Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Bsc.in fisheries and aquaculture..ndo ujuz nlio.nao..na fan yangu..toka chuo.kikuu cha.UDSM.capable in fish feed manufacturing...and all about ufugaji wa samaki.tuwasiliane.0717451771
 
DASAF...at UDSM....tupo wataalamu wa hayo.maswala wakutosha...na uwez pata shida.(department of aquatic science and fisheries at UDsm)
 
Chalengea ni.nying wataalamu.bado tunaendelea na research mbalimbali.juu ya haya maswala ya ufugaj wa viumbe majin.
 
Habar ndugu.binafsi ni mtaalamu wa maswala ya ufugaji wa viumbe wa majin wakiwmo samak.toka chuo.kikuu cha dsm..Sikushauri utumie gogle kupata ufahamu ni mana mazingira yanatofautiana baina ya eneo na eneo.ninawez kukusaidia vifaranga bora.vya monosex wa tilapia.na mambo mengne kama.ulishaj.na kadhalika.wasiliana.na mm.0717451771 muhala fadhili
thread ya miaka minne iliyopita!!!!
 
Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

--------------------------

Uvuvi%2Bbusega%2B4.jpg



-----------------------------






*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments

Ni kwel madume wanakua vizur lakin inategemea na aina ya samaki ndugu yangu.kwa nile tilapia.(sato) hawa ni sawa kabisa kua madume ndio more prefereble than female.lakin si kwa aina zote.unapotak kutengeneza monosex lazima ujue species ako.na ipi.ni bora
 
Wadau wa JF.
Mpaka sasa bado sijapata reliable supplier wa chakula cha samaki (sato) ambacho ni floating pellets.

Kuna jamaa wanaagiza toka Uganda, ila mara nyingi wanaishiwa na chakula hicho na inawachukua muda sana kuagiza tena.

Wana - JF naomba mniarifu kuhusu wapi naweza kupata chakula cha samaki ambacho ni floating pellets.

Asanteni.
 
Nami nimenufaika sana kwa michango ya wadau wa hili jukwaa, hakika JF ingekuwa hivi kila siku hakuna ambaye angebaki nyuma kimaendeleo. Nami napenda kuongezea nondo zifatazo kwajili ya ufugaji samaki.

1.Namna ya kuzalishaji wa vifaranga bora wa SAMAKI

i.Chagua samaki wazazi wazuri kulingana na umbile lao kama rangi, ukubwa, afya na sura zao. Samaki hawa watengwe na wale wasio na sifa hizo na wasiruhusiwe kuzaliana nao. Mfugaji anaweza kununua wazazi hawa kutoka katika chanzo kinachofahamika kuwa kina samaki bora.

ii.Dhibiti ubora wa samaki hawa wazazi kwa kutoruhusu miingiliano na samaki wenye ubora hafifu. Chuja vema maji yanayoingia bwawa. Ikiwezekana, tumia samaki wenye ukubwa wa zaidi ya gramu 100. Hii itakuwezesha kutenganisha wazazi kutoka kwa vifaranga kila baada ya kuzaliwa (reproduction cycle).

.Endelea kuwatumia wazazi hawa kila unapohitaji vifaranga kutegemeana na jinsi wanavyoendelea kuzaa vifaranga bora. Pamoja na ubora wa wazazi hawa, kuna umuhimu wa kuchagua na kuwaondoa vifaranga wasio kuwa na ubora unaohitajika au ambao ubora wao unatiliwa mashaka (culling).

iii.Ni muhimu mfugaji afahamu uzuri wa kutumia vifaranga bora. Kausha bwawa kabisa angalau mara moja kila baada ya miezi sita hadi nane ili kuondokana na samaki wasio na ubora unao hitajika, kuua maadui wa samaki na kuondokana na hali ya kuwa na samaki wengi kwenye bwawa zaidi ya kiwango kinachotakiwa na pia hali ya samaki kuzaliana kinasaba "inbreeding". "Culling na grading" ni muhimu kuanza baada ya siku 30 hadi 45 baada ya samaki wakubwa kuwa wamewekwa kwenye bwawa na hufanyika kwa kutumia kawavu kadogo ambacho kina matundu madogo.
Endelea kufanya kazi hii kila baada ya wiki mbili hadi nne.

2.URUTUBISHAJI WA BWAWA NA ULISHAJI WA SAMAKI

i.Mfugaji anashauriwa kuweka mbolea ya asili kama Mboji na samadi kwenye maji kabla ya kupandikiza samaki. Hii ni muhimu kwani samaki watakaopandikizwa, watahitaji chakula siku hiyo hiyo na chakula chao cha awali huwa ni vijimea na vijidudu vilivyomo ndani ya maji. Vyote hivi huwepo kwa wingi kwenye maji yenye rutuba.

ii.Iwapo maji yatakuwa yamerutubishwa vema, chakula cha ziada huhitajika kwa kiasi kidogo sana, kama (2-3%) ya uzito wa samaki husika kwa siku. Ni vema samaki wakalishwa angalau mara mbili, kiasi kidogo asubuhi ya kati ya saa tatu na nne na jioni kati ya saa 10 na 11. Pia ni vema kama eneo la kulishia ikawa ni sehemu moja ili kuwazoesha samaki kuja eneo hilo muda wa kulisha na kuwawezesha kula sehemu kubwa ya chakula watakachopewa.

