

Maana usiniambie Dar mji ambao watu wanakula mpaka vichwa vya kuku, miguu ya kuku, utumbo wa kuku, pumbu za mbuzi, pumbu za ng'ombe, kwato za wanyama, mikia vichwa na ulimi.
 
hahahaaa! nisamehe mkuu kama umenielewa vibaya, ila I doubt kuhusu soko la huyu mdudu! kama anauzika bas itakuwa bei chee kabisa! Samaki ana miba kama razor wire, kuna siku wife alipewa huko kijijini, watoto wangu wote hawakumla kabisa, hata radha yake haivutii! Sasa kibiashara mkuu inabidi kuangalia bidhaa iliyo hot sokoni!

Hata kijijini kwetu watu wanawaona kama vyura, wanawaibua kwenye mashamba ya mpunga, kwenye madimbwi, chini ya madaraja na popote penye maji na tope!
 
Mkuu pale moshi gereza la karanga wanauza mbegu ya samaki perege na wakubwa wake jamii ya sato (Nile perch)

okay ningekushauri fuga kambale (cat fish) ufugaji wake ni rahisi, wanazaana sans na mavuno ni ndani ya muda mfupi

Asante mkuu, sasa Kambale mbegu yake nitaipata wapi kwa hapa dar?
 
Habari Wadau,

Naomba kujuzwa au anae dili na kuuza samaki yaani mbegu kwa ajili ya kufuga. naitaji sato.
au aina nyingine yoyote iliyo nzuri kufuga kwenye mabwawa hapa dar.

mkuu hapa njoo hapa sokoine kuna hatchery unit watakuuzia na pia utapata ushauri wa kitaalamu...
 
Habari Wadau,

Naomba kujuzwa au anae dili na kuuza samaki yaani mbegu kwa ajili ya kufuga. naitaji sato.
au aina nyingine yoyote iliyo nzuri kufuga kwenye mabwawa hapa dar.
faith aquaculture wapo kibamb, eden wapo chanika. Ulipata ushauri wa kitaalam wa kufuga samaki?
 
Back
Top Bottom