Ahsante kwa mchango wako. Hata hivyo, ningekuelewa kama ungetuwekea huo mkokoteo wake wa faida kati ya samaki wa gram 800 na 500.
Kwanza katika bwawa il upate samaki wa gram 800 unatakiwa umfuge kwa zaidi ya miezi 12. Kwa mfano nchi zilizoendelea Israel wanapata gram 500 kwa kutumia teknolojia ya kisasa tena kwa muda wa miezi 9 hadi mwaka.Hapa nchini kwa teknolojia tunayotumia inawezekana? Labda uweke samaki wachache kwa mita ya mraba ili uhamasishe ukuaji zaidi kwa hao samaki wachache. Je, ukipiga mahesabu ya mapato na matumizi watakuwa na faida sana? Watafikia hasa hasa gram 500 ndani ya miezi 7-8. Ukichora graph ya kumtunza samaki wa gram 800 itakuwa kubwa kuliko hata wa gram 500 na mauzo utakuta yapo juu kwa samaki wa gram 500 kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kufuga mara mbili kwa mwaka, pia gharama ya kumtunza itakuwa chini kuliko huyo wa 800, watakuwa wengi katika bwawa kuliko huyo wa 800
Pili, soko lako linahitaji hao samaki wa gram 800? Hivi chukulia wewe nyumbani upate samaki 4 katika kilo na samaki 1 katika kilo utanunua samaki gani? nafikiri utataka kila mtu apate wake. Hata katika mahoteli wanapenda samaki anaekaa katika plate. Sasa samaki wa gram 800 kweli atafiti?
Mwisho, unatakiwa ujue hayo yote unapopanga kufanya ufugaji wa samaki