Wadau mimi nina fuga samaki aina ya sato na vifaranga nilichukua SUA..mpaka sasa wana kama miezi 6.5 lakini uzito wao sio wa kuridhisha sana kwani 1 anafika gramu 150 mpaka 190..nina mabwawa 4 yote yanasamaki.Je uzito huu na umri wao ni sawa kweli..wataalam naomba msaada
Pole sana mkuu! Ndaha,inaonyesha kwenye ufugaji wako wa samaki kutakuwa na mojawapo ya matatizo ndiyo maana samaki wako wanakuwa na kuongezeka uzito wao taratibu,inaweza kuwa ni mojawapo ya matatizo hayo hapo chini kama ifuatavyo:
1)IDADI KUBWA YA SAMAKI KWA MITA MRABA MOJA - Hii inamaanisha kwamba ukubwa wa bwawa lako ni mdogo ukilinganisha na idadi ya samaki waliopo bwawani kwa hiyo samaki wanakosa nafasi na hewa ya oxygen ya kutosha.
2)CHAKULA- Chunguza mchanganyiko wa chakula unachowapatia samaki wako je kina virutubisho vya kutosha(mfano: Protini,wanga,mafuta na madini muhimu) kwa kuzingatia ratio ya kitaalamu na chakula cha samaki kinatakiwa kiwe katika mfumo wa punje ndogondogo(pelletes) na siyo vumbi ili samaki aweze kula mchanganyiko wote kwa urahisi.
3)JINSIA YA SAMAKI- Pia kuna uwezekano samaki unaowafuga kwenye bwawa moja wakawa na jinsia tofauti(kike na kiume) hivyo kuzaliana,na kwa samaki aina ya sato(tilapia) uweza kuzaliana kwa haraka sana na kuongezeka ndani ya muda mfupi hivyo kupelekea kuwa na idadi kubwa ya samaki kwenye bwawa dogo na hivyo kupelekea samaki kukua taratibu.
4)HALI YA HEWA- Samaki haina ya sato ukua na kuongozeka taratibu sana kwenye maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi,hivyo wafugaji wa samaki kwenye maeneo ya baridi wanashauriwa kufuga samaki wao kwenye mabwawa ndani ya Greenhouse(Chumba maalumu) ili kuweza kudhibiti kiwango cha joto kisiwe kidogo wala kikubwa sana kuwawezesha samaki kukua vizuri.
5)MAJI-Maji ya kwenye bwawa la samaki yanatakiwa yawe na oxygen ya kutosha muda wote,hivyo unashauriwa kubadili maji mara kwa mara pindi unapogundua samaki wako wamepungukiwa na hewa ya oxygen(Mfano: samaki wanaonekana juu ya maji muda wote wakitafuta oxygen au uchafu na chakula vimejaa kwenye maji na kufunika bwawa lote kwa juu),pia maji ya kufugia samaki hayatakiwi yawe na kemikali za aina yoyote ili kulinda ustawi na ukuaji wa samaki wako.
6)ASILI YA UDONGO NA MAJI- PH ya udongo na maji huathiri ukuaji wa samaki kwa kiasi kikubwa,endapo udongo na maji ya kwenye bwawa vitakuwa na kiwango kikubwa cha acid (kwa mabwawa ambayo hayajajengewa),hivyo unashauriwa kupima na kujua asili ya udongo wa sehemu unapotarajia kuchimba bwawa la kufugia samaki wako.
Ni hayo tuu Mkuu kwasasa,ngoja na wataalamu wengine waje kuchangia hapa kwa msaada tofauti!