3.KUZALIANA KWA WINGI NDANI YA BWAWA NA NJIA ZA KUDHIBITI

KUWEPO KWA SAMAKI WENGI KULIKO IDADI INAYOTAKIWA NDANI YA BWAWA (OVERPOPULATION IN PONDS)
1. Kwa kawaida, samaki jamii ya perege wako katika makundi mawili kutegemeana na wanavyo tunza mayai/watoto wao wakati wa kuzaliana. Perege jamii ya Oreochromis aureus, O. mossambicus na O. niloticus hutaga kwenye viota lakini hutunza mayai/vifaranga vyao midomoni kwa ajili ya kuyalinda dhidi ya maadui.
2. Perege wa jamii ya T. rendalli na T. zilli hutaga na kutunza mayai/vifaranga vyao kwenye viota vinavyochimbwa na dume na jike kwa pamoja. Hulinda mayai/vifaranga vyao wakiwa kwenye viota na si kuwatunza kwenye midomo mdomoni panapotokea hatari.
3. Urahisi wa jinsi wanavyo zaliana ni moja ya sababu inayofanya perege afae kwa ajili ya kufugwa kirahisi. Lakini, tabia hii pia husababisha matatizo. Uwezekano wa kukuza vifaranga wengi ni mkubwa na husababisha kuwepo samaki wengi kwenye bwawa kuliko uwezo wa bwawa. Matokeo yake samaki hudumaa kutokana na uhaba wa chakula, hewa na hata sehemu za mapumziko. Katika hali hii, kuna uwezekano mkubwa kukuta samaki zaidi ya asilimia 75% wakiwa na ukubwa wa chini ya uzito wa gramu 100. Kwa maeneo ambayo samaki wadogo huliwa, hili linawezekana lisiwe tatizo, lakini kama lengo ni kuuza na kujipatia fedha, samaki wa ukubwa huu huuzika kwa taabu au kwa hasara. Katika kuzuia hali hiyo ya kudumaa samaki isitokee, yafuatayo huweza kufanyika:


NJIA ZA KUWEZA KUDHIBITI UWINGI WA PEREGE KUTOKEA KWENYE BWAWA
1. Uvunaji wa mara kwa mara wa vifaranga kwa kutumia wavu. Njia hii hufaa kwenye bwawa dogo, ina shuruba na haihitaji uzoefu ili vifaranga wasife kutokana na majeraha watakaopata wakati wa kuwavua.
2.
Kutenganisha jinsia baada ya vifaranga kuwa na ukubwa wa kuweza kutenganishwa (monosex culture
3. Kwa kawaida, madume hukua haraka kuliko majike. Hivyo, wengi hupendelea kufuga madume
4. Kazi ya kutenganisha huweza kufanywa na mfugaji yeyote baada ya kuonyeshwa tofauti iliyopo kati ya jinsia moja na nyinge. Mkulima anashauriwa amuone mtaalam wa uvuvi aliye karibu naye kwa maelekezo.
5. Katika mchakato wa kuwatenganisha, makosa huweza kufanyika na kusababisha baadhi ya jinsia tofauti kutotenganishwa, mkulima asikate tamaa kwani idadi itakayokuwa imetenganishwa bado itatoa tija nzuri.
6. Kupandikiza vifaranga machotara (stocking hybrid "all-male" fingerlings: Madume hukua haraka kuliko majike
7. Utahitaji samaki wazazi waliohakikiwa ubora wake (requires pure strains of broodstock.
8. Utahitaji sehemu maalum ya kuzalishia na mtaalam aliyefuzu.
9. Ili kukidhi mahitaji ya vifaranga wa perege kwa wafugaji, kuna umuhimu wa wafugaji binafsi kuanzisha "hatcheries" kwa ajili ya kuzalisha vifaranga bora na kuwauzia wengine wenye kuhitaji. Japo kuwa kwa sasa baadhi ya wafugaji huzalisha vifaranga na kuwauzia au kuwagawia wenzi wao, wafugaji hazalisha vifaranga hao kama sehemu ya uzalishaji wa samaki wa kawaida kwenye bwawa. Kwa kadiri shughuli hii inavyokuwa, wafugaji wengi hupendelea kupata vifaranga bora. Na kwa jinsi hii, "hatchery" itakayokuwa ikizalisha vifaranga bora itapata soko zuri la vifaranga wake.
UZALISHAJI WA VIFARANGA


Uchaguzi wa mbegu bora (wazazi)
Samaki aina ya perege huzaliana wakati wote wa mwaka. Wana tabia ya kuzaa vifaranga wengi. Samaki
wazazi huweza kufugwa kwenye mabwawa au matanki wakiwa wanasubiri kuzaliana. Idadi ya mayai
yatakayotagwa na perege jike hutegemea ukubwa wa kimaumbile wa samaki jike. Kwa kawaida majike
wadogo hutaga mayai machache wakati wale wakubwa hutaga mayai mengi. Hii hutokana na uwezo wa
tumbo kuweza kubeba idadi ya mayai.

Inawezekana kutofautisha perege dume na jike kwa urahisi wanapokuwa na uzito wa gramu 15. Perege
jike ana tundu moja katikati ya mapezi matatu yaliyo karibu na mwisho wa mkia eneo la tumboni. Kwa
upande wa dume eneo hilo hilo kuna mrija uliojitokeza kwa nje.

UZALIANAJI WA PEREGE

Kama ilivyokwisha elezwa hapo juu, perege ni moja ya aina ya samaki ambao huweza kuzaliana kwenye
maji yaliyozingirwa (captivity) kama vile bwawa la kuchimbwa na hata tenki.

