Jikite kwenye hoja, punguza uchawa. Katiba ya JMT ipo outdated, imempa Rais mamlaka ya Ki-Mungu. National Wealth Resources ( Permanent Sovereign) Act ya 2017 ( Revised ) ina-limit baadhi ya resources kuwa controlled na foreign territory. Hii issue ya bandari ipo sensitive sana, ilihitaji ushirikishwaji wa stakeholders wote including the public at large siyo kuwaachia wabunge wa CCM tu watuamlie tena kwa maslahi ya matumbo yao.
Umemuongelea mwendazake ( Magufuli ) kufanya maamuzi ya kujenga JNHP na kuchagua mzabuni wa kujenga SGR kwa utashi wake lakini hakufanya maamuzi ya kubinafisisha rasilimali za nchi kama huyu Bi-Tozo alivyoamua kubinafisisha rasilimali za watanzania kwa maslahi yake binafsi na genge lake. Kwa mfano, wale wamasai kuondolewa kule Loliondo unaona ni sawa? Bandari zote nchini kupewa waarabu ni sawa? Haya yote yamefanyika kwa sababu ya udhaifu wa katiba ya JMT.