Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wakuu naomba kujua mahala pa kupata karatasi za nailoni ngumu za kuzuia maji yasipenye
Toa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.
Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.
Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.
Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.
Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.
kwa aliye karibu na ziwa ,unaweza kufugia samaki kando ya ziwa badala ya kuchimba bwawa la samaki.nilishawahi kuona program ktk tv. Discover Africa ,kuna kaburu yupo zimbabwe anafuga samaki ktk ziwa,na anawalisha soya na nafaka zinginezo.
musoma kuna kituo kikubwa cha utafiti wa samaki,nina rafiki yangu alikuwa stationed huko miaka ya nyuma[/Q
naomba unijuze vyakula wanavyokula samaki.kwasababu mm nataka nianze kufuga aina ya gold
Halafu nimeshangaa kule Kyela kuna ziwa Nyasa,kuna mzungu anafanya biashara ya samaki wa mapambo anapata dola za uhakika,juzi nimeangalia Etv ya Afrika Kusini wanasema Lake Nyasa ndio ziwa pekee duniani lenye samaki wa aina mbalimbali zaidi ya aina 500 tofauti,ingekuwa makabila ziwa nyasa lina makabila 500 tofauti ya samaki.na kweli hilo ziwa lina samaki wa mapambo wazuri sana wa rangi mbalimbali,lakini wananchi bado tuko kwenye usingizi wa pono na mzungu yeye anajilia kiulaini sisi tumebaki kulalamika .Nafikiri wizara inayohusika na uvuvi pia ingesaidia hawa wananchi wa wilaya ya Kyela ziwa Nyasa ni lulu ambayo imekaa tu,naamini wananchi wangewezeshwa kwa kuwa na vyombo vya kisasa vya uvuvi /kiwanda ule umasikini uliotopea unao wazunguka wananchi wa Kyela ungepungua,na isitoshe samaki wa hilo ziwa ni watamu hawana mfano
"Nina shamba maeneo ya Bunju Dar es salaam. Ningependa kufuga samaki kibiashara. Maji ya uhakika ni ya kisima na yana chumvi kiasi. Napenda kupata maelezo zaidi yatakayoniwezesha kuanza ufugaji huu."-Angela,Dar es Salaam

Mkuu kwanini usiiweke hapahapa kila mtu akasoma?Nina maandiko ya jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji na ufugaji wa samaki kwa lugha ya kiswahili na kwa mazingira ya TZ yameeleza kila kitu kuanzia kuwatunza kuwalisha chakula n.k, kwa anayehitaji an-pm e-mail yake au tuwasiliane kupitia funzadume@yahoo.com
UJUMBE: Kwa pamoja tunaweza kuiendeleza nchi yetu
machapisho yangu yana kurasa zaidi ya mia moja kila moja na yanaeleza kwa kina ufugaji mfano mpk namna ya kuchimba bwawa kusafisha bwawa na vitu vingi sana sishindani na mtu na wala siyauzi natoa bure siwezi kuyaweka hapa kwa kuwa yana hati miliki na mimi nilipewa na watu wa kituo cha utafiti kwa kuwa nachimba mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Nikiyaweka hapa nitawa-dissapoint sana
siwezi kuyauza ninatoa bure kusaidia watu wenye interest, sina tatizo la kuuza vitu kama hivyo ninafanya hivyo kama kuwasaidia wenye nia ya kubadilisha maisha yao. Kuna baadhi ya watu nimeshawatumia bure ila kwa mwenye kuhitaji serious tu. Kwani tuna ugomvi kaka mbona kama hutaki nifanye wema mmenizoea jukwaa lile tu mnaona kila kitu ni naniliuSasa wakisikia kuwa unayauza kwa email ndio watafurahi?
Wana JF
Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.
Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.
Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.
Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.
Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.
Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.
Nawasilisha kwa michango yenu.
Nteko Vano Maputo
Penye nia pana njia
--------------------------
![]()
-----------------------------
*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments