Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Mkuu nakushukuru sana kwa kutupatia maarifa na utaalam mzuri wa kutengeneza bwawa la kufugia samaki. Ndoto yangu ya kufuga samaki nyumbani itatimia sasa! Vipi
kuhusu maji, kutakuwa na haja ya kuyabadili baada ya muda au ni hayo hayo?

Ndio mkuu, ila style ya jubadilisha sio kuyatoa yote bali ni kujazia pale ambapo yatakua yamepungua either kwa jua (evaporation) kuyachota kidogo na kujaza mapya.
 
Kiongozi mzee wangu anataka Jenga na cement...we wa mifuko ya plastic umenifungua...NPR link ya kitabu sijakiona hapo juju...thanks
 
Kama ungependa kujua ni jinsi gani unaweza kutengeneza bwa la samaki yaani FishPond.
Fuata steps zifuatazo.

  1. Chimba bwawa lako kwa ukubwa utakao kulinga na eneo lako linavyo kuruhusu
  2. Funika na Mfuko mgumu wa plastic ili kuzuia maji yasipotee sana
  3. Zungusia matofali Bwawa lako
  4. jaza maji
  5. weka samaki wako
NB: Hakikisha hakuna wanyama waaaribifu kama kuku na mifugo mingine.
Chini hapa nimeeambatanisha na kitabu kidogo kitakachokupa mwongozo halisi zikiwemo na picha
View attachment 186400
mkuu samahani kwa hapa dar hiyo mifuko ya nailon inapatikana wapi kaka.Nimependa sana post yako na Mungu akubariki uwe na moyo huo huo wa kusaidia watanzania wenzako
 
mkuu samahani kwa hapa dar hiyo mifuko ya nailon inapatikana wapi kaka.Nimependa sana post yako na Mungu akubariki uwe na moyo huo huo wa kusaidia watanzania wenzako

Kwanza shukrani mkuu kwa kunitia moyo,

Mifuko hiyo ya plastic naweza nikasema ni ideal, ila ujanja wako hapa inabidi ukuongoze kama ifuatavyo.

1. unaweza ukanunua turubai flani hivi za plastic zinakuwaga na rangi ya blue, turubai hizi zinapatikana kariakoo sokoni kwa shilingi 20,000 - 25,000 ni kubwa kiasi japo sikumbuki vipimo.

2. Kama bwawa lako ni dogo unaweza ukatumia hata nylon lile linalopatikana baada ya kununua goadoro..

Mkuu mjini kuna vibanda vingi juu utaona wameezeka na mifuko ya plastic sasa hapohapo anzia kuwauliza wao waliyapata wapi.
karibu.
 
Kwanza shukrani mkuu kwa kunitia moyo,

Mifuko hiyo ya plastic naweza nikasema ni ideal, ila ujanja wako hapa inabidi ukuongoze kama ifuatavyo.

1. unaweza ukanunua turubai flani hivi za plastic zinakuwaga na rangi ya blue, turubai hizi zinapatikana kariakoo sokoni kwa shilingi 20,000 - 25,000 ni kubwa kiasi japo sikumbuki vipimo.

2. Kama bwawa lako ni dogo unaweza ukatumia hata nylon lile linalopatikana baada ya kununua goadoro..

Mkuu mjini kuna vibanda vingi juu utaona wameezeka na mifuko ya plastic sasa hapohapo anzia kuwauliza wao waliyapata wapi.
karibu.

Hizo nailon unapata kwenye maduka ya ujenzi ni 2500 kwa mita nadhani
 
Mkuu library hongera sana kwa kuleta hii mada hapa jamvini kwani nafikiri itasaidia wengi kwa kuleta michango yenye tija kutoka kwa watu mbalimbali wenye uzoefu na shughuli hizi za ufugaji wa samaki na hivyo kutusaidia sisi ambao tunaihitaji kufahamu kuhusiana na tasnia ya ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Lakini nafikiri kama nimekuelewa vizuri ufugaji wa samaki ulioumaanisha ni ule kitaalamu wanauita Extensive fish farming ambapo ndani ya square mita moja uwezi fuga zaidi ya samaki watatu(3) kutokana na kwamba hilo bwawa la kujengwa kwa kutumia nylon halitakuwa na system ya kuingiza na kutolea maji otherwise utumie ndoo kuyachota toka bwawani kitu ambacho ni kigumu kama bwawa lako litakuwa kubwa kwani ufugaji wa kibiashara unahitaji ufanye atleast ufugaji aina ya semi-intensive fish farming ambapo bwawa litakuwa na system ya kuingiza na kutolea maji na hivyo kukuwezesha kufuga zaidi ya samaki saba(7) ndani ya square mita moja.
Labda kama kuna utaalamu mwingine ambao mimi siufahamu ambapo utaweza kutengeneza bwawa lako kwa kutumia nylon ngumu na kuweka system ya kuingiza na kutolea maji.Tunaomba ushari kwenye wenye ujuzi maaana nimeona kwenye mtandao mabwawa ya namna hii yenye nylon lakini sijajua wanatumia utaalamu gani kuweza kufuga samaki wengi kwa pamoja.
Natanguliza shukrani!.
 
