Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Kama nilichosema ni uongo,leta ukweli unaoujua wewe.
A) Tuambie MTU wa kwanza ni Nani?
B). Tuambie ni kwa Nini tunatofautiana rangi sisi wanadamu?
C) Huyo MTU wa kwanza alikuwaje na alikuwa na rangi gani?
D) Eleza pia Cain alivyokimbilia nchi ya Nodi aliwakuta kina Nani?

NOTE.
Hakikisha unaleta reference ili kuthibitisha maelezo yako. Hizo reference ziwe za uhakika.
Utakuwa umetusaidia wengi kuujua ukweli.
Duuuu mkuu mbona umekuwa muongo kiasi hiki?

Sent using LEAGOO M12
 
Hebu soma hapa.. Refer kule pm Sanaa ya kifo - JamiiForums

Jr[emoji769]
 

Ujinga sio tusi, hivyo lisikuumize sana hilo neno. Of course wewe ni mjinga, tena mjinga kikwelikweli, yan.mjinga hasaaa. Na si mjinga tu bali pia wewe ni kipofu ingawa macho yako ni mazima. Ushahid unaouhitaj ulishapewa, toa wako.

We jamaa mjinga wa fly-over, unadai wengi wanakujibu KINADHARIA tu, sasa unapotaka ushahidi kutoka ktk Quran na Bible, Je unatarajia kupata ushahidi wa aina gani kama si wa KINADHARIA? Au nadharia hujui maana yake? Hii ndio imani, unaamini usichokiona lakin unaamini maandiko ya yule aliyeumba mbingu na ardhi (MWENYEZI MUNGU) ambaye anajua mwanzo wake mpaka mwisho wake. Ingekuwa watu wana kujibu KIDHANA (yan kwa kutumia mawazo yao tu bila ushahidi wowote) hapo sawa. Na kama ungekuwa na mapepo ungepata ushahidi wa kivitendo zaidi ulioambatana na imani badala ya NADHARIA pekee kutoka kwa viongozi wa dini kuondoa mapepo uliyo nayo. Lakin ktk hili ushahid wake haupo mwingine zaid ya huo wa kinadharia ambapo wale wenye akili, wanaotafakari huamini lakin wale walio kufuru ni kama wanyama wa kufugwa pindi wanapoitwa au kuelekezwa waelekee ktk usawa, utawaona wanakutazama kama vile wanakuelewa kumbe hawasikii ila wito na sauti tu. Ni viziwi, vipofu hivyo hawana akili. Na hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye wala hawaamini. Kama NADHARIA, MTU na NABII umeshindwa kuyatumia maneno hayo ktk usahihi wa matumizi, sipati picha tunachokiandika hapa unakielewa vipi. Na hapa nahisi ndo kuna tatizo ndio mana unatusumbua sana kwa7bu hata tukueleze vipi huwez kuelewa. Matumiz ya lugha yenyewe yanakupiga chenga, hayo maandiko utaelewa kweli. Ndio maana nikasema kaa usome kwanza, sio kukurupuka tuuuu.

Biblia: Mwanzo 5:1-2, Mwanzo 1:27, Mwanzo 2:7 na 1Wakorintho 15:45 inamaliza kazi

Quran: Surah Al Baqara 2:30-36 inaelezea wazi waliokuwepo kabla ya Adamu kuumbwa ni akina nani, kisha kuumbwa kwa Adamu, namna Adamu alivyofundishwa na Mola wake majina ya vitu kama vile wanyama ambayo malaika waliulizwa wayataje lakin wakashindwa, kisha inaelezea pia namna ibilisi alivyoasi amri ya Mola wake na namna alivyowashawishi Adamu na mkewe kula tunda walilokatazwa.


Kaa chini usome wewe, sio ukurupuke. Ushahid unapewa lakin matamanio ya nafsi yako yanakudanganysna au wewe ni kipofu au hujui kusoma?

Pitia hivyo vifungu, vinaeleza wazi kabisa na vimemtaja Adamu kwa.jina lake kabisaaaaaaa. Unataka ushahid upi sasa?
 
Naomba ninukuu aya ambazo wewe umezitaja kisha utaniambia wapi ametajwa Adamu kuwa ndio mtu wa kwanza
Sura 2:30-36
Aya ya 30: Na kumbuka mola wako alipowaambia malaika:Hakika mimi nataka kumteua khalifa katika ardhi,wakasema:je utamweka humu atakayefanya uharibifu humona kumwaga damu,hali sisi twakutukuza kwa sifa zako na kukutaja utakatifu wako?Akasema:Hakika mimi nayajua msiyoyaju

Aya 31 Na akamfundisha Adamu majina yote kisha akawaweka viumbe wale mbele ya malaika na akasema,niambieni majina ya hawa ikiwa mwasema kweli

Aya,32. Wakasema utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ulivyotufundisha,bila shaka wewe ndiwe mjuzi mwenye hakima

Aya,33. Akasema ewe Adamu,waambie majina yao,basi alipowaambia majina yao,Akasema,je sikuwaambieni kwamba mimi naijua siri ya mbinguni na ya aridhi na nayajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha

Aya 34. Na(kumbukeni) Tulipowaambia malaika,mtiini Adamu,na wakatii wote isipokuwa Ibilisi alikataa na akafanya kiburi,naye alikuwa ni miongoni mwa makafiri