Ili mfugaji atape mbegu bora, ni vema akaanda mazingira mazuri yatakayopelekea kupatikana kwa
mbegu (vifaranga) bora. Hatua zifuatazo ni muhimu:

1. Chagua samaki wazazi na kuwaweka kwenye bwawa au tenki uliloliandaa kwa kuzalishia vifaranga. Uwiano unaopendekezwa ni wa samaki majike 2 kwa dume 1. Huyo dume mmoja ana uwezo wa kurutubisha mayai ya majike hayo2. Ukiweka madume wengi, watakuwa wakigombana wao kwa wao badala ya kuzaliana. Chagua samaki wenye ukubwa na umbo linalofaa na linalopendeza.
2. Mara tu baada ya vifaranga kuanguliwa huweza kuogelea wakiwa wamejichukulia kiini cha yai (yolk sack) ambacho hutumika kama chakula kwa muda wa siku 2 –3. Baada ya hapo, vifaranga uanza kujilisha vimelea (planktons) vitakavyokuwa vikipatikana ndani ya maji. Baada ya muda, vifaranga hao watakuwa na uwezo wa kuendelea kula vimelea hivyo, vijidudu na hata chakula cha ziada kama pumba za mahindi, za mpunga kama watapewa kama chakula cha ziada. Waachwe wakue kwa muda wa wiki tatu au zaidi kabla ya kuwahamisha kwenda kwenye bwawa la kukuzia. Kwa kuwa vifaranga hawa watakuwa na umri mmoja (ni wa rika moja), ukubwa sawa na ni wachanga, watakuwa na uwezo mkubwa wa kukua kwa ubora zaidi.

UHIFADHI WA MBEGU KWA AJILI YA MZUNGOKO MWINGINE WA UPANDAJI SAMAKI BWAWANI NA MATATIZO KATIKA UFUGAJI SAMAKI..

Unapovuna samaki, hakikisha kuwa vifaranga au samaki wazazi utakaokuwa umewachagua wanawekwa katika kijibwawa kingine (kinachojulikana kama nursery pond) kabla ya kuwarudisha bwawa la kukuzia (production pond). Ni muhimu kufanyia bwawa matengenezo na kulijaza maji kabla ya kuweka samaki tena. Hili ni muhimu kwa mfugaji kwani kinamhakikishia mfugaji kujua kuwa anapanda mbegu changa na ambao hawajadumaa. Pia humhakikishia kujua kuwa samaki waliopandwa wanalingana na ujazo wa bwawa, yaani vifaranga viwili kwa kila mita moja ya mraba na pia hurahisisha maji ya bwawa kurutubika kirahisi.

MATATIZO YA UFUGAJI SAMAKI
Ingawa ufugaji wa samaki si kazi ngumu sana, kuna matatizo mbali mbali ambayo mfugaji anaweza
kukumbana nayo. Lakini, matatizo mengi yanaweza kuepukika kama mfugaji ataweza kufuata kikamilifu
maelekezo ya ujengaji na utunzaji wa bwawa.
1. Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Iwapo utakumbana na tatizo hili, muone afisa uvuvi aliye karibu nawe upate ushauri.
2. Tatizo la maadui wa samaki kama vile ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Kwa kiasi kikubwa tatizo hili huambatana na ujengaji bwawa mbali na nyumbani na bwawa kuwa na nyasi nyingi (halifyekewi). Suluhisho ni kufweka nyasi kila mara, kujenga uzio kwa kutumia matete na hata nyaya za seny'enge, kuwinda ndege na kuharibu mazalia/maskani yao, bwawa kuwa karibu na maskani ya watu.
3. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa. Tatizo hili hutokana na kutokukaushwa bwawa kwa kipindi kirefu. Utatuzi huweza kuwa; kukausha bwawa kila baada ya miezi 6 hadi 9
4. Ugumu wa kukausha maji bwawani. Husababishwa na bwawa kujenjwa kwenye eneo la tambarare kiasi kuwa hakuna uwezekano wa kutumia bomba au kukata kuta za bwawa kuondoa maji. Utatuzi; chimba bwawa kwenye eneo lenye mteremko wa wastani
5. Bwawa lisilo kaushika huwa mazalia ya Mbu wakati linapokuwa halina samaki ndani yake na kusaidia kuenea kwa malaria. Konokono wenye mabuu ya kichocho huzaliana kwenye mabwawa yenye kina kifupi au yenye majani mengi. Ni vema kuwa na bwawa yenye kina cha kutosha, lisilo na nyasi au majani ndani yake na linaloweza kukaushika kirahisi ili kuondokana na matatizo haya.
Matunzo, uvunaji wa samaki na zana ziazotumika kuvulia samaki

MATUNZO YA SAMAKI BWAWANI.

Ili bwawa liweze kutoa samaki wazuri muda wote yafaa bwawa la samaki lihudumiwe kwa kufuata
maelekezo yafuatayo;
1. Angalia samaki wanavyoogelea na kula wakati unapowalisha. Kama hawana matatizo, watajitokeza juu kwa wingi na kula vizuri kwa furaha.
2. Ondoa magugu na mimea katika bwawa.
3. Fyeka majani kando kando ya bwawa.
4. Angalia kila siku kiasi cha maji kama yananywea au hayanywei, yanatosha au hayatoshi.
5.
Angalia rangi ya maji ili ujue kama unahitaji kuongeza mbolea.
6. Chunguza kama kuna ndege na wanyama waharibifu na ukiwabaini, wadhibiti mapema.


