Lugoba Investment
Senior Member
- Dec 5, 2013
- 180
- 188
Mbona wakubwa tu wako fresh,pamoja na pumba anawatengenenzea pia wadudu wadogo wadogo (zooplanktons)Kwa hiyo diet lazima wadumae.
Nina maswali juu ya ufugaji wa samakiNimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani,nitawafuata mbegani,wapo kule.
Jamani ambaye anafuga atupe uzoefu nasi tujaribu
Karibu sana kiongozi.
Ndio ni mzoefu.
Mimi siuzi vifaranga wala sitegemei kufaidi chochote kwa huu uzi,hapa tunapeana maarifa tu.Tahadhari wote. wengi wanaojitangaza hata kwenye redio na TV, hawana kabisa uelewa wa ufugaji samaki na mara nyingi wanadanganya hata faida inayotegemewa ili wauze vifaranga. Nawashauri sana musijiingize kwenye ufugaji huu kabla ya kuiona idara ya Ufugaji samaki ktk wizara ya Kilimo.
Naandika kwa uhakika. Ufugaji nimeuona ktk nchi za Misri na Cameroon kwa afrika. Nigeria inajitahidi pia. South east asia, indonesia wako juu sana. Tatizo kubwa kabisa ni ubora wa maji. Sehemu kubwa ya TZ ina maji ya hovyo kwa ufugaji huu. Mbinu za kuyafanya yawe bora ni finyu na hatuna mitaji ya kufanya hivyo. Uholanzi wanafuga sato ktk matanki kama hayo ya 'simtank' lakini techolojia ya kusafisha maji iko juu. Naweza sema mengi juu ya hili. Jihadhalini!
Mimi siuzi vifaranga wala sitegemei kufaidi chochote kwa huu uzi,hapa tunapeana maarifa tu.
Na ndio moja ya miradi yangu nayoifanya so naandika vitu halisi.
Tilapia (sato/perege) wa maji baridi anafugika katika umunyu (chumvi) kuanzia 0-5. Maji ya kisima hayawezi kuzidi hapo hivyo unaweza kufuga. Vile vile tafiti nyingi zinaonesha huyo tilapia wa maji baridi anakuwa zaidi katika umunyu mpaka 15. Kwa ziada kuna tilapia wa maji chumvi. Kuhusu acidity yanatakiwa yawe 7-8.5 hii ndio bomba kabisa. Ukishafanya vipimo vya maabara weka hapa tukusaidie kutafsiri.
Umeandika kwa miezi 6 sato au tilapia atakuwa na gram 500. Kawaida kwa ufugaji wenye faida, tilapia anatakiwa awe na gram 800! Hii ni kama mazingira yanafaa kiutaalamu.
Hao catfish uliowataja lazima uwauzie vifaranga tu maana uzaaji wake ni lazima urutubishe mayai kwa mkono (artificial). ubaya zaidi ukuaji wake kwa maji ya bwawa ni mbaya kabisa, labda uwe unatengeza chambo kwa kuvulia samaki wengine.
Wale wote wanaotusikiliza narudia tena, tatizo kubwa ni ubora wa maji. ongeza tatizo la vyakula ingawa hili unaweza kuelekezwa kwa nusu saa ukaweza.
Nimesema at least awe 500grams au zaidi.
Pale mwishoni kwenye original thread nimeandika kama wengine wana utaalamu zaidi wachangie,sasa wewe umekuja kukosoa au kuchangia?
Halafu mbona unanilazimisha niuze vifaranga? Nimekwambia mimi siuzi vifaranga aina yeyote unasema lazima niwauzie catfish fry,una shida gani? Au wewe ndo unataka kuwauzia? Sema tu naruhusu watu kuanzishia biashara kwenye huu uzi.
Umeandika kwa miezi 6 sato au tilapia atakuwa na gram 500. Kawaida kwa ufugaji wenye faida, tilapia anatakiwa awe na gram 800! Hii ni kama mazingira yanafaa kiutaalamu.
Hao catfish uliowataja lazima uwauzie vifaranga tu maana uzaaji wake ni lazima urutubishe mayai kwa mkono (artificial). ubaya zaidi ukuaji wake kwa maji ya bwawa ni mbaya kabisa, labda uwe unatengeza chambo kwa kuvulia samaki wengine.
Wale wote wanaotusikiliza narudia tena, tatizo kubwa ni ubora wa maji. ongeza tatizo la vyakula ingawa hili unaweza kuelekezwa kwa nusu saa ukaweza.