Aya 35. Na tulisema Ewe Adamu,kaa wewe na mkeo katika bustani,na kuleni humo kwa maridhawa popote mpendapo,lakini msiukaribie mti huu waila mtakuwa miongoni mwa wadhalimu

Aya 36. Basi shetani akawatelezesha humo wote wawili katika suala la mti ule na akawatoa mle walimokuwemo hapo awali,Ndipo tukawaambia tokeni mmaadui ninyi kwa ninyi na (imekadiriwa kuwa)mtakaa na kunufaika katika ardhi hii hadi muda fulani

Hizo ni aya ambazo zinapatika ktka sura ya 2:30-36 ambazo wewe umezinukuu
Swali nitajie aya kati ya hizo ambayo inasema Adamu ni mtu wa kwanza
 

Aya 30: Mazungumzo yanafanyika baina ya Mwenyezi Mungu na Malaika, ktk mazungumzo hayo amezungumziwa KHALIFA ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumteua. Je Khalifa maana yake ni ipi? Na nini makusudio ya neno Khalifa? Wakat Mwenyezi Mungu anafanya hayo mazungumzo na Malaika, Je, Adamu alikuwa wapi na huyo Khalifa anayezungumziwa hapo ni yupi?


Aya 31: Anatajwa Adamu awatajie majina ya viumbe malaika. Kwanini afundishwe Adamu pekee asiwe mtu mwingine tofauti na Adamu? Hao watu wengine waliotangulia kabla ya Adamu wako wapi? Na amewataja wapi? Au kwanini hakuwataja kama wapo kabla yake Adamu? Kama.unatafuta ushahid wa senetensi ya moja kwa moja kama utakavyo ili kuonesha kuwa Adamu ndio mtu wa kwanza, kwanini hujanukuu 1Wakorintho 15:45?

Na kama sentensi ya moja kwa moja inayoonesha kuwa kuna watu walikuwepo kabla ya Adamu haipo ktk biblia wala Quran, Je ndo itasemwa kuwa watu walitokana na nyani? Kama walitokana na nyani, kwanini nyani mpaka saiv bado wapo na wasibadilike wote kuwa binadamu? Ilikuaje wengine walibadilika na wengine hawakubadilika? Na kwanini miili na rangi zetu zinatofautiana na hao nyani?

Jua na sayari zingine vimetoka wapi? Na kama viliumbwa na Mungu, wapi imeandikwa kuwa Mungu aliumba jua, dunia na sayari zingine? Andiko likikosekana ndo itasemwa hakuna aliyeumba vitu hivyo? Kama havikuumbwa vimetoka wapi? Mungu haonekani kwa macho, je kutokuonekana kwake ndo itasemwa hayupo? Na kama yupo ushahidi wako ni upi? Akili haionekani lakin uwepo wake unafahamika kupitia matendo ya mtu. Ukiambiwa toa ushahid kuonesha una akili utaonesha nini kama ushahid?
 
JIBU: Biblia imetupa majibu kama ifuatavyo..

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Huo ni mstari wa kwanza kabisa unaozungumzia uumbaji wa mwanadamu katika biblia, hakuna mstari mwingine kabla ya huu.. Na unasema Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. (maneno hayo mawili yapo katika umoja.). Na haijasema Mungu alimwumba Mwanaume na wanawake.. wala haijasema Mungu alimuumba mwanamke na wanaume.

Kwahiyo hakukuwa na mwanaume Zaidi ya Adamu, na wala hakukuwa na mwanamke mwingine Zaidi ya Hawa katika uumbaji.

Jambo linalowachanganya wengi ambalo ndilo limezua swali hili, ni kuhusu mke wa Kaini, kwamba Kaini alitolea wapi mke?

Kwanza kabisa Ni muhimu kufahamu kuwa Adamu na Hawa, walizaa Watoto wengine wengi wakike na wa kiume baada ya Habili na Kaini. Watoto wa Adamu hawakuwa wawili tu, bali wengi.

Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.

Kwahiyo miongoni mwa hao Watoto wa kike aliowazaa Adamu, mmojawao ndio alikuwa mke wa Kaini, na Kaini na mkewe walizaa Watoto, na watoto wao walizaa Watoto, na wajukuu zao pia walizaa..Na wakati huo watu walikuwa na uwezo wa kuishi mamia ya miaka.

Kwahiyo ni uongo kusema kuwa Adamu alikuwa na mke mwingine tofauti na Hawa.
 
Ahahhahah ahahahahahah hii ndio kwanza naisikia kwako hakuna hata sehem nimewahi kusikia wala kusoma habari ya huyo lilith ..lakini maneno ya kuambiwa changanya na akili zako
 
Yaani kuna mengi sana tusiyoyajua ila tupeane jamani ili tuzidi kuongeza maarifa ila Mungu pengine aliyaficha mengine ili tu tuwe salama
 
Ahahhahah ahahahahahah hii ndio kwanza naisikia kwako hakuna hata sehem nimewahi kusikia wala kusoma habari ya huyo lilith ..lakini maneno ya kuambiwa changanya na akili zako
Je umeshasoma maarifa yote kuhusu Biblia zote ukakuta hakuna?
 
hata Adam na Eva hawakuumbwa na utashi na akili, walipata utashi baada tu ya kula tunda ndipo wakaweza kujua Jema na baya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…