Ndugu soko lipo juuu sana sio kwa dar tu..nilipata order ya kg300 ya samki ila.akashindkana mtu wa kua nao..ss kama kg moj.dukan ni sh.7000 ad 8000..jumla utapatana na mnunuzi and utaona.how much itaingiza
namba uliyotoa sio sahihi
Sato vifaranga wapo..na ambao mono sex na wasio monosex..ukihitaji nitafute071745177
Habari.
Kupitia jukwaa hili tumekua tukijifunza vitu tofouti juu ya namna ya kujiendeleza kiuchumi ili kujikwamua kutoka katika hali tulizonazo. shukrani kwa wale walionitafuta na wakapata ushauri, nadhani bado tupo pamoja na mtafanikiwa.
Bado nasisitiza uchaguaji wa eneo na uchimbaji wa bwawa unahitajika umakini kwani ndipo ambapo utakua unafanya mladi hivo ikiwa kama initial stage ,inabidi umakini,hivo ujumuisha, uwepo wa maji safi kwa kiasi kikubwa, na uwezekeno wa kupata chakula cha samaki wako.
Mahitaji ni makubwa kulinganisha na wataalamu tuliopo, ivo tuendelee kuwasiliana kwa ajili ya kupeana ujuzi na ushauri, fuga samaki mana ni biashara inayolipa sana. kwa maelezo zaid wasiliana nami 0717451771.
Vifaranga sato madume (monosex) shilingi ngapi kila kimoja au unauzaje mkuu.
Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wanaolalamika kuwa samaki wao hawakui hasa tilapia.
Zifuatazo ni sababu zilizobainika kuwa ndio chanzo cha tatizo hilo:
1. Mfugaji kapata wapi hiyo elimu ya ufugaji
2. Idadi ya samaki wanaopandikizwa kwa mita ya mraba kwa mabwawa ya ardhini na kujengea kwa cement. Kiwango halisi ni vifaranga 5-7 kwa mita ya mraba kwa aina ya monosex na 1-3 kwa mixed sex na sio 10-20 kama inavyoelekezwa na baadhi ya watoa elimu.
3. Chakula feki kinachouzwa mitaani. Watu wanatumia tu pumba na kuwadanganya wakulima kuwa ni chakula special. Nunueni chakula kilichokuwa na label inayoonesha ingredients na percentage yake ikiwemo chapa ya tbs.
4. Ulishaji wa chakula. Wakulima wanalisha chakula kiasi kidogo. Kopo dogo la uhai sio kipimo jamani. Samaki anakula 1/3 ya uzito wakee au lisha mpaka uone hakuna samaki anahangaikia chakula ktk bwawa.
5. Uzito wa samaki mmoja ndani ya miezi 6 ni 200-400 g tena hiyo 400 uwe umefanya management ya nguvu. Hii ni kwa bwawa la ardhini na kujengea. Sio kilo moja kama mnavyoamonishwa.
Hitimisho: Kabla ya kuanza kazi za ujenzi na ufugaji tembelea wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanapatikana Temeke vetenari
kaka nimekupata vizuri kabisa. Mimi ni mmojawapo wa wanaotaka kujiingiza katika kilimo hiki, naomba pia kama una info za gharama ya ujenzi wa bwawa la ardhini nipatie tafadhali
Asante mkuu,nimepata elimu hapa kwani nina ndoto ya kufuga samaki..
Asante ndugu yangu Udongo wake ni kichangaUdongo ktk eno lako ni wa aina gani?
Asante mkuu,nimepata elimu hapa kwani nina ndoto ya kufuga samaki..
ahsante mkuu,wewe unafaa kuwa rafiki yangu,maana una ideas za maendeleo kama mm.
Nashukru kwa maarifa haya mkuu
Nimenufaika. Asante sana.
Barikiwa sana ..... tupo pamoja