UVUNAJI WA SAMAKI.

Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea wanavyokula, wingi wao bwawani na joto la maji. Samaki wanakuwa haraka kwenye maji ya joto kuliko kwenye maji ya baridi. Pia mfugaji mwenye bidii ya kulisha na kutunza bwawa, samaki wake watakua haraka. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 9.
Ni ukweli usiopingika kuwa; kwa kadiri juhudi na maarifa yanavyoongezwa katika bwawa, ndivyo kiasi cha samaki kitakachovunwa kitakavyoongezeka.

ZANA ZITUMIKAZO KATIKA UVUNAJI SAMAKI

Kwa kawaida, kuna makusudi mawili ya kuvuna samaki waliofugwa bwawani:
1. Kwa ajili ya kitoweo au kiasi kidogo kwa ajili ya kuuza.
2. Uvunaji wa samaki wote ili kuhitimisha msimu mmoja wa ufugaji samaki.
Kwa samaki wachache wa mboga au kuuza, unaweza kutumia kipande cha nyavu, mitego ya asili (migono), ndoano na hata kipande cha nguo. Kwa uvunaji wa samaki wote ili kuhitimisha msimu wa ufugaji, njia nzuri ni kuondoa maji yote kutoka katika bwawa na kukamata samaki wote mara moja. Unaweza kuondoa maji kwa namna mbili:
• Kukata ukuta ulio upande wa kina kirefu, weka chujio ili kuzuia samaki kutoka halafu ruhusu maji kutoka.
• Kutumia bomba la kuondolea maji kwa kufunikwa na kipande cha nyavu au kitu cho chote kisichoruhusu samaki kutoka bwawani isipokuwa maji.
Njia hii ni muhimu kwani isipofanyika kwa kipindi kirefu, samaki watakuwa wengi mno bwawani na kusababisha wengi kudumaa na kuwa na umbo dogo.
Samaki wanaofugwa bwawani huweza kuliwa wabichi baada ya kupikwa, kuchomwa, kukaangwa au kuuzwa kwa wanaohitaji.
Mfugaji pia anaweza kuuza samaki wachanga (vifaranga) kwa watu wenye kuhitaji mbegu za kupanda.
Baadhi ya samaki wakubwa wanaweza kukaushwa kwa moto, moshi, jua au kutiwa chumvi ili wasiharibike au kuoza upesi. Hii ni katika kuwahifadhi.

URUTUBISHAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MBOLEA NA (MAJIVU) PAMOJA NA USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI.

1. Kutegemea aina ya udongo, majivu ya moto huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuingiza maji ili kupunguza Tindikali ya udongo na kuua baadhi ya wadudu walio maadui wa samaki waliopo katika eneo la bwawa.
2. Mbolea huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuweka maji ili kusaidia kujenga mazingira ya maji kutuama (yaani Kushikamanisha udongo).
3. Vinginevyo, mbolea huwekwa eneo maalum (Uzio) mara baada ya maji kuingizwa bwawani ili kulirutubisha na Kuliwezesha liwe na vijimea na vijidudu vidogo vidogo vitakavyokuwa chakula cha awali cha samaki.
4. Dalili za kuwepo kwa vijimelea hivyo bwawani ni kugeuka rangi ya maji na kuwa ya kijani.
5. Aina ya mbolea hutegemea upatikanaji wake. Samadi ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na hata Majani mabichi yaozayo kirahisi na yasiyo sumu kwa wanyama na binadamu huweza kutumika.
6. Kiasi cha kuweka mbolea hutegemea sana ukubwa wa bwawa, aina ya samadi na idadi ya samaki waliomo.
7. Kipimo kizuri cha kiasi kinachotosha ni kuingiza mkono ndani ya maji hadi kufikia kwenye kiwiko, na usipoona Kiganja chako, basi simamisha uwekaji wa mbolea kwani vijimelea na vijidudu waliomo wanatosha kulisha samaki Waliomo kwenye bwawa kwa muda wa siku kadhaa.
8. Ukizidisha mbolea ni hatari kwa samaki, kwani wanaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni, hasa nyakati za usiku.



USAFIRISHAJI, UPANDAJI NA ULISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI

USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI
Upatapo vifaranga, visafirishe wakati wa asubuhi kwa kutumia ndoo ya plastiki, chungu, maplastiki makubwa.

Weka kiasi cha vifaranga 200 katika ndoo moja. Ni vema mkulima kuwa na tabia ya kupunguza maji
kwenye ndoo yenye samaki na kuweka mengine afikapo eneo lenye maji.

Ufikapo bwawani
, inamisha ndoo ili maji ya kwenye ndoo yaingiliane na yale ya bwawani.
Hii ni kuruhusu joto la maji na mazingira ya maji yaingiliane na kuwa sawa.

Waruhusu samaki watoke bwawani wenyewe bila ya kuwamwaga. Itachukuwa muda kabla ya vifaranga wote kuingia bwawani. Kwa kufanya hivyo, samaki hawatapata mshituko ambao wanaweza kupata kama
watamwagwa. Mshituko wa ghafla huweza kusababisha vifo.


UPANDAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI.
Ubora wa samaki utakao wafuga utategemea sana ubora wa vifaranga utakaokuwa umepanda bwawani.

