Ndo umekasirika mkuu?Majibu umepewa. Nmeyaona yapo sawa pamoja na tafsiri zake kuwa na changamoto, ndo maana nikatoa maoni.
Anyways, upo sawa Adam hakuwa mtu wa kwanza na waliokujibu hawajui. Ww unafahamu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo umekasirika mkuu?Majibu umepewa. Nmeyaona yapo sawa pamoja na tafsiri zake kuwa na changamoto, ndo maana nikatoa maoni.
Anyways, upo sawa Adam hakuwa mtu wa kwanza na waliokujibu hawajui. Ww unafahamu.
Duuuu mkuu mbona umekuwa muongo kiasi hiki?
Sanaa ya kifo - JamiiForumsKWA mujibu wa Kitabu cha ZUGRIL GALAYO (Nguvu Iliyodunu Katika Jadi)
Mtu wa Kwanza Alitambulika kwa Majina yaliyotokana na mazingira na jambo lililomuhusu katika kuishi kwake.
1. FUMBA KASA - lilipatikana ktk kipindi cha kukusanywa kwake.
2. SABKORODAMS - lilipatikan alivyoanza kula
3. MID ERA - Alivyoanza kuvaa nguo (kujisitiri)
4. MUNDU - Alivyoanza kuwa na Lugha
5. ZUNDRAGA - Alivyoanza kufanya matembezi
6.MASON KWATA - Alivyopata jinsia ya pili iliyotokana na yeye
7. ABE EI - alipoanza kuzaa na kulea
8. ESTONE - Alipoanza ujenzi wa vitu
GOWESHAN - Alipanza kuweka hifadhi kwa ajili ya familia yake
9. MTALAY - wakati anaacha wosia kwa watoo wake.
ALIUMBWAJE SASA!!?
Mtu huyu aliumbwa kwa mkusanyiko wa vumbi kutoka mabara saba lillokusanyika katika eneo la SHANKOMBOLUZU Ambalo leo hi linatambulika kama URUSI.
Aliumbwa akiwa na urefu wa Km Nne (4) upana wa kifua Mita mia tatu akiwa na rangi nyeusi na mwenye asili ya Nywele Ngumu zisimamazo kwa umbile lake.
NAWAOMBENI MKITAFUTE HIKI KITABU SANA SANA SANA MAANA NDANI YAKE KINAMUELEEZEA HADI ADAM ALIVYOKUJA KUPATIKANA NA HAKIMUELEEZEI KAMA ALIKUA MTU WA KWANZA KUUMBWA.
Nilibahatika kukipata na kwa kuwa sikuwa na muda wakuweza kutulia na kukisoma kutokana na uharaka wa aliyekuwa nacho, nilimuomba japo nikinakili ingawa pia sikuweza kukimaliza chote kukichapa kwa uharaka wa mwenye nacho.
Kina mengi mengi yakuyatafakari, na ni kitabu cha asili ya Muafrika na kina hadi namba na herufi za kibantu achana na hizi alfabeti tuzijuazo, humo ndio namba zinaandikwa mosi mpaka kenda nk, namna makabila na nchi mbalimbali duniani zilivyoanza....
nilijaribu kushare na watu wengi hawakua wakikifaham nikaona nisije kuonekana mimi ndio mtunzi ila nilipomsikia Mwanamuziki akijiita Ibrozama nikajua ni kitabu kijulikancho kwa wengine maana jina hilo linapatikana ndani ya kitabu hiko na lina historia yake.
sipo vizuri kukieleezea sana ila nitapenda kukishare na Mshana Jr, then atatusaidia kama kina lolote la kujifunza au kukipuuza japo kina typing error kidogo kutokana na kukichapa mwenyewe na mpaka sasa sijapata muda wakutulia kukiedit coz hard copy yake bado naendelea kuhangaika niipate tena.