tshabalala_the_greto
ahsante kwa mchango wako.
Katika kipengele cha kutandika mfuko mgumu wa plastic ni kujaribu kupunguza gharama za kutandika zege na ku okoa maji yatakayokuwa yakipotea kwenda chini.
Lakini kwa kutumia style hii unaweza kufanya extensive fish farming kwa kuchimba vibwawa vya saizi ya kati vingi katika eneo moja. Yaani unaweza kuchimba mabwawa kama haya hata kumi kama una nguvu.
Halafu hiyo dhana ya samaki 7/sqm inatokana na kina cha bwawa pia.
Mfano ukichimba mabwawa 10 ya 20sqm then utakua na 200sqm ukizidisha na idadi samaki unajikuta una samaki zaidi ya 1000.
Karibuni na wengine tujadili.
 
Mkuu Library nimekupata vizuri kuhusu nia yako ya kuwaelimisha watu juu ya ufugaji wa samaki usiotumia gharama kubwa ya mtaji kwa maana ya initial investment capital endapo mtu atahitajika kujengea bwawa lake kutokana na asili ya udogo wa eneo lake kutokuwa mfinyanzi.Lakini dhana ya kujenga vibwawa vidogo vingi haibadili ushauri wa kiutaalamu wa kufuga samaki watatu(3) ndani ya square mita moja endapo bwawa alijajengewa mfumo wa kubadilisha maji(i.e: extensive fish farming) ili samaki wako waweze kukua kwa muda unaoutarajia wa kati ya miezi 6-8 waweze kuvunwa na kupelekwa sokoni,na kama nimekuelewa vizuri hiyo ratio ya 200sqm kwa samaki zaidi ya elfu moja (1000) tayari unakuwa umelenga mfumo wa semi-intensive fish farming(i.e:zaidi ya samaki watano(5) kwa square mita).
Hapa kwa mawazo yangu nafikiri kwa mfugaji anayeanza kufuga samaki kwa mara ya kwanza na yupo katika eneo ambalo anahitajika lazima ajengee bwawa lake kutokana na asili ya udongo wake kutokuwa mfinyanzi anaweza akafunika ardhi ya bwawa lake(la ukubwa wowote) kwa hiyo material ya nylon lakini itampasa agharamikie kukunua pump ya kuvuta maji kutoka kwenye bwawa pindi maji yatakapobidi kubadilishwa na kuingiza maji mengine masafi.Hii itasaidia samaki wake waweze kupata hewa ya oxygen kwa kiwango cha kutosha,na pia waweze kula vizuri na kukua kwa wakati.
 
Unacho kisema kiko sawasawa kabisa.
Lakini hapa ni kujaribu kutafuta mbadala katika kila ugumu. Pump inachofanya ni kuokoa muda tu, ila kama huna mambo ambayo yamekubana kutwa nzima unaweza kuwa unachota ndoo za maji kumi kila siku na kujaza mengine. Kitendo hichi ktakusaidia kufanya water dilution ambacho kitakua kina slow down mchakato wa maji kuchafuka kwa kasi.
 
Hizo nylon za kuweka kwenye bwawa zipo pia special (maalum kwa kaz iyo tu) zinaitwa "pond liner" niliambiwa kenya zinapatikana lakin cjui kama hapa bongo pia zinapatikana. Technolojia hii ni kwaajili ya sehemu ambazo udondo hautuamishi maji hasa kichanga.
 
Asante Mr.Venture kwa ufafanuzi,ni kweli nimeona kwenye mtandao wakenya wanatumia hii technology ya matumizi ya hizi nylon ili kusave gharama za ujenzi wa bwawa kwa cement na tofali,pia nafikiri kuna utaalamu wa kuliweka hilo nylon kwenye bwawa ili maji yasiweze potea,lakini kinachonisikitisha yaani inamaana hakuna hata kiwanda kimoja hapa kwetu kinachotengeneza hizo nylon(i.e😛ond liner)?!
 
