Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ni namna gani ninaweza kuzuia upotevu wa maji bwawani (seepage and evaporation) kwa mimi mfugaji mdogo?

Seeppage nimeelezea mkuu. Evaporation sina uhakika nayo lakini ukifanya indoor aquaculture itapunguza kiasi. Wale watu wa chemistry watatusaidia hapa. Ila kwa ufugaji lazima uwe na maji reserved kufidia loss of water kupitia evaporation na seepage
 
Kwa ufugaji wa kawaida, idadi ya samaki kwa cubic meter ni 40. Hivyo kwa tanki kama hilo utaweka samaki 400.Kwa idadi hii utahitaji kufanya water exchange 15-20% kwa kila baada ya siku tatu. Ila kwa yale marefu ambayo utahitajika kukata nusu hivyo itakuwa samaki 200. Ukitaka kufanya intensive farming katika tank hilo: samaki 120 kwa cubi meter, hivyo utaweka samaki 1200. Kwa idadi hii utahitajika kufanya water exchange kwa kila 1-2 hours na hewa ya ziada au maji yawe yanaingia na kutoka wakati wote bila-hewa ya ziada haitajika. Yale matanki ulioliza hayapo hapa lakini unaweza kutengeneza. Karibu

Ahsante kwa majibu yako

Je ukitaka uweke hao samaki 400 inamaana unanunua vifaranga 400? au unaweka wachache halafu wenyewe wanaongezeka?

Gharama ya kutengeneza hayo matanki sh ngapi kwa mfano?

Kuingiza hewa na kutoa unatumia kifaa gani? gharama zake?
 
Toa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.

Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.

Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.

Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.

Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.

Mkuu Malila tafadhali naomba namimi ndugu yangu unitumie hizo manual kwenye Email address yangu ambayo nimeku-PM
 
Huwezi kuvitundika hapa?

Karibu vitabu vyote vimetoka humu humu jamvini,nimevikusanya ili niwe na maktaba yangu ndogo,inakuwa rahisi kumtumia mtu. Pitia nyuzi za samaki za nyuma utaviona.

Ni vichache sana ambavyo nilitumiwa na wadau. Kwa hiyo ukitaka kitabu cha ufugaji Kambale kwa kule Kenya unapata,au pelege hapa Bongo nakurushia. Nikikurushia vyote waweza shindwa kusoma.
 
mkuu vifaranga wa sato wanauzwaje?
wapi wanapatikana?
na wa kambale?

Kibamba/Kwembe kuna jamaa wanauza vifaranga vya samaki,

Lakini nawaamini Kinguluira sababu ni taasisi ya serikali chini ya FAO. Pale utapata sato kwa Tsh 30/= kambale ilikuwa 150/. Unaweza kupata vifaranga wa jinsia moja. Ili ufanikiwe ni vizuri kuomba wakuandalie mapema kabla hujaenda. Hiyo bei ni ya 2012 nilipoenda mimi. Usisahau ndoo ya kubebea vifaranga wako.
 
KAMA KUKU WANAVYOWEZA kukuzwa kwa wiki 6 KUNA TECH YEYOTE au BREED type ya samaki wa mda mfupi ili uweze pata faida ktk mda mfupi?kama kuku/ wataalamu wa sayansi watujuze

Mpaka sasa, muda mfupi ninao ufahamu ni miezi sita kwa sato/pelege,ngoja tusubiri wadau wengine huenda sayansi imetupeleka huko. Kingine ni kwamba unaweza pata vifaranga wa jinsia moja ambao ni wazuri kwa biashara.

Mkuu wa kituo Kinguluira juzi aliniambia kuwa unaweza ukafundishwa jinsi ya kuandaa vifaranga wako mwenyewe. Si ajabu na hilo lako likawa tayari.
 
