Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Marks mana utatujuza manake naona Ikulu watakuwa wamepiga simu TBC matangazo yakatwe kisingizio mitambo inakorofisha.
Watake wasitake ujumbe wa DR Slaa utafika kwa watz wote by anymeans.
One day yes,wamekata wakati Marando anashusha nyundo za haja.
Roho inaniuma sitaweza msikiliza Dr Slaa.
Huwezi amini sasa TBC wanapiga mziki khaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hivi Chadema hawakufahamu kuwa TBC wangefanya uhuni wa aina hiyo?Kwanini hawakununua air time ITV au Channel Ten,and then kama tv stations hizo zingefanya uhuni wa kukatama matangazo zingekuwa sued for breach of contract?
 
Lakini ni haki kwa luninga ya taifa inayolipiwa kodi kukatisha matangazo ya chadema? wadau mnaoelewa hebu tuelezeni
 
Hivi Chadema hawakufahamu kuwa TBC wangefanya uhuni wa aina hiyo?Kwanini hawakununua air time ITV au Channel Ten,and then kama tv stations hizo zingefanya uhuni wa kukatama matangazo zingekuwa sued for breach of contract?
Kwa maelezo niliyopata toka kwa jamaa wa juu ndani ya CHADEMA ni kuwa walienda kununua muda ITV wakazungushwa na vilevile Channel 10.

Ni bora TBC1 kuliko huko kwingine, sidhani kama kukataa kumwonyesha Mpinzani ni jambo jema... Inasikitisha
 
Unajua sikuwa namtazama Jane Shirima? Jana kwenye kipindi cha TUAMBIE alikuwa anawaburuza watazamani waliokuwa wakipiga simu, alikuwa anawakatisha akidai kwamba kuna simu nyingi! WAPI! Huyu anatafuta maslahi CCM, anajua kwamba akiishabikia CCM atakuja kuula baadaye, anajipendekeza. Tatizo ni kwamba, upo uwezekano wa CCM kutokurejea madarakani. Kampeni ya CHADEMA ni KALI, ni mwiba kwa CCM.

Tundu Lissu ameuonesha Mkataba wa Bulyankhulu kwenye umma wa Watanzania, na kumwuliza Jakaya aseme ni lini atawaomba radhi Watanzania kwa kusaini mkataba uliosababisha Watanzania wafe kule Bulyankhulu, na lini atamwomba yeye (Tundu Lissu) radhi kwa kusababisha akamatwe kwa jambo lile lile ambalo Jakaya alisema ni uchochezi, huku leo anasema atawalipa fidia wakazi wa Bulyankhulu?!

Hatudanganyiki na hivyo vipindi vyenu vya muziki, na upuuzi mwingine! CHADEMA wamewasha moto, ambao hautazimika mpaka Oktoba 31, 2010!

-> Mwana wa Haki

Amandla! Awetu! Amandla! Maatla! People's Power! Power to All the People!
 
Mtu mzima taulo ilikua magotini, wameogopa kwamba baada ya mkutano wa leo wangetembea uchi...
 
King ebu nyosha maelezo u mean mpaka apo Jangwani hamna mawasiliano,wamekata umeme.
Ebu fafanua pls.
CCM mwaka huu imekula kwao.
Amenifurahisha Marando kuwa vyombo vya habari kesho wasije sema Makani ameanguka kam Kikwete,wajue fika Makani ana 80 something na JK is only 57 so ni kama first born wake
 
Duh! Hivi hizi Jumuiya Nafiki za Kimataifa zinaona kweli hili? Halafu mwisho wa siku watasema Uchaguzi ulikuwa wa Huru! Fairness iko wapi jamani? hivi jana kwenye CUF nako walizima?
 
Kwa maelezo niliyopata toka kwa jamaa wa juu ndani ya CHADEMA ni kuwa walienda kununua muda ITV wakazungushwa na vilevile Channel 10.

Ni bora TBC1 kuliko huko kwingine, sidhani kama kukataa kumwonyesha Mpinzani ni jambo jema... Inasikitisha


Mkuu Invisible, I wish tungemuandaa mtu wetu wa JF awepo pale Uwanjani.

Jamaa wamewanyima haki yao ya katiba Watanzania

Watawala Bwana . . . wanataka vitu laini laini tu na kusifiwa
 
Mkuu Invisible, I wish tungemuandaa mtu wetu wa JF awepo pale Uwanjani.

Jamaa wamewanyima haki yao ya katiba Watanzania

Watawala Bwana . . . wanataka vitu laini laini tu na kusifiwa
Hujakosa, mpigie Regia... Akuweke hewani; uzuri ni 1shs per sec.

I tried to call you but seems you're away from your mobile
 
Hivi tukitangaza KUSUSIA matangazo ya TBC1 na ITV, itakuwaje? Tunaweza?
 
Anasema Lissu amemtuma aweke Pingamizi Jumatatu

Sheria hairuhusu Kuhonga

Kawaambia wana Kagera atawaletea Meli Mpya . . Hongo hiyo

Kuongeza Mishahara . . . Hongo . . .

Tendwa ana wajibu wa Kumsimamisha Jk asigombee


Aisee hawa jamaa wamejipanga

Nimeona ile picha kwa Michuzi JK yupo na Mama mlemavu amemuahidi kuwa atamnunulia baiskeli, hivi hiyo sio rushwa ya Uchaguzi? why ahadi kama hiyo wakati wa kampeini?
 

Attachments

  • 8E9U8550.jpg
    8E9U8550.jpg
    102.6 KB · Views: 36
Ha kumbe Bob kaanguka jukwaani

Aisee!! wampe glucose au Padri Slaa amtoe mapepo mabaya Alhaj Mohammed Nyange ( Bob Makani ) Pole sana kamanda wa udongo get well soon.... I hope "umefunguiia"
 
Xuma, nilikuwa sijaona topic yako kabla ya kuanzisha ya kwangu.

Huu ni upuuzi na ufisadi mkubwa sana. Wamezoea sana hawa TBC.

Cha kushangaza ni hayo matangazo waliyoyaweka, hivi kuna mtanzania anakata kusikiliza hiyo miziki kwa sasa wakati kuna kitu mhimu kuhusu mustakabali wa taifa lao?
Hata kama ni ukibaraka inabidi waangalie namna ya kufanya hayo madudu Yao!
 
Niko hapa uwanjani.TBC wanadai kuwa mitambo imekorofisha hivyo tuvute subira.Kwa sasa wanamuziki wetu ndio wanatumbiza tukisubiri mitambo iwe sawa.Muda wetu kuongezwa.Namaamini mambo yatakwenda vizuri.

Mkoloni na kundi lake ndio wako stejini sana.

Hakuna kulala mpaka kileweke.
Poleni sana.
 
kuna haya ya kubadilisha title ya hii thread ... isomeke kuwa TBC watangaza na kukata matangazo ya chadema
 
Hujakosa, mpigie Regia... Akuweke hewani; uzuri ni 1shs per sec.

I tried to call you but seems you're away from your mobile

Mkuu nipe namba ya Regia ya Zain. Nitumie kwenye Zain yangu na Mwambia nampigia aniconnect Live ili niendelee kutuma updates.

Ingawa huku kwangu Kijijini Network ya shida nitajitahidi
 
Back
Top Bottom