mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Kuna uzi Pascal Mayalla kafafanua kabisa kuwa IGA ni Sawa na MoU... memorandum of understanding tu.. makubaliano ya kidiplomasia zaidi ambayo hayana nguvu yeyote ya kisheria Hadi mtakapoingia mkataba halisi....
Umeuliza why hii inapingwa zaidi?
Hujui kuna watu wataathirika na biashara? Karamagi na Ticts?hakawalipa watu "wampambanie"?
Unaamini ni uzalendo wake Tibaijuka anaenda Hadi kwenye TV kupinga Dpworld? Huyu Tibaijuka aliepewa mgao escrow?? Hajapewa mgao na Karamagi??..
Huoni kuna kundi linatumia nguvu kupinga Dpworld Kwa sababu ambazo haziko clear??
Moja, hoja yako ya kuhusisha mkataba wa IGA na Ticts au makosa ya utawala uliopita siyo sahihi ni kama unahamisha nguzo za gori ili mpira uingie gorini.
Pili, IGA siyo MoU labda kama hujausoma au unautetea kwa sababu unazozijua mwenyewe.
Tatu, hujajibu swali langu la msingi Kwa nini DPW haiwekezi nchini kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo kama makampuni mengine ya kibiashara? Kumbuka hata Ticts, unayoshutuma ukimhusisha Prof Tibaijuka, haikuwekeza kwa njia inayotaka kutumiwa na DPW ikitetewa kwa nguvu kubwa na Utawala ulioko madarakani. Kuna nini?
Bila majibu yenye ushahidi usio na mashaka, DPW ikiwekeza kupitia IGA, wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mwakani, nitajitokeza mbele ya wapiga kura, wagombea wa chama tawala, ngazi zote, waeleze kilicho nyuma ya uwekezaji huo.