Dawa ya ukuaji wa samaki ni mlo kamili na hizo mbegu.Kuna mbegu hata ukimpelekea myahudi hawezi kuwakuza.Ahsante kwa mchango wako. Hata hivyo, ningekuelewa kama ungetuwekea huo mkokoteo wake wa faida kati ya samaki wa gram 800 na 500.
Kwanza katika bwawa il upate samaki wa gram 800 unatakiwa umfuge kwa zaidi ya miezi 12. Kwa mfano nchi zilizoendelea Israel wanapata gram 500 kwa kutumia teknolojia ya kisasa tena kwa muda wa miezi 9 hadi mwaka.Hapa nchini kwa teknolojia tunayotumia inawezekana? Labda uweke samaki wachache kwa mita ya mraba ili uhamasishe ukuaji zaidi kwa hao samaki wachache. Je, ukipiga mahesabu ya mapato na matumizi watakuwa na faida sana? Watafikia hasa hasa gram 500 ndani ya miezi 7-8. Ukichora graph ya kumtunza samaki wa gram 800 itakuwa kubwa kuliko hata wa gram 500 na mauzo utakuta yapo juu kwa samaki wa gram 500 kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kufuga mara mbili kwa mwaka, pia gharama ya kumtunza itakuwa chini kuliko huyo wa 800, watakuwa wengi katika bwawa kuliko huyo wa 800
Pili, soko lako linahitaji hao samaki wa gram 800? Hivi chukulia wewe nyumbani upate samaki 4 katika kilo na samaki 1 katika kilo utanunua samaki gani? nafikiri utataka kila mtu apate wake. Hata katika mahoteli wanapenda samaki anaekaa katika plate. Sasa samaki wa gram 800 kweli atafiti?
Mwisho, unatakiwa ujue hayo yote unapopanga kufanya ufugaji wa samaki
Ahsante kwa mchango wako. Hata hivyo, ningekuelewa kama ungetuwekea huo mkokoteo wake wa faida kati ya samaki wa gram 800 na 500.
Kwanza katika bwawa il upate samaki wa gram 800 unatakiwa umfuge kwa zaidi ya miezi 12. Kwa mfano nchi zilizoendelea Israel wanapata gram 500 kwa kutumia teknolojia ya kisasa tena kwa muda wa miezi 9 hadi mwaka.Hapa nchini kwa teknolojia tunayotumia inawezekana? Labda uweke samaki wachache kwa mita ya mraba ili uhamasishe ukuaji zaidi kwa hao samaki wachache. Je, ukipiga mahesabu ya mapato na matumizi watakuwa na faida sana? Watafikia hasa hasa gram 500 ndani ya miezi 7-8. Ukichora graph ya kumtunza samaki wa gram 800 itakuwa kubwa kuliko hata wa gram 500 na mauzo utakuta yapo juu kwa samaki wa gram 500 kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kufuga mara mbili kwa mwaka, pia gharama ya kumtunza itakuwa chini kuliko huyo wa 800, watakuwa wengi katika bwawa kuliko huyo wa 800
Pili, soko lako linahitaji hao samaki wa gram 800? Hivi chukulia wewe nyumbani upate samaki 4 katika kilo na samaki 1 katika kilo utanunua samaki gani? nafikiri utataka kila mtu apate wake. Hata katika mahoteli wanapenda samaki anaekaa katika plate. Sasa samaki wa gram 800 kweli atafiti?
Mwisho, unatakiwa ujue hayo yote unapopanga kufanya ufugaji wa samaki
Mkuu vizuri kwa maelezo yako mimi nimekuwa nikisoma na kuupenda uzi ulioanzishwa na bukoba boy kwa sababu zangu binafsi, pamoja ninaunga mkono maelezo yako lakini ninataka nikueleze jambo moja, ni muhimu pia kujifunza kwa mtu anayetekeleza jambo sio kutegemea theories peke yake ingawa utaalamu na wataalamu ni muhimu, Wakina bukoba boy wameeleza mambo mengi muhimu ambayo mengine hao wataalamu hawatoi ushauri unaoendena na mazingira yetu.Nadhani hutaki kunisikiliza. Nilikuwa nawapa tahadhari ya juwaepuka wanaojitangaza redioni na TV. Mmoja wapo yuko hapa mkoa wa pwani njiani ukielekea morogoro, ambaye anapofuatwa ni kuwapa matumaini wafugaji ili yeye auze vifaranga.
Bahati mbaya wewe ukadhani nakuzungumzia wewe na kuanza kujibu kwamba huuzi vifaranga. Wapi niliposema unauza vifaranga?
