Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Huo upendo unatia mashaka, sio wa kibinadamu wa kawaida.

It’s way too good to be true!
 
Huo upendo unatia mashaka, sio wa kibinadamu wa kawaida.

It’s way too good to be true!
Mkuu nazifaham changamoto za maisha za jamii ya chini nami nipo huko moyo wangu unaniuma Sana unakuta mtu eneo analo linafaa kwa ufugaji lkn hajui chochote.

Nimesaidiwa kujua namimi ni nani nisijitolee
 
Nadhani Kama una Nia ya dhati ya kutusaidia wenzio ungeeleza hapahapa jukwaani kuliko kuitana kwa mawasiliano au PM.

Something bizarre may happen in future [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nadhani Kama una Nia ya dhati ya kutusaidia wenzio ungeeleza hapahapa jukwaani kuliko kuitana kwa mawasiliano au PM.

Something bizarre may happen in future [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo mpango mzuri umekaa kwenye lengo baya
Mimi ninania nzuri tu lkn inawezekana ukafkiria vibaya
Walionipigia nimeongea nao vzr tu na wamenielewa vzr Sana
Sjadai pesa ni hiki nilichonacho na wengine wapate

Lkn pia nashkuru kwa ushauri wako nikimaliza project zangu za strawberry nitakuja kufundisha hapahapa

Barikiwa sana
 
Habarini ndugu zangu Kama heading inavyosomeka hapo juu

Mimi ni kijana wa kiume nimeamua kujitolea kwa yeyote anaetaka kufuga samaki iwe ni kibiashara au kwaajili ya matumizi ya nyumbani anicheki nitamsaidia bure kumshauri au hata kufika eneo analotaka kufugia kwa gharama zake

Nitamsaidia na kumshauri mambo yote yanayohusika na ufugaji kuanzia mwanzo mpaka mwisho .

Lengo-
Ujuzi huu Mimi niliupata mbeya tena bure kwa ufadhili wa serikali yetu ili kuinua uchumi wa wanainchi kupitia ufugaji samaki

Baada ya mafunzo hayo pia nilifanya kazi hio kwa miaka 4 nikapata uzoefu wa kutosha
Baada ya kuondoka mbeya tukapewa darasa la uzalendo na kuinuana

Muda wote sikuwahi kulipa chochote kila kitu nilipata bure

Kwahio Kama unataka au unatamani kufuga samaki na huna uelewa juu ya biashara hio nichek
Nimepewa bure na mimi natoa sadaka kwa wahitaji ili niwe huru kwenye nafsi yangu

0714839251
KaribunH
Bingwa naomba ushauri juu ya chakula kipi bora kwa ukuaji wa kambale....
 
Ntakutumia formula ya chakula mkuu
Mkuu ninaomba unisaidie maarifa kuhusu maswali machache.

1. Unapochimba bwawa, hususan eneo ambalo ni tambarare (bwawa la kujengea zege), vigezo gani hutumika kuchagua upande upi wa bwawa uwe deep na upi uwe shallow? mfano, issue ya direction of sunlight inahusika?

2. Nikifuga sato inatakiwa mita moja niweke samaki wangapi (nikitumia extensive, semi-intensive na intensive system)

3. Kati ya intensive, semi-intensive na extensive methods, ipi ina tija kwa mkulima?
 
Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

Uvuvi%2Bbusega%2B4.jpg










*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments
Mkuu naomba ku shea document za ufugaji wa samaki.Asante
 
Back
Top Bottom