Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Niliwahi kumsikia Mtaalam mmoja akisema kuwa, "samaki wanaofugwa katika maji yasiyotembea hawawezi kuzaliana kwa kuwa samaki hutaga mayai anapoogelea dhidi ya mkondo".

Naomba ufafanuzi wa Kitaalamu kuhusu uzalishaji wa samaki ktk mapipa. Je, wanazaliana ama la?
 
Ndiyo maana ukiwa na hela unaweka fountain inatengeneza mkondo
 
Samaki anayetaga kulingana na kupanda na kushuka kwa kina cha maji ni catfish(kambale), lakini Sato(Tilapia), hao kwa kuzaliana ni popote kambi.
 
Reactions: al1
Kitaalamu, samaki wa kufugwa haitaji kuzaliana. Kumbuka unafuga samaki katika eneo ambalo ukubwa wake uko defined, na tayari unakuwa na budget ya ulishaji ambayo iko pre determined na idadi ya samaki waliopo in terms ya chakula, oxygen etc.


Kitendo cha kuacha samaki wazaliane, kitakufanya mfugaji kutojua idadi halisi ya samaki katika bwawa. Wanaweza wakawa wengi kuliko chakula unachowapa, na kusababisha wadumae, au kufa kwa kukosa oxygen ya kutosha.

Kwa iyo kinachofanyika ni kutumia homones maalumu kubadili jinsia ya samaji na kuwafanya wote wawe jinsia moja (Mono sex). Hii inazuia kuzaliana na kufanya management ya bwawa kuwa rahisi na matokeo kuwa poa.

So, hii ya samaki kutozaliana hakutokani na maji yaliotuama, ni vifaranga vyao kuwa mono sex
 
Samahani mkuu, hivi kwa haraka haraka tu nikitaka kuanza na samaki elf naweza kuhitaji budget ya kiasi gani kwa makadirio mpaka nitakapoweza kuwavuna kiongozi...?
 
👍Aquaculturist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…