Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Walikatiza kwa sababu ya mabomu ya Marando, sasa wamerejesha. Uhuni mtupu!
 
Kamanda Mbowe ndio anakanyaga twende.TBC wako hewani sasa.Muda wetu kuwa pale pale masaa matatu.
 
Duh ngoja tuone hawa jamaa maana naona wanakoroga kwa makusudi!! waambieni kabisa tutashusha guruneti hapo K/nyama limalize kazi ndani ya dakika moja. Yapo makombora kibao hayajafanyiwa testing siku kibao.
 
Pambaf sana, Bravo wananchi wenye hasira nadhani TBC wameamua kurejesha ili kuwanusuru mafundi mitambo wao. Nyambaf
 
Mbowe anawaomba wa TZ Watulie. Waandishi wa TBC wanafanya kazi nzuri. Si kosa lao ni la viongozi wao.

Ni haki yetu Kusikilizwa ndani na nje ya Nchi.

Wenzetu kwa sababyu ya woga walitoa matangazo yakatizwe

Watanzania tulieni

Tuende kwenye hoja za msingi

CCM tayari wana Kiwewe
 
TBCCM wameona haya wameturudisha hewani,Mbowe amesema watu waligoma uwanajani na kuanza kuleta fujo.
Huu mwamko unatakiwa.
Mbowe anasema kuwa kwa kukatiza matangazo ni kiwewe
 
Walikatiza kwa sababu ya mabomu ya Marando, sasa wamerejesha. Uhuni mtupu!

Wameadai kwamba mitambo iliharibika kidogo.Pamoja na hayo ujumbe umefika na tukio hili linarekodiwa tutasambaza nchi nzima.Na magazeti yataandika tu.

Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Niko hapa uwanjani.TBC wanadai kuwa mitambo imekorofisha hivyo tuvute subira.Kwa sasa wanamuziki wetu ndio wanatumbiza tukisubiri mitambo iwe sawa.Muda wetu kuongezwa.Namaamini mambo yatakwenda vizuri.

Mkoloni na kundi lake ndio wako stejini sana.

Hakuna kulala mpaka kileweke.
Poleni sana.


Mkuu TBCI wanadanganya hao....wanasahau kuwa wanaishi kwa kodi zetu...ingekuwa mitambo imeharibika wangeomba radhi....lakini kwa waliokuwa wanaangalia live mmeona hawajaomba radhi kama ilivyo kawaida ya maadili ya uandishi......wamezima tv makusudi kuwakomoa CHADEMA kwa maagizo maaulum ya IKULU!!!...Hii ni moja ya mifano hai ya uvunjaji wa haki...za mpiga kura..
 
CCM Hizi ni Rasha rasha
Shughuli bado
Waandishi tulieni
Wanachadema tuwaonyeshe amani
Tunawaonya TBC wasirudie
Nguvu ya Umma itawashughulikie
 
Kumekucha! TBC wanaonywa, nguvu ya umma ikiamua kuwashughulikia hakuna jeshi litakaloweza kuwasimamisha. Anawaambia Watanzania damu ya Mtanzania isimwagike kwa ajili ya Dk Slaa kwenda Ikulu. Vijana wa TBC wasiumizwe. Damu isimwagie kwa ajili ya kwenda Ikulu. Busara hizo! Wamefanyiwa uhuni lakini wao wanadai AMANI!

CCM wangeweza hayo?
 
Kaka, hujasoma vizuri... Halima Mdee (Muislam), Anna Maulidah Komu (Muislam), Alhaji (Muislam), lakini haya ni baadhi tu ya majina... Usituletee porojo zako! Kama CHADEMA ni chama cha Wakristo, mbona wameanza kampeni na dua ya Kiislam, iliyosomwa na Hassan Yahaya Hussein?

Ongea POINT! Usilete mzaha!

CHADEMA INAKUBALIKA kwa Waislam na Wakristo! Inakubalika, na Watanzania walio wengi. Kama wewe ni mwanachama wa Chama Cha Mafisadi (CCM), hilo ni shauli lako!

Hujui ulisemalo! nani kakuambia Halima Mdee Muislamu? kasilimu lini? kwa taarifa yako ni msabato tena msabato masalia! Na huyu Anna Komu nae kasilimu lini? mgala na nguruwe anakula!

Get your facts right kabla kapayuka ovyo.
 
Mkuu madege ya jeshi hauyafahumu,si second hand yale yana mikelele kama yale magari ya mashindano.
Likipita pale jangwani wote mnapatwa na matatizo ya masikio
 
Hatutaki kwenda Ikulu kwa kumwaga Damu.

Tumekuja kusikiliza na Watanzania na taifa
Wako wanachama wa kila chama na wasio na chama
Msiwaguse TBC
wala msiwaguse wengine maana tunahitaji kura zao 31st october siku ya Kumpeleka Slaa Ikulu
 
Kuna fununu zozote zilizopo kwa nini TBC walikata matangazo ya live...

Kaka, ilipigwa simu TBC1 pale ambapo Marando alipoanza kumtaja JK kuhusika na EPA... matangazo yakakatwa! Hiyo ndiyo sababu! Unataka nyingine?
 
Walikatiza kwa sababu ya mabomu ya Marando, sasa wamerejesha. Uhuni mtupu!

Ili ku-prove siyo mabomu ya Marando yaliyopelekea kukatika matangazo, Marando aongelee kitu hicho hicho leo (kama kuna muda wa kutosha) au siku nyingine TBC watakapokuwa wanaonesha matangazo live.
 
Miaka 50 ya bakora ya CCM iwe ya kutujenga kufanya maamuzi ya kupiga kura
WaTZ kazi ya Ukombozi si nyepesi na si ya Chadema pekee yake
Chadema tumekubali kuwa jukwaa, jahazi, kuunganisha fikra za watanzania wote
 
Back
Top Bottom