Mkuu hongera sana. hapa kwenye chakula ulaji wa samki pananichanganya kidogo. kwa siku kwa hao samaki 5000 wanakula kiasi gani? hicho chakula cha 50,000 (20kg) wanakitumia kwa mda gani?
Nafikiri kuna gharama kubwa san kwenye chakula kwani mtaalamu hapa kasema wakiwa wadogo wanakula 5% ya uzito wao. maana yake kwa hao 5000 tuseme wana uzito wa 20kg watakula 5000g kwa siku sawa na 5kg. kwa mwezi watakula 150kg kwa mwezi ambayo itakuwa 450,000tsh kwa bei ya 3,000tsh kwa kilo. sasa kwa miezi mitatu ya mwanzo itakuwa zaidi ya 1.4M kumbuka uzito unazidi kuongezeka. sasa kwa miezi ya 4-7 ambapo watakuwa wanakula 5% ya uzito sema wamefika 400g+ maana yake mmoja atakula 20g kwa siku. 5000 watakula 100kg kwa siku.. sasa kwa miezi 3 itakuwa ni 9,000kg ambazo ni 27,000,000tsh ( kwa bei ya 3,000tsh kwa kg)..
sasa faida itakuwa wapi mkuu?
Naomba kuelimishwa hapa wakuu