Mimi niliwaelekeza wizarani kwenye wataalamu wa kazi hiyo ambao hawawezi kukupa hadithi za uongo. Sijasema nioneni mimi. btw. lazima ufahamu kwamba kituo kikubwa cha kuzalisha vifaranga che serikali kiko morogoro.
Kilijengwa na FAO. hao wengine wasanii. Hawawezi hata kufanya sex reversal! Nazungumza kitu ninachokifahamu.
Nawe mkubwa sasa unanishangaza! Kweli kuna anayejua ufugaji wa samaki kwa theory? nani huyo? Haya ndo mambo ya mafundi gereji kudhani ni mafundi kuliko mainjinia, kwa sababu tu anaweza kuinama uvunguni na injinia hawezi.Mkuu vizuri kwa maelezo yako mimi nimekuwa nikisoma na kuupenda uzi ulioanzishwa na bukoba boy kwa sababu zangu binafsi, pamoja ninaunga mkono maelezo yako lakini ninataka nikueleze jambo moja, ni muhimu pia kujifunza kwa mtu anayetekeleza jambo sio kutegemea theories peke yake ingawa utaalamu na wataalamu ni muhimu, Wakina bukoba boy wameeleza mambo mengi muhimu ambayo mengine hao wataalamu hawatoi ushauri unaoendena na mazingira yetu. Mimi binafsi kuna mambo fulani sikupata ufafanuzi unaofaa hata kipindi nilipoamua kutembelea Maonesho ya kilimo(Nane nane) Lindi ambapo idara unazosema zilikwepo na niliziuliza hasa issue za samaki bongo, theories ni nyingi kuliko practical. Kwa hiyo watu waliopo field kama wakina Bukoba boy wana umuhimu sana. Mimi hakuna kitu nilichokosa majibu Tanzania kama jinsi tunavyoshindwa kutumia elimu na utaalamu tuliosomea kwenye vitendo, hapo kama ujui ndio ugonjwa wetu Tz unaoturudisha nyuma.
NB: UNAWEZA KUJIFUNZA MAMBO MENGI JF KULIKO UNAVYOZANI
Mimi sio msomi kama wewe. Isipokuwa JF Ni sehem ya kupeana maarifa. Hivyo hiyo paper ichambue hapa kwa faida ya wote. Kama unakubali soko ndilo linalopelekea ukubwa WA samaki basi usiseme bila kupata 800g hakuna faida. Vile vile usibase kwenye paper 1 kutoa conclusion. Isitoshe Rwanda ni wachanga Sana ktk fieldSuala la faida linategemea aina ya soko. Kama soko lako ni Tandika sokoni, kauze dagaa. Kama soko lako ni kisutu uza Tilapia wa kueleweka. Mimi naweza kulenga soko la mahoteli, niwauzie fillets! Usijichanganye maana ndo maana biashara inatushinda.
Kama we ni msomi kama mimi, tafuta paper ya Nathaniel Hishamunda, tumia google na utapata maelezo toka Rwanda. Achana na mambo ya Israel mbali huko. Kumbuka ukishindwa kuwapa uzito huo mradi umekushinda. Samaki ni viumbe walio na high food conversion ratio (kama unaifahamu).
Ni kweli lakini nitajie wapi wanafikisha hiyo gram 800? ipi ina faida kati wa 500g vs 800g?Dawa ya ukuaji wa samaki ni mlo kamili na hizo mbegu.Kuna mbegu hata ukimpelekea myahudi hawezi kuwakuza.
Fisheries mwanza..ofcourse huyo wa 0.8kg ndo profitableNi kweli lakini nitajie wapi wanafikisha hiyo gram 800? ipi ina faida kati wa 500g vs 800g?
Fisheries? wanafuga samaki?wanafanya tafiti? Ili sisi wadau tufaidike tupe hiyo elimu. 1.Vifaranga wametoa wapi 2. wametumia stocking density ipi 3.wanafuga ktk mfumo upi 4.Wamefuga kwa muda gani?5. Wanatumia chakula gani 6. Kuna mkulima ameweza kukopi hiyo teknolojia?Fisheries mwanza..ofcourse huyo wa 0.8kg ndo profitable
Fisheries? wanafuga samaki?wanafanya tafiti? Ili sisi wadau tufaidike tupe hiyo elimu. 1.Vifaranga wametoa wapi 2. wametumia stocking density ipi 3.wanafuga ktk mfumo upi 4.Wamefuga kwa muda gani?5. Wanatumia chakula gani 6. Kuna mkulima ameweza kukopi hiyo teknolojia?