Chanzo chako cha vifaranga ni bora kiwe na vifaranga wenye umri mdogo na ambao hawajadumaa.

Kwa samaki aina ya Perege, panda vifaranga viwili (2) hadi watatu (3) kwa kila mita moja ya mraba.

Kwa sasa, samaki aina ya Perege ndio wanaoshauriwa kufugwa na wafugaji wa maji baridi hapa nchini.

Kambale huweza kufugwa na mkulima mzoefu kwani huduma yake huitaji mtaji mkubwa katika
kuwalisha na Utaalam katika kuzalisha vifaranga vyake.


ULISHAJI WA SAMAKI.

1. Samaki, Kama walivyo wanyama wengine, wanahitaji kula.
2. Chakula cha samaki huweza kugawanywa katika makundi mawili:-
3. Cha asili kipatikanacho ndani ya bwawa kama vile vijimea, vijidudu na samaki wadogo.
4. Cha ziada ambacho huongezwa bwawani na mkulima.
5. Ili chakula cha asili kipatikane bwawani, ni vema bwawa liwe limerutubishwa vizuri, kwani vijimea vinavyotarajiwa humea palipo na rutuba.
6. Chakula za ziada huwekwa bwawani na mkulima mwenyewe. Aina ya chakula cha ziada hutegemea upatikanaji wake, gharama na aina na ukubwa wa samaki. Baadhi ya chakula cha ziada ni kama: pumba za mahindi, za mpunga, mashudu ya pamba na karanga, machicha ya pombe, ugali na masazo ya jikoni, baadhi ya majani pori, majani yatokayo bustanini.
7. Inashauriwa mfugaji alishe kila siku, kwa muda ule ule, saa ile ile na sehemu ile ile. Tabia hii hujenga mazoea ya samaki kula zaidi na kupunguza wingi wa chakula kinachopotea.
8. Usilishe chakula kingi zaidi ya mahitaji ya samaki kwa siku hiyo. Mfano, usiweke debe zima la pumba kwa mara moja na kuacha kulisha kwa wiki nzima! Sehemu ya chakula kitakachosalia, kitaoza na baadhi ya siku samaki hawatakuwa na chakula, watashinda na kulala njaa!




PART II

UFUGAJI WA SAMAKI: MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI


Hili ni bwawa la kuchimbwa chini, lipo katika kituo cha ufugaji wa samaki cha serikali kilchopo Kingolwira mjini Morogoro. Yapo na mabwa mengine mengi kama yanavyoonekana pembeni mwa bwawa hili.


Hii ni aina nyingine ya bwawa lililochimbwa na kujengwa kwa simenti na kulifanya liwe imara zaidi. Nalo lipo katika kituo cha ufugaji wa samaki Kingolwira mjini Morogoro.

Bwawa hili limejengwa pia kwa simenti kutoka usawa wa ardhi kwenda juu, ni la mduara kama linavyoonekana kwenye picha hii. Yapo mabwawa mengi ya aina hii katka kituo cha kufugia samaki Kingolwira mjini Morogoro.

Ufugaji wa samaki unamanufaa sana kwa mfugaji kwani unaweza kumuondolea Mtanzania umaskini huku akiendelea kujipatia kitoweo. Soma zaidi HAPA kuhusu jinsi ya kuanza kufuga samaki na ufugaji wenyewe.

VIDEO ZINAZOHUSU SAMAKI TANZANIA
Video hii inaonyesha baadhi ya wanachi wa mkoa wa Kagera walioamua kunzisha miradi ya ufugaji wa samaki. Wameamua kufuga samaki baada ya kuona upatikanaji wa samaki Toka ziwa Victoria umekuwa mgumu sana na uhitaji wa samaki ni mkubwa sana. Waliamua kuanza kidokidogo na hatimaye miradi yao kuendelea kukua kadri siku zinavyoendelea.
Kuna uhaba mkubwa sana wa samaki Tanzania, ukipita katika masoko ya samaki hasa asubuhi utaona wafanyabiashara wanavyogombania samaki. Hii inaonyesha msisitizo kuwa uhitaji wa samaki Tanzania ni mkubwa na watu wengi wanahitajika kuingia katika ufugaji wa samaki. Itawasaidia kujikwamua kimaisha lakini pia kuwafanya Watanzania wengi wapate kitoweo cha samaki. Tazama video hii hapa chini inayoonyesha uhaba wa samaki Tanzania hadi kulazimika kuagiza nje ya nje ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani.




PART 3

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE BWAWA

"NINA SHAMBA MAENEO YA BUNJU DAR ES SALAAM. NINGEPENDA KUFUGA SAMAKI KIBIASHARA. MAJI YA UHAKIKA NI YA KISIMA NA YANA CHUMVI KIASI. NAPENDA KUPATA MAELEZO ZAIDI YATAKAYONIWEZESHA KUANZA UFUGAJI HUU."

Wakulima wanaweza kuongeza kipato kutokana na ufugaji wa samaki katika maeneo yao
UFUGAJI WA SAMAKI KAMA ILIVYO SHUGHULI NYINGINE YOYOTE YA KIUCHUMI INAHITAJI USIMAMIZI MZURI ILI UWEZE KUWA NA FAIDA. MBALI NA HILO, MFUGAJI WA SAMAKI ANATAKIWA KUZINGATIA VIGEZO VINGI KABLA YA KUANZA UFUGAJI. MOJA YA VIGEZO HIVYO NI SOKO. SI JAMBO LA BUSARA KUANZA SHUGHULI YOYOTE KABLA HAUJAFANYA UCHUNGUZI NA KUJUA KAMA KUNA MAHITAJI YA BIDHAA UNAYOKUSUDIA KUZALISHA. WAFUGAJI WENGI WAMEANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI LAKINI WAKAISHIA KUPATA HASARA KUTOKANA NA UKOSEFU WA SOKO. NA WENGINE WAMEANGUKA KUTOKANA NA UTUNZAJI MBOVU WA MABWAWA YA SAMAKI.