Malila Mungu akubariki sana kwa kuanzisha huu uzi,japo huu uzi una zaidi ya miaka mitatu(3) sasa humu JF lakini umekuwa na msaada sana kwa watu wengi waliousoma,na mimi ningependa kujua hii project ya kufuga samaki unaifanyia wapi ili tuwasiliane siku nikutembelee ili kupata shule zaidi.Shukhrani!
 
Aisee kaka naomba contact zako kwa mawasiliano vizur ningependa kupata ushaur wako kwa ufugaj wa samaki
 
Je suala la usafishaji maji ya samaki jee? Pia ni tatizo kubwa, jee hapa samaki walio kusudiwa ni wepi?
 
Asante ndugu yangu Udongo wake ni kichanga

Kwa uzoefu: Bwawa la sqm 600 utatumia matofali 1200 hadi 1600, cement mifuko 50-60, mchanga trip 6, wiremesh 4 na nondo kama 6. Mahesabu haya ni kwa bwawa ulilochimba na kujengea. Lakini ukipata fundi mzuri anaweza akakujengea la juu ukapunguza gharama ya kuchimba. Tafadhali kwa uhakika nenda na fundi site. Karibu
 
Je suala la usafishaji maji ya samaki jee? Pia ni tatizo kubwa, jee hapa samaki walio kusudiwa ni wepi?

Ni kweli ili upate mavuno bora lazima maji yawe clean hivyo ni vema kufanya exchange walau kwa wiki mara 1 kwa kutoa sentimeta 10-15 na kingiza mapya kwa kiwango hicho. Hata, hivyo matatizo niliyoyataja ndio nimeyashudia field
 
Ni kweli ili upate mavuno bora lazima maji yawe clean hivyo ni vema kufanya exchange walau kwa wiki mara 1 kwa kutoa sentimeta 10-15 na kingiza mapya kwa kiwango hicho. Hata, hivyo matatizo niliyoyataja ndio nimeyashudia field

Ahaa hapo sasa tupo pamoja, sio lazima kufanya exchange zipo mashine za kusafisha maji. Pump hii au machine hio ni nzuri kwa kutumia katika fish pond kama picha hapo chini.
 

Attachments

  • 1411500460099.jpg
    1411500460099.jpg
    20.4 KB · Views: 317
  • 1411500487354.jpg
    1411500487354.jpg
    67.8 KB · Views: 344
  • 1411500565832.jpg
    1411500565832.jpg
    52.4 KB · Views: 278
  • 1411500594534.jpg
    1411500594534.jpg
    50.8 KB · Views: 265
  • 1411500615644.jpg
    1411500615644.jpg
    53.6 KB · Views: 240
Asante ndugu, maana hapa JF wafanyabiashara wachache sana wanaeleza uhalisia. Ukikurupuka na data za hapa bila kufanya utafiti binafsi unaweza kuumia
Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wanaolalamika kuwa samaki wao hawakui hasa tilapia.

Zifuatazo ni sababu zilizobainika kuwa ndio chanzo cha tatizo hilo:

1. Mfugaji kapata wapi hiyo elimu ya ufugaji

2. Idadi ya samaki wanaopandikizwa kwa mita ya mraba kwa mabwawa ya ardhini na kujengea kwa cement. Kiwango halisi ni vifaranga 5-7 kwa mita ya mraba kwa aina ya monosex na 1-3 kwa mixed sex na sio 10-20 kama inavyoelekezwa na baadhi ya watoa elimu.

3. Chakula feki kinachouzwa mitaani. Watu wanatumia tu pumba na kuwadanganya wakulima kuwa ni chakula special. Nunueni chakula kilichokuwa na label inayoonesha ingredients na percentage yake ikiwemo chapa ya tbs.

4. Ulishaji wa chakula. Wakulima wanalisha chakula kiasi kidogo. Kopo dogo la uhai sio kipimo jamani. Samaki anakula 1/3 ya uzito wakee au lisha mpaka uone hakuna samaki anahangaikia chakula ktk bwawa.

5. Uzito wa samaki mmoja ndani ya miezi 6 ni 200-400 g tena hiyo 400 uwe umefanya management ya nguvu. Hii ni kwa bwawa la ardhini na kujengea. Sio kilo moja kama mnavyoamonishwa.

Hitimisho: Kabla ya kuanza kazi za ujenzi na ufugaji tembelea wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanapatikana Temeke vetenari
 
Back
Top Bottom