mangapwani zenj
Member
- Oct 24, 2019
- 7
- 3
Habar wana jamii vipi nitaweza kufuga sato na wapi nitavipata vifaranga vyake
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku za karibuni nimekuwa nikipitia makala mbalimbali juu ufugaji samaki kibiashara, nitaweka link baadae naamini itakuwa ni msaada mkubwa kwako na wengine.Habar wana jamii vipi nitaweza kufuga sato na wapi nitavipata vifaranga vyake
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu na Mimi nina shida na huyo mhusikaNisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.
Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.
Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.
Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.
salaam,Mkuu na Mimi nina shida na huyo mhusika
Hongera mkuu.ukiitaj vifaranga vipo
Habari yako Mkuu unaweza kunipa msaada wa mawasiliano wa huyo muhusika kutoka Kinguruila gerezani anayeuza kambale kwa tsh 30 maana nimetokea kuvutiwa na bei yake nzuri asante sana.salaam,
Mkuu unamtaka huyu wa samaki Kinguluira?
kifaranga cha kambale kwa tsh 30?Habari yako Mkuu unaweza kunipa msaada wa mawasiliano wa huyo muhusika kutoka Kinguruila gerezani anayeuza kambale kwa tsh 30 maana nimetokea kuvutiwa na bei yake nzuri asante sana.
Unaweza kuna wazalishaji wa vifaranga wakubwa inategemea na ulipo mfano kama uko Dar kuna Bigfish kigamboni wayakupa vifaranga na elimuHabar wana jamii vipi nitaweza kufuga sato na wapi nitavipata vifaranga vyake
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vizuri kumuona mtaalam wa samaki akakusaidia njia nzuri ya kupata mbegu iliyo bora. Sometimes kuna uhuni unaweza kufanyiwa kwa kupewa mbegu ambayo tayari imedumaa hivyo kushindwa kufikia malengo uliyoyatarajia.Habari yako Mkuu unaweza kunipa msaada wa mawasiliano wa huyo muhusika kutoka Kinguruila gerezani anayeuza kambale kwa tsh 30 maana nimetokea kuvutiwa na bei yake nzuri asante sana.
Kwenye bwawa ambalo lilikuwa na kambale nafanyaje kuwaondoa kambale wanaojificha kwenye tope kabla sijaingiza vifaranga wa sato?Mkuu Gidbang heshima kwako kwanza kwa kuwa na bwawa lenye ukubwa huo kwani huo ni mtaji tosha sana kwenye biashara ya ufugaji wa samaki.
Kulisafisha hlo bwawa ni kazi rahisi mno kwani unachotakiwa kufanya kwanza ni kutoa hao samaki wote na vyura waliomo either kwa kutumia net au kwa kutoa maji yote then uwatoe. Njia ya pili ni nzuri kwani hautopata tabu ya kuanza kuwavua kwanza then ndo utoe maji yote.
Baada ya kutoa maji na hao viumbe waliopo, inatakiwa uliache kwa muda wa kama siku moja au mbili then safisha kuta za bwawa kwa kuondoa kama kuna majani yameota ndani kwenye kuta za bwawa. Baada ya hapo toa udongo (tope kwenye sakafu ya bwawa ) kiasi cha sentimeta ishirini.
Baada ya kufanya hayo yote mwaga lime ( chokaa ) kwenye sakafu ya bwawa ili kuua vijidudu vidogo vidogo vinavyoweza kuwepo kwenye bwawa na liache likauke bila kuweka maji kwa muda wa wiki mbili hadi tatu ili kuhakikisha kuwa hakuna aina yoyote ya kiumbe au mmea uliobakia kwenye bwawa.
Baada ya hapo then unaweza kuendelea na taratibu zinazofuata kwenye ufugaji wa samaki katika bwawa lako.
Ahsante !!!!!!!!!!!!!!
umefikia wapi na ufugaji wako mzee? bado unafuga?Nisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.
Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.
Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.
Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.
umefikia wapi mzee?Mimi ndio naanza kufuga sato kwa bwawa la asili. Nishalipia bwawa najiandaa kununua vifaranga kama 11,000. God is able!View attachment 1438645
Sent using Jamii Forums mobile app
Nishaweka oda ya vifaranga. Sasa nasaka chakula cha fingerlings. Ni adimu sana kwa sababu ya Coronaumefikia wapi mzee?