Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki


Dah mkuu nikushukuru sana kwa ushiriki wako na hizi nondo zako. Nafikiri nikianza na mabwawa kama matatu hivi ya SATO yaliyochimbwa chini nitapata pa kuanzia.

Ngoja nifuatilie mazingira ya hapa BONGO na namna ya kuwakuza maana sijajua bado growth rate yao inakuaje mkuu.
 
Nani mwenye uelewa kuhusu Samaki wa Maji Chunvi? make nasikia unaweza kuwafuga sehemu yoyote na kinacho takiwa ni kuchota maji Baharini na kuwawekea
 
hivi haya mabwawa mnayatengenezaje?

Yapo mabwawa/ponds za kienyeji na kisasa. Ili ufuge samaki vizuri lazima ujue shape ya bwawa, bwawa lazima liwe na slop ktk sakafu yake, yaani upande mmoja uwe na kina kirefu 1.2M na upande mwingine uwe na kina kifupi kama 0.8M ili samaki aweze kucheza sawa na joto la maji linavyobadilika.

Ukubwa mzuri ni kuzingatia idadi ya samaki unayotaka kufuga, 1square metre kwa samaki 4. Ni vizuri kama maji yatakuwa yanaingia na kutoka, lakini hata static water samaki wanaishi na kukua vizuri,ila kuongeza maji kila mara ni vizuri sana kwa afya ya bwawa, pia kuna kama maturubai ya plastic pia watu wanatumia kufugia samaki. Soil structure ni muhimu sana.

La muhimu zaidi ni kuangalia chanzo cha maji, na lazima maji yapimwe mapema. Haya ni machache ambayo ni basic.
 
Jamani tusaidiane chanzo cha maji kinachofaa. Maji ya mto, ya bomba, au ya kisima? Tusaidiane tafadhali, je maji ya bomba yanafaa kufugia samaki?

Maji yaliyo salama kwa ujumla wake yanafaa, ila maji yenye chemicals hayafai. Kabla hujaanza kufuga inabidi upime Ph, acidity, alkalinity, dissolved oxygen, seapage kama ni bwawa la kuchimba,na salinity. Mtalaam atakupa data za maji yanayotakiwa.
 

watu hao wana wivu wa maendeleo. Unadhani watu kama hao wataweza kuwatunza hao samaki wakiachiwa?.

Nahisi hamana fikra za kiujasiria mali.
"wivu haujengi" hali kama hii inasababishwa pia na ufinyo wa elimu hivyo msiwalaumu kwa kuwa ni wajinga (hawaja elimika).

Kwa upande wangu niliwahi kumshauri mzee wangu ampe ruhusa mtu mwenye uwezo wa kulima shamba la mpunga alilo nunua mwaka 2009 kwa misimu mitatu bila malipo yeyote kwa sababu hakuwa na mpango wa kulitumia na lilikuwa linazidi kuwa pori.
 
Asanteni sana wadau namimi naomba kuchangia!

Ni vizuri sana ukafanya EXTENSIVE POLYCULTURE ni kimaanisha ufuge samaki wa aina tofauti kwenye bwawa moja na hii kutokana na utafiti ya kuwa ukifuga Tilapia pekee kwenye bwawa wanazaliana sana na ukuaji wake unakuwa shida na ukubwa wa samaki unauwa mdogo kwa vile wanagombania chakula!

Hivyo basi ukiweka kambale wao wakuwa kama simba porini kwa ajili ya kupunguza vitoto vya samaki kwa kuvila(Predetors)

Njia hii haitaji ununue vyakula vya samaki unatumia mbolea kama samadi, mboji bmolea ya mbuvi hata Nguruwe na hii inasaidi sana kupunguza gharama za vyakula ambapo pia hadi sasa hatujaweza kuzalisha vyakula vya kiwango.

Nina project hapo BWAI unaweza kuni pm ila haihusiani na Aquaculture ila tunaweza kushirikiana kuinvest pamoja ni dream yangu na hivi ninavyoandika ni kwa workshop inayohusiana na mabo hayo unaweza yapata kupitia IFOAM.


Asanteni.
 

Polyculture ni nzuri, lakini lazima iwepo formula, ili kama naanza na tilapia 400 ktk bwawa la 10m x10m natakiwa niweke kambale wangapi. Bila formula unaweza ukashangaa tilapia wanaishia.

Njia nyingine ya kisasa ni kuchukua samaki wa jinsia moja tu kama unalenga kufuga kibiashara. Ukiweka mavi ya nguruwe kama unafuga kibiashara unaweza kimbiza wateja wako. Weka usiku watu wasikuone.

BWAI ndio wapi mkuu? Na IFOAM ni nini?
 

Ah ah ah ah! umenichekesha sana mkuu! ulikuwa ni mfano tu! ki imani Nguruwe itawakwaza wengi.

Nakubaliana haswa na wewe issue ya kukadilia predators na kwa kweli ni seme haya mambo siyo ya kufanya kienyeji ni lazima wataalam watumike.
BWAI ni eneo lipo Musoma vijijini ndilo mdau mwenye bandiko alitakufanyia mradi wake.

IFOAM ni International Federation Organic Agriculture Movement. Ambapo Organic Aquaculture inahusika.

Asante mkuu kwa kushare.
 
I wish I could be your apprentice, at least I could observe what's really into field with fish and all that. Kazi zinanibana aisee, but I hope to get that virgin chance one time and learn all about fish growing and market, otherwise thanks
 
Thanks much mkuu! Mungu akubariki sana sana!
 

Poa,

Nimeanza kufuga kienyeji kidogo kwa kukamata kambale pori na kuwafuga, jaribio la kwanza nimefaulu, sikuwapima uzito nilipowakamata,ila volumewise wamefikia viwango vizuri. Hawa IFOAM hawa website? Natamani sana kulima kilimo hai,yaani organic farming.
 
thanks guys for contributions in here, i attest today i have learned a lot from this thread!
 

Hiyo safi sana Malila! labda ugemwaga na aina ya bwawa ulilolima hili wadau tufaidike pia kwani hilo nalo ni tatizo! IFOAM wanayo website na ukigoogle IFOAM utapata mkuu.

Pia tanzania wana mshirika wao anayeitwa TOAM Tanzania Organic Agriculture Movement kama upo dar wanaweza kukupa mwanga haswa organic Aquaculture ingawa nashauri sana kwanza tufanye convesional aquaculture kwani the opposite bado tuna vikwanzo sana kulingana na viwango vya kimataifa!

Pia kwa knowledge zaidi ingia Organic Services:-international consultancy.
 

Niweke picha au nitoe maelezo.
 
Niweke picha au nitoe maelezo.

Mkuu maelezo ni muhimu sana lakini usisahau kuwa picha pia uzungumza vitu kibao! so utachoona au napendekeza yote mawili!

Thanks as always!
 
Mkuu maelezo ni muhimu sana lakini usisahau kuwa picha pia uzungumza vitu kibao! so utachoona au napendekeza yote mawili!

Thanks as always!

Vuteni subira kidogo,kama week moja hivi, niko mkoani, nikirudi Dar nitawawekea picha ya fish ponds zangu.
 

Kuna sehemu ukilima msimu wa kwanza wakiona mazao unayopata hawakutaki tena, wanaanzisha zengwe wanasema huyu tajiri wa Dsm anatuletea fujo.
 
nipm nikupe contact za afisa uvuvi mtaalam sana ye nimstaafu kwa sasa wengi anawafanyia hizo kazi but yupo Iringa town
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…