MAJI
UPATIKANAJI WA MAJI NA UBORA WAKE NI KIGEZO MUHIMU KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI. MTIRIRIKO WA MAJI NI NJIA RAHISI KWA MFUGAJI. MAJI MACHAFU HAYATAKIWI KWA UFUGAJI WA SAMAKI. WAFUGAJI NI LAZIMA WASAIDIWE NA MAAFISA KILIMO KATIKA ENEO LAO KAMA MAJI YANAYOPATIKA YANA UBORA KWA AJILI YA UFUGAJI WA SAMAKI. KWA WAKAZI WA DAR ES
SALAAM, INAWEZEKANA PIA KUFUGA SAMAKI KWENYE BWAWA, ENDAPO MAJI YANA CHUMVI YA WASTANI, NA KWA KIWANGO KINACHOSHAURIWA KITAALAMU, BASI SAMAKI WANAWEZA KUSTAHIMILI, NA KUKUA VIZURI.

BWAWA

BWAWA LA SAMAKI LINAHITAJI NAFASI KUBWA YA ARDHI, YENYE MWINUKO PAMOJA NA ENEO LA SAMAKI KUKIMBILIA. HII NI NJIA RAHISI YA UFUGAJI ENDAPO ARDHI NA MAJI HAVINA GHARAMA KUBWA. ENEO KUBWA ZAIDI LINARUHUSU UZALISHAJI USIOHITAJI NGUVU YA ZIADA NA WENYE TIJA.

UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MAENEO YENYE UDONGO WA KICHANGA KAMA DAR ES SALAAM, MFUGAJI ATALAZIMIKA KUCHIMBA NA KUWEKA KARATASI YA NAILONI. HII, ITASAIDIA KUZUIA UPOTEVU WA MAJI PAMOJA NA KUZUIA BWAWA KUPOROMOKA.

NI VYEMA UPANDE MMOJA WA BWAWA UKAWA NA KINA KIREFU KULIKO MWINGINE. UPANDE MMOJA UNAWEZA KUWA NA KINA CHA MITA MOJA NA NUSU, NA MWINGINE MITA MOJA. HII ITAMSAIDIA MFUGAJI KUWEZA KULIHUDUMIA BWAWA VIZURI, HATA KAMA NI KUINGIA NA KUFANYA USAFI.

UTUNZAJI WA BWAWA

INASHAURIWA KUFANYIA BWAWA USAFI MARA KWA MARA, HASA KWA KUONDOA MAJANI ILI KUEPUSHA WADUDU KUFANYA MAKAZI NA HATIMAYE WAKAWADHURU SAMAKI. PIA UKIACHA MIMEA BWAWANI ITATUMIA VIRUTUBISHO KWA KIASI KIKUBWA NA KUONDOA HEWA YA OXIJENI.
HIVYO, KILA UNAPOONA UCHAFU, SAFISHA MARA MOJA.

ULISHAJI

WAFUGAJI WALIO WENGI, WAMEKUWA HAWAZINGATII KANUNI ZA ULISHAJI WA SAMAKI. KWA KAWAIDA INATAKIWA KUWALISHA SAMAKI MARA MBILI HADI MARA TATU KWA SIKU.

AINA YA CHAKULA

SAMAKI WANAWEZA KULISHWA KWA KUTUMIA PUMBA YA MAHINDI, MASHUDU YA PAMBA NA ALIZETI, SOYA, MABAKI YA DAGAA. HAISHAURIWI KULISHA CHAKULA KILICHOKO KWENYE MFUMO WA VUMBI, BALI KIWE MABONGE MADOGO MADOGO, KWA WASTANI WA TAMBI.

MAGONJWA

KWA KAWAIDA SAMAKI HAWANA MAGONJWA MENGI SANA YANAYOWASHAMBULIA, ILA KUNA BAADHI YA YALIYOZOELEKA KAMA VILE MAGONJWA YA UKUNGU (FANGASI), MAGONJWA YATOKANAYO NA VIRUSI, PAMOJA NA MINYOO.

SAMAKI WANAPOSHAMBULIWA NA FANGASI, HUONEKANA KWA MACHO KWA KUWA HUWA NA MADOA MADOA. SAMAKI AINA YA KAMBALE HUSHAMBULIWA ZAIDI KULIKO PEREGE.

PIA UNAWEZA KUTAMBUA KUWA SAMAKI NI MGONJWA KWA KUWA HUZUBAA SEHEMU MOJA KWA MUDA MREFU. MAGONJWA KWA SAMAKI PIA YANAWEZA KUTOKANA NA MRUNDIKANO KWENYE BWAWA. HIVYO, NI MUHIMU KUWAPUNGUZA KILA WANAPOONGEZEKA.

TIBA

TIBA ILIYOZOELEKA KWA SAMAKI NI KWA KUWEKA CHUMVI KWENYE MAJI, KASHA KUWATUMBUKIZA SAMAKI UNAOWAONA KUWA NI WAGONJWA, KISHA KUWATOA NA
KUWARUDISHA BWAWANI.

