Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Wadau mimi nina fuga samaki aina ya sato na vifaranga nilichukua SUA..mpaka sasa wana kama miezi 6.5 lakini uzito wao sio wa kuridhisha sana kwani 1 anafika gramu 150 mpaka 190..nina mabwawa 4 yote yanasamaki.

Je uzito huu na umri wao ni sawa kweli, wataalam naomba msaada
 
Wadau mimi nina fuga samaki aina ya sato na vifaranga nilichukua SUA..mpaka sasa wana kama miezi 6.5 lakini uzito wao sio wa kuridhisha sana kwani 1 anafika gramu 150 mpaka 190..nina mabwawa 4 yote yanasamaki.Je uzito huu na umri wao ni sawa kweli..wataalam naomba msaada

Pole sana mkuu! Ndaha,inaonyesha kwenye ufugaji wako wa samaki kutakuwa na mojawapo ya matatizo ndiyo maana samaki wako wanakuwa na kuongezeka uzito wao taratibu,inaweza kuwa ni mojawapo ya matatizo hayo hapo chini kama ifuatavyo:

1)IDADI KUBWA YA SAMAKI KWA MITA MRABA MOJA - Hii inamaanisha kwamba ukubwa wa bwawa lako ni mdogo ukilinganisha na idadi ya samaki waliopo bwawani kwa hiyo samaki wanakosa nafasi na hewa ya oxygen ya kutosha.

2)CHAKULA- Chunguza mchanganyiko wa chakula unachowapatia samaki wako je kina virutubisho vya kutosha(mfano: Protini,wanga,mafuta na madini muhimu) kwa kuzingatia ratio ya kitaalamu na chakula cha samaki kinatakiwa kiwe katika mfumo wa punje ndogondogo(pelletes) na siyo vumbi ili samaki aweze kula mchanganyiko wote kwa urahisi.

3)JINSIA YA SAMAKI- Pia kuna uwezekano samaki unaowafuga kwenye bwawa moja wakawa na jinsia tofauti(kike na kiume) hivyo kuzaliana,na kwa samaki aina ya sato(tilapia) uweza kuzaliana kwa haraka sana na kuongezeka ndani ya muda mfupi hivyo kupelekea kuwa na idadi kubwa ya samaki kwenye bwawa dogo na hivyo kupelekea samaki kukua taratibu.

4)HALI YA HEWA- Samaki haina ya sato ukua na kuongozeka taratibu sana kwenye maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi,hivyo wafugaji wa samaki kwenye maeneo ya baridi wanashauriwa kufuga samaki wao kwenye mabwawa ndani ya Greenhouse(Chumba maalumu) ili kuweza kudhibiti kiwango cha joto kisiwe kidogo wala kikubwa sana kuwawezesha samaki kukua vizuri.

5)MAJI-Maji ya kwenye bwawa la samaki yanatakiwa yawe na oxygen ya kutosha muda wote,hivyo unashauriwa kubadili maji mara kwa mara pindi unapogundua samaki wako wamepungukiwa na hewa ya oxygen(Mfano: samaki wanaonekana juu ya maji muda wote wakitafuta oxygen au uchafu na chakula vimejaa kwenye maji na kufunika bwawa lote kwa juu),pia maji ya kufugia samaki hayatakiwi yawe na kemikali za aina yoyote ili kulinda ustawi na ukuaji wa samaki wako.

6)ASILI YA UDONGO NA MAJI- PH ya udongo na maji huathiri ukuaji wa samaki kwa kiasi kikubwa,endapo udongo na maji ya kwenye bwawa vitakuwa na kiwango kikubwa cha acid (kwa mabwawa ambayo hayajajengewa),hivyo unashauriwa kupima na kujua asili ya udongo wa sehemu unapotarajia kuchimba bwawa la kufugia samaki wako.

Ni hayo tuu Mkuu kwasasa,ngoja na wataalamu wengine waje kuchangia hapa kwa msaada tofauti!
 
Hivi haiwezekani kuchkua hiyo mbegu na kuileta huku Dar?

Moja ya Watalaam waliopo pale Kinguluira ni mzaliwa wa pande zile za Igowole, na anajua ninachosema hapa, nilipomuuliza kwa nini wasisambaze mbegu ile maeneo mengi, alinijibu kuwa mchakato wa kufanya hivyo bado haujaanza.

Nikamuuliza pia kwa nini yule samaki adimu duniani, ila yupo Morogoro hatangazwi ili afugwe zaidi, jibu ni lile lile,hakuna hela ya kufanyia utafiti. Huyu samaki wa morogoro anaitwa Mjonga, ni mtamu balaa, ila anapotea mdogo mdogo sababu ya uharibifu wa mazingira. Inaaminika yupo Morogoro tu kule Kilombero.

Hawa wa Igowole inawezekana kwa juhudi binafsi. Serikali bado wanawaza uchaguzi 2015.
 
