Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Kama Mimba ya Binadamu...

Idea Zingine unaweza kugeuka Masikini kwa muda mfupi.... Gharama zote hizo siku unavuta unaishia kulipa madeni... Deal kama hizi uwe na kipato kingine cha kuendesha Maisha
Kawaida ni miezi 6 unapata gram 250 hadi 350. Hiyo 9 kama unaitafuta nusu kilo. Vile vile inatafutwa kizazi kitakachokuwa kinafugwa kwa muda mfupi. Mfano Thailand wanacho kizazi cha tilapia cha aina hiyo
 
kwa samaki 5000 utavuna kilo 1000-1700 za samaki. Chakula utatumia kilo 1000 -2000 mpaka kuvuna.Kwa maana ya 1:1.5
 
Nitakutafuta mkuu siku moja ,Kwan kuna sehem nimetoka juz kutembea kwa ajili ya kupata eneo ..ufugaji wa Samaki ni moja ya malengo yangu ya siku za mbelen
 
kwa samaki 5000 utavuna kilo 1000-1700 za samaki. Chakula utatumia kilo 1000 -2000 mpaka kuvuna.Kwa maana ya 1:1.5
Na kilo Moja ya Samaki nadhani kuanzia 6,000/= hadi 9,000/= so ukipata kila 1,000 mean ukiuza unapata million 6 hadi tisa... Si Mbaya ila msoto wastan wa pato lako kwa mwezi ni million 1 si haba something is better than nothing kama upo kitaa au unaongeza kipato mbadala
 
katika huu uzi nimejifunza mengi lakini naomba orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo samaki wanakula vyaasili
 
Kwani unatakiwa kuwalisha kiasi gani cha chakula kwa siku hao samaki elfu tano?
 
Hivi wakati wa kuwavuna ni njia gani inatumika kuwakusanya samaki kutoka kwenye bwawa la kutengeneza mwenyewe?
 

NIMEKUWA NIKITAFUTA SANA GHARAMA ZA ULISHAJI WA SAMAKI HADI KUWAVUNA. Hapa naona nimeanza kupata mwangaza. Nadhani tunatakiwa kupiga hesabu sawasawa, au mimi sijaelewa.
Kama chakula kilo 20 = Tzs 50,000/- na miezi yote 9 kitatumika jumla ya kilo 1000 inamaanisha mifuko 50 ya 20kgs @ Tzs 50,000/-. Hapo tunapata kama 2.5 m ya chakula + gharama za mfanyakazi (labda very minimum 150k per month)=1.35m + gharama nyingine (bado sizijui) itakuwa inakimbilia 5m+ (bila kuweka baadhi ya gharama). Mwisho wa siku unapata kama 7m kwa mauzo na ukitoa 5m zinabaki 2m. Ukizigawanyia kwa miezi tisa unapata kama 222,222/- .
Je hesabu ziko sawa hapa wataalamu?
 
Lazima ununue chakula?unaweza kutengeneza mwenyewe kuna mashine zipo.
 
je? hakuna group watsup linalohusiana na ufugaji wa samaki?
 
Hii Biashara Ni Pasua Kichwa Mkuu Usijaribu.... zipo Njia za Kisasa waeza jaribu sio hizi za kulisha hadi kichwa kipasuke... nadhani mleta mada na wachangiaji wengi wanatumia njia za ufugaji wa kale... kuna mhindi mtaalamu wa kiwanda pale kipawa aliniambia kufuga si mchezo kunahitaji pesa nyingi huu mdogo mdogo ni kuwaste time tu...

Unatakiwa kufuga samaki wa maji ya chumvi kuna maeneo yaliyo mazuri karibu na bahari unajengea na kuset maji yanatoka baharini yanakuja bwawani and then yanatoka na kurejea baharini smaki wanakuwa wenyewe tu chakula unaweka kidogo sana ila project na technology yake inaweza kukucost kama usd 20,000 ambazo ni sawa na 43M ila unavuna continuous so waeza kuwa millionaire kwa miaka hii kufanya biashara kwa ajili ya pesa ya kula Watanzania tuache... sasa hivi tufikiria biashara za kitajiri yaani hadi unayemuajiri uwe unamlipa kama manager wa bank kuu...

Tumuombe Magufuli naye atembelee Israel wana technolgy kali sana niliona wanafuga fish kwenye matank wanawalisha eels na wadudu wengine wanawazalisha na chaula kidogo waeza fuga hata juu gholofani au kwenye jangwa na ukawa tajiri sio mtafuta mboga ya kula...
 
Vipi wewe unafanya biashara gani ya kitajiri?
 
Nahitaji ramani ya uchimbaji wa bwawa la samaki kwa usahihi zaidi,isiwe fade kama hii hapo kwenye forum
 
Huu ushauri hautoki kwa Great thinker daima huwa hatujifunzi kwa walio shindwa Kama wewe, tena nikwambie tuu ukifuga kwa asili wanakuwa wakubwaa hakika na hakuna gharama. Twendeni Busokelo tukafuge maji ni tele mwandosya katunuku
 
Mkuu bukoba naomba mchanganyo wa chakula cha samaki. Na vipi hiyo mashine na bei gani madukani
 
Huu ushauri hautoki kwa Great thinker daima huwa hatujifunzi kwa walio shindwa Kama wewe, tena nikwambie tuu ukifuga kwa asili wanakuwa wakubwaa hakika na hakuna gharama. Twendeni Busokelo tukafuge maji ni tele mwandosya katunuku
Wewe Great thinker unadanganya watu.... watakao fuata ushauri wako na kutimiza watafail... na kukulaani.... nani katumia njia zisizo na new tech kafanikiwa? hebu orodhesha zaidi ya kuganga njaa.... Serikali inajua yote ndio maana imeamua kuwe na viwanda tuwe matajiri na sio waganga njaa miaka yote.... kijana angalia umri unaenda unawaza kinume nyume... You don't need a lot of land,Water,Fish food you need Knowledge
 
Microorganisms ( mimea na wadudu),ambavyo vinatokana na fertilization ya maji ya bwawa ulifanya.

***Planktons(phytoplanktons-mimea midogo sana, zooplanktons-wadudu wadogowadogo), Hivyo Mkuu (microorganisms) sioni kama litakuwa neno sahihi hapo juu kwa maana halisi ya Micro-organisms.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…