UPATIKANAJI


UNAWEZA KUPATA VIFARANGA WA SAMAKI KUTOKA KATIKA KITUO CHA KUZALISHA NA KUFUGA SAMAKI KINGOLWIRA MOROGORO. BEI YA KIFARANGA CHA PEREGE NI SHILINGI 50, NA KAMBALE NI SHILINGI 150
 
Wadau wa JF.
Mpaka sasa bado sijapata reliable supplier wa chakula cha samaki (sato) ambacho ni floating pellets.
Kuna jamaa wanaagiza toka Uganda, ila mara nyingi wanaishiwa na chakula hicho na inawachukua muda sana kuagiza tena.
Wana - JF naomba mniarifu kuhusu wapi naweza kupata chakula cha samaki ambacho ni floating pellets.

Asanteni.

Kuna post humu ya ufugaji wa samaki itafute ina mambo mengi inaweza saidia, na kama hupo dar kama hautojali naomba nije kuona bwawa lako maana nilijaribu kufuga kwenye bwawa perege na kambale wakawa wanakufa nahisi ni maji yalikuwa machafu ningependa pata experience zaidi
 
Mkuu, kwanza nikupongeze kwa kujihusisha na ufugaji wa samaki kwani inaonesha kuwa watanzania sasa tumeanza kuamka na kuchangamkia fursa hii hapa nchini.
Kuhusu chakula cha samaki hususani sato kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kumpata reliable supplier kwa hapa nchini kwani bado hatujawa na industry zinazojihusisha na kutengeneza aquafeeds kwa ubora hapa nchini. Tofauti na jirani zetu wanaotuzunguka kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Mozambique ambao wao wamepiga hatua kubwa sana katika ufugaji wa samaki na hvyo kuweza kuanzisha viwanda vya kutengeneza vyakula vya samaki.
Ushauri mdogo ninaoweza kukupa ni kuwa jaribu kuformulate chakula cha samaki ww mwenyewe kwa kutumia mchanganyiko wa dagaa, soya, pumba za mpunga, mashudu ya alizeti pamoja na mchanganyiko wa vitamin na minerals katika ratio inayofaa kwa kila mojawapo ya hvyo nilivyotaja ili kupata chakula kamili chenye kiac kinachotakiwa cha protini, wanga, madini, mafuta na vitamini kwa ajili ya ukuaji bora wa samaki.
Baada ya hapo ili kupata pellets unaweza kutumia mashine za kawaida (pelletizing machine) zinazopatikana sehemu mbalimbali hapa nchini. Kwa upande wa floating pellets unaweza kuongea na watu kwenye viwanda vikubwa vya kutengeneza vyakula mbalimbali vya mifugo katika mfumo wa pellets kama vile hill feeds bagamoyo au tan feeds morogoro wanaweza kukutengenezea floating pellets kwa kutumia formulation yako ya chakula ulichokitengeza kama nilivyokuelekeza hapo juu. Hii wanaweza kukufanyia kwa makubaliano maalum na kwa kiac Fulani cha pesa hvyo basi unaweza kuondokana na tatzo la reliable supply ya chakula cha samaki kwa kutumia njia hyo hapa hapa nchini.

All the best mkuu !!!!!!!!
 
Wadau wa JF.
Mpaka sasa bado sijapata reliable supplier wa chakula cha samaki (sato) ambacho ni floating pellets.
Kuna jamaa wanaagiza toka Uganda, ila mara nyingi wanaishiwa na chakula hicho na inawachukua muda sana kuagiza tena.
Wana - JF naomba mniarifu kuhusu wapi naweza kupata chakula cha samaki ambacho ni floating pellets.

Asanteni.
Mkuu hebu jipe muda wa kufanya ziara pale SUA uonane na wataalam wa ufugaji samaki naamini pale watakupatia hadi formula ya kutengeneza hicho chakula. Nenda uonane na Dr. Benno Mnembuka mkuu wa idara ya sayansi ya wanyama, atakuelekeza mtu sahihi wa kutatua matatizo yako. Dar - Moro siyo mbali kivile.
 
Mkuu hebu jipe muda wa kufanya ziara pale SUA uonane na wataalam wa ufugaji samaki naamini pale watakupatia hadi formula ya kutengeneza hicho chakula. Nenda uonane na Dr. Benno Mnembuka mkuu wa idara ya sayansi ya wanyama, atakuelekeza mtu sahihi wa kutatua matatizo yako. Dar - Moro siyo mbali kivile.

Asante sana mkuu, nitatembelea huko hivi karibuni.
 