Mshana Jr ukiridhia nitakutumia PM!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana.Ndo umekasirika mkuu?
Mkuu pamoja na kwamba unaniita mjinga lakini hakuna hata mmoja ambaye amejibu maswali yangu.wengi mnanijibu kinadharia nipo tayari kukubaliana nanyi kuwa Adam ndio mtu wa kwanza kama utafanya yafuatayo
1. Kupitia Quran uje na aya iliyomtaja Adam kuwa ndio mtu wa kwanza moja kwa moja.
2.kupitia bible uje na aya inayomtaja adam moja kwa moja kuwa adam ndio mtu wa kwanza kuumbwa
Naomba ninukuu aya ambazo wewe umezitaja kisha utaniambia wapi ametajwa Adamu kuwa ndio mtu wa kwanzaUjinga sio tusi, hivyo lisikuumize sana hilo neno. Of course wewe ni mjinga, tena mjinga kikwelikweli, yan.mjinga hasaaa. Na si mjinga tu bali pia wewe ni kipofu ingawa macho yako ni mazima. Ushahid unaouhitaj ulishapewa, toa wako.
We jamaa mjinga wa fly-over, unadai wengi wanakujibu KINADHARIA tu, sasa unapotaka ushahidi kutoka ktk Quran na Bible, Je unatarajia kupata ushahidi wa aina gani kama si wa KINADHARIA? Au nadharia hujui maana yake? Hii ndio imani, unaamini usichokiona lakin unaamini maandiko ya yule aliyeumba mbingu na ardhi (MWENYEZI MUNGU) ambaye anajua mwanzo wake mpaka mwisho wake. Ingekuwa watu wana kujibu KIDHANA (yan kwa kutumia mawazo yao tu bila ushahidi wowote) hapo sawa. Na kama ungekuwa na mapepo ungepata ushahidi wa kivitendo zaidi ulioambatana na imani badala ya NADHARIA pekee kutoka kwa viongozi wa dini kuondoa mapepo uliyo nayo. Lakin ktk hili ushahid wake haupo mwingine zaid ya huo wa kinadharia ambapo wale wenye akili, wanaotafakari huamini lakin wale walio kufuru ni kama wanyama wa kufugwa pindi wanapoitwa au kuelekezwa waelekee ktk usawa, utawaona wanakutazama kama vile wanakuelewa kumbe hawasikii ila wito na sauti tu. Ni viziwi, vipofu hivyo hawana akili. Na hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye wala hawaamini. Kama NADHARIA, MTU na NABII umeshindwa kuyatumia maneno hayo ktk usahihi wa matumizi, sipati picha tunachokiandika hapa unakielewa vipi. Na hapa nahisi ndo kuna tatizo ndio mana unatusumbua sana kwa7bu hata tukueleze vipi huwez kuelewa. Matumiz ya lugha yenyewe yanakupiga chenga, hayo maandiko utaelewa kweli. Ndio maana nikasema kaa usome kwanza, sio kukurupuka tuuuu.
Biblia: Mwanzo 5:1-2, Mwanzo 1:27, Mwanzo 2:7 na 1Wakorintho 15:45 inamaliza kazi
Quran: Surah Al Baqara 2:30-36 inaelezea wazi waliokuwepo kabla ya Adamu kuumbwa ni akina nani, kisha kuumbwa kwa Adamu, namna Adamu alivyofundishwa na Mola wake majina ya vitu kama vile wanyama ambayo malaika waliulizwa wayataje lakin wakashindwa, kisha inaelezea pia namna ibilisi alivyoasi amri ya Mola wake na namna alivyowashawishi Adamu na mkewe kula tunda walilokatazwa.
Kaa chini usome wewe, sio ukurupuke. Ushahid unapewa lakin matamanio ya nafsi yako yanakudanganysna au wewe ni kipofu au hujui kusoma?
