Ni namna gani ninaweza kuzuia upotevu wa maji bwawani (seepage and evaporation) kwa mimi mfugaji mdogo?
Kwa ufugaji wa kawaida, idadi ya samaki kwa cubic meter ni 40. Hivyo kwa tanki kama hilo utaweka samaki 400.Kwa idadi hii utahitaji kufanya water exchange 15-20% kwa kila baada ya siku tatu. Ila kwa yale marefu ambayo utahitajika kukata nusu hivyo itakuwa samaki 200. Ukitaka kufanya intensive farming katika tank hilo: samaki 120 kwa cubi meter, hivyo utaweka samaki 1200. Kwa idadi hii utahitajika kufanya water exchange kwa kila 1-2 hours na hewa ya ziada au maji yawe yanaingia na kutoka wakati wote bila-hewa ya ziada haitajika. Yale matanki ulioliza hayapo hapa lakini unaweza kutengeneza. Karibu
Toa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.
Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.
Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.
Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.
Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.
Huwezi kuvitundika hapa?
mkuu vifaranga wa sato wanauzwaje?
wapi wanapatikana?
na wa kambale?
KAMA KUKU WANAVYOWEZA kukuzwa kwa wiki 6 KUNA TECH YEYOTE au BREED type ya samaki wa mda mfupi ili uweze pata faida ktk mda mfupi?kama kuku/ wataalamu wa sayansi watujuze
Wana JF nimepata eneo la Heka 4, kandokando ya ziwa, wilaya ya chato ninataka nifuge samaki aina ya Sato, ninahitaji maelekezo namna ya kuchimba bwawa, kulea samaki na chakula cha samaki. kifupi, sijui A-Z ktk mradi huu
Habari wana JF,Nimejenga kabwawa ka samaki nyumbani kwangu kwa ajiri ya majaribio ya biashara ya ufugaji samaki naomba anayejua mbegu nzuri za samaki zinazotamba ktk soko pia ningependa kujua vyakula mda wa kuvuna pia DOs and Don't za hii biashara ya ufugaji samaki
sina uhakika kama kuna tofauti ya sato na pelege, ninachojua ni kuwa wote ni sato. (tilapia) katika kundi hili la sato au tilapia kuna mgawanyiko wa aina na aina ya samaki hawa, humo ndimo unakutana na hii jamii ya pelege. ngoja nimyumie copy Malilanipo vikindu mkuranga nataka nifuge sato au pelege bwana ni ukubwa wa chumba cha kawaida.
Karibu mkuu. Eneo lako lipo wapi? Je, eneo lina udongo wa aina gani? Una maji ya kutosha (hanzo chako cha maji)?. Sato ni Perege na Perege ni Sato. Sangara wapo katika majaribio. Karibu