Mkuu, kwanza nikupongeze kwa kujihusisha na ufugaji wa samaki kwani inaonesha kuwa watanzania sasa tumeanza kuamka na kuchangamkia fursa hii hapa nchini.
Kuhusu chakula cha samaki hususani sato kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kumpata reliable supplier kwa hapa nchini kwani bado hatujawa na industry zinazojihusisha na kutengeneza aquafeeds kwa ubora hapa nchini. Tofauti na jirani zetu wanaotuzunguka kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Mozambique ambao wao wamepiga hatua kubwa sana katika ufugaji wa samaki na hvyo kuweza kuanzisha viwanda vya kutengeneza vyakula vya samaki.
Ushauri mdogo ninaoweza kukupa ni kuwa jaribu kuformulate chakula cha samaki ww mwenyewe kwa kutumia mchanganyiko wa dagaa, soya, pumba za mpunga, mashudu ya alizeti pamoja na mchanganyiko wa vitamin na minerals katika ratio inayofaa kwa kila mojawapo ya hvyo nilivyotaja ili kupata chakula kamili chenye kiac kinachotakiwa cha protini, wanga, madini, mafuta na vitamini kwa ajili ya ukuaji bora wa samaki.
Baada ya hapo ili kupata pellets unaweza kutumia mashine za kawaida (pelletizing machine) zinazopatikana sehemu mbalimbali hapa nchini. Kwa upande wa floating pellets unaweza kuongea na watu kwenye viwanda vikubwa vya kutengeneza vyakula mbalimbali vya mifugo katika mfumo wa pellets kama vile hill feeds bagamoyo au tan feeds morogoro wanaweza kukutengenezea floating pellets kwa kutumia formulation yako ya chakula ulichokitengeza kama nilivyokuelekeza hapo juu. Hii wanaweza kukufanyia kwa makubaliano maalum na kwa kiac Fulani cha pesa hvyo basi unaweza kuondokana na tatzo la reliable supply ya chakula cha samaki kwa kutumia njia hyo hapa hapa nchini.

All the best mkuu !!!!!!!!

Nashukuru sana kwa ushauri wako.
Naanza kuufanyia kazi.
Asante sana.
 
Kuna post humu ya ufugaji wa samaki itafute ina mambo mengi inaweza saidia, na kama hupo dar kama hautojali naomba nije kuona bwawa lako maana nilijaribu kufuga kwenye bwawa perege na kambale wakawa wanakufa nahisi ni maji yalikuwa machafu ningependa pata experience zaidi

Ngoja niangalie nafasi za weekend zijazo kama sitakua na safari za shamba tutawasiliana.
 
Kinatokea hapa hapa TZ?

Kwa kilo kumi sidhani kama ana haja ya kuagiza kutoka nje,

Ingekua ni kg nyingi sawa, ila fomula zipo za kutengeneza chakula cha samaki but it is a challenge kama unafuga samaki wengi, Ila kama ni hao wa kwake (from the way it looked) ni rahisi kuwatengenezea chakula chao hapa hapa.
 
Hii pomd size yake ni ndogo na anaweza tengeneza chakula mwenyewem naweka material ya Kenya na ya Tanzania na maelezo kidogo ya formula ya chakula apate pa kuanzia
You can increase the productivity of your pond and speed up the growth
of your fish by providing them with supplemental food, i.e., prepared
feeds they can consume in addition to the natural foods they find in the
pond. This is one way of intensifying your fish production system. Refer to
Section 4.8 if you are interested in other ways of intensifying production.
Feeds for fish
Manufactured fish feeds are not widely or readily available in East
Africa. Exceptions exist where larger commercial operations such as
TamTrout produce their own feeds for their own fish and may have
excess quantities available for sale. Where manufactured feeds are
available, they might be found in one or more of the following forms:
• Meal
• Crumble
• Dry sinking pellets
• Moist sinking pellet
• Floating pellet
Several different diet formulations have been tested at Sagana
Aquaculture Centre, with the most effective formulation having the
following composition:
Cottonseed cake 37%
Wheat bran 57%
Freshwater shrimp (Caradina spp.) 6%
Vitamin mix minimal
Some farmers are successfully
using feeds they have mixed for
themselves. Examples of mixes that
are easily prepared and economical
to use include:
• Mixture of 76% rice bran and
24% fish meal
• Mixture of dried freshwater
shrimp (Caradina spp.) and
maize bran, sometimes with
some omena meal added
238881245001835271

Kwa kilo kumi sidhani kama ana haja ya kuagiza kutoka nje,

Ingekua ni kg nyingi sawa, ila fomula zipo za kutengeneza chakula cha samaki but it is a challenge kama unafuga samaki wengi, Ila kama ni hao wa kwake (from the way it looked) ni rahisi kuwatengenezea chakula chao hapa hapa.
 

Attachments

guys this thing is very serious!!
unajua kuna siri moja kubwa ya matatizo ya tanzania nayo ni ujinga.
ujinga wenyewe unatokana na ubinafsi,kutokuwa makini, na kutokuona mbali.
unajua nchi za ulaya,marekani zinaendelea sio kwasababu wananchi au raia wote wanahusika bali kuna watu wachache wenye akili sana wamewekwa zile sehemu nyeti zote na ndio hao wanafanya decition making and all the planning.

lakini ukija sisi watanzania zile sehemu nyeti zote watu wamewakana pale kwa kujuana,urafiki,undugu..nk
KUANZIA BENKI KUU,TRA,WIZARA ZOTE MUHIMU,UBALOZINI,KWENYE MABENKI,TANESCO,BANDARI etc utaona wengi wanaofanya kazi huko waliwekwa tu, kwasababu walipigiwa cross na jamaa zao au ndugu zao.

sasa matokeo yake nini.
tuna vijana wengi wenye uwezo mkubwa kiakili lakini matokeo yake vijana hawa wanaajiriwa na makampuni binasfi au wengine wanatokomea ulaya na marekani na wanaishia huko.
huku nje wapo watanzania ambao wanafanya mambo makubwa kwenye sekta mbalimbali lakini serikali yetu inashindwa kuwathamini watu kama hawa na matokeo yake ndio haya tunayoyapata.

Kaka upatikani...
 
Back
Top Bottom