Wana JF nimepata eneo la Heka 4, kandokando ya ziwa, wilaya ya chato ninataka nifuge samaki aina ya Sato, ninahitaji maelekezo namna ya kuchimba bwawa, kulea samaki na chakula cha samaki. kifupi, sijui A-Z ktk mradi huu
 
alisema na yeye segerea karibu na kinyerezi.well sijapajua ila nilipeana nae miadi ya jumamosi hii inayokuja.

Kama utapenda twende basi twendelee kuwasiliana.
 
Mpigie jamaa mmoja anaitwa Emanuel Ndanya, namba yake ya simu ni 0757142048, mwambie namba yake umeipata kwa Mr Ng'oma au mzee wa hatchery, jamaa yuko nondo sana mambo ya samaki, atakufungua kwa mengi.
 
Habari wana JF,Nimejenga kabwawa ka samaki nyumbani kwangu kwa ajiri ya majaribio ya biashara ya ufugaji samaki naomba anayejua mbegu nzuri za samaki zinazotamba ktk soko pia ningependa kujua vyakula mda wa kuvuna pia DOs and Don't za hii biashara ya ufugaji samaki
 
Habari wana JF,Nimejenga kabwawa ka samaki nyumbani kwangu kwa ajiri ya majaribio ya biashara ya ufugaji samaki naomba anayejua mbegu nzuri za samaki zinazotamba ktk soko pia ningependa kujua vyakula mda wa kuvuna pia DOs and Don't za hii biashara ya ufugaji samaki

Upo mkoa gani? unataka kufuga samaki aina gani? bwawa lina ukubwa gani? Karibu upate ushauri baada ya kujibu hayo
 
nipo vikindu mkuranga nataka nifuge sato au pelege bwana ni ukubwa wa chumba cha kawaida.
 
nipo vikindu mkuranga nataka nifuge sato au pelege bwana ni ukubwa wa chumba cha kawaida.
sina uhakika kama kuna tofauti ya sato na pelege, ninachojua ni kuwa wote ni sato. (tilapia) katika kundi hili la sato au tilapia kuna mgawanyiko wa aina na aina ya samaki hawa, humo ndimo unakutana na hii jamii ya pelege. ngoja nimyumie copy Malila

kwa upande wangu nakushauri ufuge samaki kulingana na soko la hapo ulipo.
 
Last edited by a moderator:
Katika Kufikiri Kwangu Sana, Nimefikiri Biashara Hii Ninayo Ipendekeza Kwenu Wajasiliamali Na Wajasiliamali~tarajali Wenzangu. Samaki Wana Soko Kubwa Sana Hapa Nchini.

Wanahitajika Na Watu Wa Hadhi Zote. Niseme Tu Kwamba Kwa Jinsi Wanavyo Hitajika Ni Vigumu Kuondokea Wajasiliamali Watakao Kidhi Kiasi Cha Walaji. Naamini Hapa Jamvini Kuna Wataalamu Kadhaa Wanao Weza Kutupatia Maelekezo Ya Namna Ya Utunzaji Wa Samaki, Mahali, Chakula, Magonjwa Na Chanjo Na Tiba.

Hii Itawasaidia Wajasiliamali Kufukua Hazina Hii Ambayo Haija Fukuliwa Bado!
 
kidudume kakuuliza maswali mazuri nami nakuuliza maswali machache! eneo lako unalotegemea kufugia samaki lina ukubwa gani ? na je unataka kufuga kibiashara au kwa ajili ya chakula tu? karibu
 
Karibu mkuu. Eneo lako lipo wapi? Je, eneo lina udongo wa aina gani? Una maji ya kutosha (hanzo chako cha maji)?. Sato ni Perege na Perege ni Sato. Sangara wapo katika majaribio. Karibu

Mm nipo dar eneo.lina ukubwa wa mita 25 hadi 30 ni udongo aina ya kichanga ,ni kwa ajili ya biashara hao samaki,sina uzoefu wala sijawahi fuga hao samaki ,naomba uzoefu wa namna ya kujenga mabwawa,aina ya samaki wa kufuga kwani ni kwa ajili ya biashara
 
Back
Top Bottom