Ndgu zangu wana jf, mimi nina shamba na bustani ambayo ina maji maji ya kutosha ,
nataka kuanzisha mradi wa ufangaji wa samaki,,

naomba mwenye ufaham zaidi kuhusiana na ufungaji wa samaki na utaratibu.....! anijuze

asanten sana
 
Mkuu Search uzi wa Malila - Pata ushauri, michango, mawazo juu ya Ufugaji wa Samaki.
Utapata mengi zaidi. Kila la Kheri.
 
samaki wakue haraka chakula kiwe cha pallets,pumba itakula kwakoii,o
 
kuna wakati nilieleza kuwa nilihudhuria semina ya ufugaji wa samaki kwa kweli nami nilivutiwa sana na waalimu ambao walikuwa wanatoa mada.Kweli kama mtu unataka kufanya biashara ya samaki lazima kweli uwe umedhamiria sana na kuipenda biashara hii (INTEREST).

kwani kama unataka kufuga samaki angalia mazingira yako kama ulivyosema.Umesema kuna maji mengi tu na ninaamini kuwa yanatuama ndio maana ulipochimba wakati wa kiangazi hayakukauka.kwa maana nyingine hapo kwenye eneo lako kuna udongo wa Mfinyanzi ambao unafaa sana kwa kilimo hiki cha samaki.Japo pia unaweza kulijengea vema tu cement na kwa utaalamu bado ukafuga.

Lakini pia unaweza kutengeneza bwawa lako katika vyanzo vya maji vya uhakika kama vijito,chemichemi au mifereji.Pia kwenye udongo unaofaa,eneo lenye mwinuko wa wastani pia lililo karibu na unakoishi kwani bwawa lako linatakiwa kuwa karibu na wewe ili uweze kulilinda na pia kuliangalia kwa namna nyingi kama kulisha chakula n.k pia liwe kwenye eneo lenye miti ili kuleta kivuli.

Hii ni kwa manufaa ya wengine.Kuna umuhimu sana wa kuhudhuria semina hizi zinazotolewa kwani Zinajenga sana na unaendelea kuwasiliana na waalimu wako siku zote.Hawa Africa Upendo Group ndio wanaoendesha semina hizi.kuna njia za kupima udongo kama unafaa.Pia kabla ya kuweka samaki unapaswa kurutubisha bwawa lako vema.yaani liwe na vyakula vya asili vya utosha.unarutubisha kwa kutumia vitu mbalimbali kama mbolea mimea n.k baada ya muda unaweza kupanda vifaranga vyako na kuwapa chakula na mbolea na kuleta ile rangi nzuri ya kijani katika maji na hewa.Samaki anakula vyakula vya kawaida sana ambavyo vinapatikana kirahisi na nikidogo tu bila gharama yoyote kubwa.Hata wadudu bado ni chakula kwao.

samaki hawatakiwi kuwekwa kwenye kina kirefu sana ni kama mita moja tu kwenda chini na inategemea unataka ukubwa gani kama 10 kwa 10 wanaweza kukaa hata samaki elfu kumi hata laki kutegemea na aina ya samaki.Nile-Tilapia ni mbegu nzuri sana kwa biashara hasa ukinzingatia leo kuwa wengi wa wafanya biashara hasa mahotelini wanahitaji gramu 250 ukiwa ndicho kipimo kizuri kwa wateja wengi katika mahotel.utalamu wa kufuga Cat fish au kambale ni tofauti sana kwani wale wanaishi ardhini na huzaana sana wakati wa mvua na mafuriko.Hwazai kabisa kama utawafuga kama hawa samaki wengine.

Mkuu asante kwa ufafanuzi...bila ya kuwa na interest na ufanyacho ni kazi bure!!
 
Wadau mimi nina fuga samaki aina ya sato na vifaranga nilichukua SUA..mpaka sasa wana kama miezi 6.5 lakini uzito wao sio wa kuridhisha sana kwani 1 anafika gramu 150 mpaka 190..nina mabwawa 4 yote yanasamaki.Je uzito huu na umri wao ni sawa kweli..wataalam naomba msaada
Bwana Ndaha, je vifaranga ulivyochukua vilikuwa na gram ngapi? Je, una rekodi ya joto la maji kwa kipindichote cha ufugaji ( au ulifuga msimu wa joto au baridi?).
 
Malila Mungu akubariki sana kwa kuanzisha huu uzi,japo huu uzi una zaidi ya miaka mitatu(3) sasa humu JF lakini umekuwa na msaada sana kwa watu wengi waliousoma,na mimi ningependa kujua hii project ya kufuga samaki unaifanyia wapi ili tuwasiliane siku nikutembelee ili kupata shule zaidi.Shukhrani!

Mkuu mimi nafugia Mkuranga kijijini Msorwa.
 
Niliamua kufanya utundu kidogo,
Mwaka huu mvua ilinyesha vizuri na hivyo kambale walizaliana sana. Sasa mimi nikapiga mbiu kwa madogo kule Mkuranga karibu na shambani kwangu kwamba nanunua kambale. Nimepata kambale wengi sana, na bado nawakusanya. Kasheshe ni chakula. Mdau mmoja alinitembea na kunihakikishia kunipa formula ili nitengeneze chakula changu mwenyewe, hasa floating pellets.

Hawa kambale pori wako vizuri.
 
Mungu akubariki nirushiekaka zqkukuwakienyeji
 
Ni samaki wa aina gani hao na hao ambao hizaliana ni kwa muda hani na kwa kiwango gani
 
Back
Top Bottom