Pitia hivyo vifungu, vinaeleza wazi kabisa na vimemtaja Adamu kwa.jina lake kabisaaaaaaa. Unataka ushahid upi sasa?
Naomba ninukuu aya ambazo wewe umezitaja kisha utaniambia wapi ametajwa Adamu kuwa ndio mtu wa kwanza
Sura 2:30-36
Aya ya 30: Na kumbuka mola wako alipowaambia malaika:Hakika mimi nataka kumteua khalifa katika ardhi,wakasema:je utamweka humu atakayefanya uharibifu humona kumwaga damu,hali sisi twakutukuza kwa sifa zako na kukutaja utakatifu wako?Akasema:Hakika mimi nayajua msiyoyaju
Aya 31 Na akamfundisha Adamu majina yote kisha akawaweka viumbe wale mbele ya malaika na akasema,niambieni majina ya hawa ikiwa mwasema kweli
Aya,32. Wakasema utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ulivyotufundisha,bila shaka wewe ndiwe mjuzi mwenye hakima
Aya,33. Akasema ewe Adamu,waambie majina yao,basi alipowaambia majina yao,Akasema,je sikuwaambieni kwamba mimi naijua siri ya mbinguni na ya aridhi na nayajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha
Aya 34. Na(kumbukeni) Tulipowaambia malaika,mtiini Adamu,na wakatii wote isipokuwa Ibilisi alikataa na akafanya kiburi,naye alikuwa ni miongoni mwa makafiri
Aya 35. Na tulisema Ewe Adamu,kaa wewe na mkeo katika bustani,na kuleni humo kwa maridhawa popote mpendapo,lakini msiukaribie mti huu waila mtakuwa miongoni mwa wadhalimu
Aya 36. Basi shetani akawatelezesha humo wote wawili katika suala la mti ule na akawatoa mle walimokuwemo hapo awali,Ndipo tukawaambia tokeni mmaadui ninyi kwa ninyi na (imekadiriwa kuwa)mtakaa na kunufaika katika ardhi hii hadi muda fulani
Hizo ni aya ambazo zinapatika ktka sura ya 2:30-36 ambazo wewe umezinukuu
Swali nitajie aya kati ya hizo ambayo inasema Adamu ni mtu wa kwanza
..inasemekana hivyo ndgAcha kudanganywa mate...
Yaani kuna mengi sana tusiyoyajua ila tupeane jamani ili tuzidi kuongeza maarifa ila Mungu pengine aliyaficha mengine ili tu tuwe salamaLilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.
Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.
Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?
Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.
Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.
Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.
Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwa wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.
Ibada za kutoa kafara katika satanism
Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.
Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.
Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.
Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.
Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.
Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?
Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!
Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.
Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.
Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.
Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.
Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!
Je umeshasoma maarifa yote kuhusu Biblia zote ukakuta hakuna?Ahahhahah ahahahahahah hii ndio kwanza naisikia kwako hakuna hata sehem nimewahi kusikia wala kusoma habari ya huyo lilith ..lakini maneno ya kuambiwa changanya na akili zako
hata Adam na Eva hawakuumbwa na utashi na akili, walipata utashi baada tu ya kula tunda ndipo wakaweza kujua Jema na bayaLilith atakua ni shetani lakini hakua mwana wa adam,atakua ni mmoja wa malaika walio hasi kwa molah wao.katika uumbaji alioufanya mungu akuumba kiumbe chochote chenye utashi na akili kama adam,hata hao malaika mwanzo wa biblia haijataja uumbaji wao,lakini wakati mungu anaumba mbingu na ardhi na kila kitu alikua na malaika na ndo maana mungu alipowaambia malaika wamsujudie adam ndo wakaasi na kuitwa ibilis,hata mm naweza kuungana kua ibilisi ni shetani mwanamke,lkn mara nyingi shetan anatambulishwa sana kwa jinsi ya kike zaidi ya mwanaume
Sent using Jamii Forums mobile app