Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

mwambie mtaalam afanye utafiti upya, nipo nafanya utafiti na sangara anaishi vizuri kwenye bwawa.
 
Wakufunzi naomba mnijuze ukubwa wa bwawa la vifaranga 50000 sato/ perege,naweza kupataje calculations yake ili wawe wanaweza kula vzr na ukuaji wenye tija!
 
Kwa anayejua ufugaji wa samaki maji chumvi kma prawns [emoji1654] ashushe nondo tafazali
 
Wakufunzi naomba mnijuze ukubwa wa bwawa la vifaranga 50000 sato/ perege,naweza kupataje calculations yake ili wawe wanaweza kula vzr na ukuaji wenye tija!
1m=6 samaki
M? = 50000 samaki
50000/6= 8000mita za mraba
Ukubwa wa bwawa inatakiwa iwe 8000 mita za mraba.

Bwawa linaweza likawa na urefu mita 29 na upana 29 au tofauti lkn ukizidisha ur x up upate 8000.
 
Reactions: PYD
1m=6 samaki
M? = 50000 samaki
50000/6= 8000mita za mraba
Ukubwa wa bwawa inatakiwa iwe 8000 mita za mraba.

Bwawa linaweza likawa na urefu mita 29 na upana 29 au tofauti lkn ukizidisha ur x up upate 8000.

Hivi inachukua muda gani kuwavuna hawa mkuu....?
 
Kwa hao hao utakaowaweka au wanazaliana na kuongezeka mkuu...? Na bei ya vifaranga Huwa wanauzwa mmoja mmoja...?
Kifaranga mpaka atakapofikia kutaga mayai au kuliwa ndo huchukua muda huo.
Huwa wanauza kifaranga 50 pelege na 200 kambale kwa huku niliko Njombe, naamini bei sijajua kwa maeneo mengine ila nahisi hazipishani sana.
 
Na hao vifaranga 50 ni bei gani kiongozi...?
 
Jamani hivi samaki anafugika sehem yeyote au Kuna maeneo maalum ya kuwafugia?
 
Jamani hivi samaki anafugika sehem yeyote au Kuna maeneo maalum ya kuwafugia?
Samaki anafugwa kwenye bwawa la udongo (earthen pond), lililo sakafikwa (concert pond) au bwawa ulilotanguliza lyron.

Mara nyingi aina ya bwawa unatengeneza kulingana na upatikanaji wa maji lakini pia inategemeana na mtaji.
Pia unaweza kufuga kwenye tenki na kwenye maji yanayotembea japo hii sio kwetu haipo.

Naami kuna wataalum zaidi wanaweza kujazia.

Samaki anafugwa mikoa yote Tanzania isipokua ni kama kuku anakua zaidi maeneo ya joto.
Kifaranga wa siku moja ukimuweka Njombe-Makete na Morogoro.

Utaanza kumla wa Moro wakati huo wa Njombe bado kifaranga.!
 
Hivi kwa mtaji wa milioni 5 au 10 naweza kuanza na vifaranga vingapi kuanzia mwanzo mpaka navuna kiongozi...?
 
Hivi kwa mtaji wa milioni 5 au 10 naweza kuanza na vifaranga vingapi kuanzia mwanzo mpaka navuna kiongozi...?
Inategemeana na sehemu unayotaka kuwekeza gharama za ujenzi upoje, lkn pia unataka uwekezaji wa aina gani, tumesema kuna bwawa lipo jiran na mto hivyo utalichimba tu na kuweka maji, kuna mwingine anatumia maji ya bomba au mtu hivyo ili yadipotee kwa wingi atatanguliza lailoni chini màji yasipotee, mwingine atataka bwawa lake liwe la kudumu hivyo atasakafia au atajenga la juu.

Ukimaliza ujenzi sijajua unataka bwawa lipi kati ya hayo, baada ya hapo kwenye hiyo m10 utanunua chakula na vifaranga.

Kwa uhakika zaidi fanya consultant na mtaalamu aje aone saiti na mjadiliaje mambo machache ndo utajua utaweza kupanda vifaranga wangapi lkn kwa hapa siwezi kukudanganya nikupe idadi akati sijajua gharama za ujenzi n. K
 
Unawalisha chakula cha dukani tupu?gharama za chakula zikoje?
 
Kifaranga mpaka atakapofikia kutaga mayai au kuliwa ndo huchukua muda huo.
Huwa wanauza kifaranga 50 pelege na 200 kambale kwa huku niliko Njombe, naamini bei sijajua kwa maeneo mengine ila nahisi hazipishani sana.
Gharama za Njombe.kuchimba bwawa kwa mikono hua zikoje mkuu.mfano la ukubwa 10x20m?
 
Mie naomba msaada kupata leseni ya biashara ya ya dagaa wa kigoma kuleta dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…