....Mkuu, haya maneno naomba mkutano uishe kwanza salama ndio uyaseme. ameishasema mchangiaji mmoja hapa, hawakawii hawa kukata umeme na kudai kuwa kuna waya umetafunwa na mamba Kihansi
Aisee!! wampe glucose au Padri Slaa amtoe mapepo mabaya Alhaj Mohammed Nyange ( Bob Makani ) Pole sana kamanda wa udongo get well soon.... I hope "umefunguiia"
Niko hapa uwanjani.TBC wanadai kuwa mitambo imekorofisha hivyo tuvute subira.Kwa sasa wanamuziki wetu ndio wanatumbiza tukisubiri mitambo iwe sawa.Muda wetu kuongezwa.Namaamini mambo yatakwenda vizuri.
Mkoloni na kundi lake ndio wako stejini sana.
Hakuna kulala mpaka kileweke.
Poleni sana.
Mbona majina yamelalia upande mmoja wa dini tena ya kikristo, na ukichanganya na mgombea Padri sina imani na Chadema
Huu ni udikteta wa hali juu, CCM oneni aibu Mrudieni Mungu, La sivyo Kikwete utalaanika vibaya sana! acha kuibia raia wema, acha kuua raia wema, kikwete ona aibu!
Regia nakupigia kwenye Zain inaita tu.
Tafadhali pokea na uniunganishe Live nipate kutuma updates wana JF wapate haki yao
Kaka, hujasoma vizuri... Halima Mdee (Muislam), Anna Maulidah Komu (Muislam), Alhaji (Muislam), lakini haya ni baadhi tu ya majina... Usituletee porojo zako! Kama CHADEMA ni chama cha Wakristo, mbona wameanza kampeni na dua ya Kiislam, iliyosomwa na Hassan Yahaya Hussein?
Ongea POINT! Usilete mzaha!
CHADEMA INAKUBALIKA kwa Waislam na Wakristo! Inakubalika, na Watanzania walio wengi. Kama wewe ni mwanachama wa Chama Cha Mafisadi (CCM), hilo ni shauli lako!