Mkuu nakushukuru sana kwa kutupatia maarifa na utaalam mzuri wa kutengeneza bwawa la kufugia samaki. Ndoto yangu ya kufuga samaki nyumbani itatimia sasa! Vipi
kuhusu maji, kutakuwa na haja ya kuyabadili baada ya muda au ni hayo hayo?
mkuu samahani kwa hapa dar hiyo mifuko ya nailon inapatikana wapi kaka.Nimependa sana post yako na Mungu akubariki uwe na moyo huo huo wa kusaidia watanzania wenzakoKama ungependa kujua ni jinsi gani unaweza kutengeneza bwa la samaki yaani FishPond.
Fuata steps zifuatazo.
NB: Hakikisha hakuna wanyama waaaribifu kama kuku na mifugo mingine.
- Chimba bwawa lako kwa ukubwa utakao kulinga na eneo lako linavyo kuruhusu
- Funika na Mfuko mgumu wa plastic ili kuzuia maji yasipotee sana
- Zungusia matofali Bwawa lako
- jaza maji
- weka samaki wako
Chini hapa nimeeambatanisha na kitabu kidogo kitakachokupa mwongozo halisi zikiwemo na picha
View attachment 186400
mkuu samahani kwa hapa dar hiyo mifuko ya nailon inapatikana wapi kaka.Nimependa sana post yako na Mungu akubariki uwe na moyo huo huo wa kusaidia watanzania wenzako
Kwanza shukrani mkuu kwa kunitia moyo,
Mifuko hiyo ya plastic naweza nikasema ni ideal, ila ujanja wako hapa inabidi ukuongoze kama ifuatavyo.
1. unaweza ukanunua turubai flani hivi za plastic zinakuwaga na rangi ya blue, turubai hizi zinapatikana kariakoo sokoni kwa shilingi 20,000 - 25,000 ni kubwa kiasi japo sikumbuki vipimo.
2. Kama bwawa lako ni dogo unaweza ukatumia hata nylon lile linalopatikana baada ya kununua goadoro..
Mkuu mjini kuna vibanda vingi juu utaona wameezeka na mifuko ya plastic sasa hapohapo anzia kuwauliza wao waliyapata wapi.
karibu.
Asante ndugu yangu Udongo wake ni kichanga
Je suala la usafishaji maji ya samaki jee? Pia ni tatizo kubwa, jee hapa samaki walio kusudiwa ni wepi?
Aisee kaka naomba contact zako kwa mawasiliano vizur ningependa kupata ushaur wako kwa ufugaj wa samaki
Ni kweli ili upate mavuno bora lazima maji yawe clean hivyo ni vema kufanya exchange walau kwa wiki mara 1 kwa kutoa sentimeta 10-15 na kingiza mapya kwa kiwango hicho. Hata, hivyo matatizo niliyoyataja ndio nimeyashudia field
Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wanaolalamika kuwa samaki wao hawakui hasa tilapia.
Zifuatazo ni sababu zilizobainika kuwa ndio chanzo cha tatizo hilo:
1. Mfugaji kapata wapi hiyo elimu ya ufugaji
2. Idadi ya samaki wanaopandikizwa kwa mita ya mraba kwa mabwawa ya ardhini na kujengea kwa cement. Kiwango halisi ni vifaranga 5-7 kwa mita ya mraba kwa aina ya monosex na 1-3 kwa mixed sex na sio 10-20 kama inavyoelekezwa na baadhi ya watoa elimu.
3. Chakula feki kinachouzwa mitaani. Watu wanatumia tu pumba na kuwadanganya wakulima kuwa ni chakula special. Nunueni chakula kilichokuwa na label inayoonesha ingredients na percentage yake ikiwemo chapa ya tbs.
4. Ulishaji wa chakula. Wakulima wanalisha chakula kiasi kidogo. Kopo dogo la uhai sio kipimo jamani. Samaki anakula 1/3 ya uzito wakee au lisha mpaka uone hakuna samaki anahangaikia chakula ktk bwawa.
5. Uzito wa samaki mmoja ndani ya miezi 6 ni 200-400 g tena hiyo 400 uwe umefanya management ya nguvu. Hii ni kwa bwawa la ardhini na kujengea. Sio kilo moja kama mnavyoamonishwa.
Hitimisho: Kabla ya kuanza kazi za ujenzi na ufugaji tembelea wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanapatikana Temeke vetenari