Katiba ya JMT 1977 ,151 (1) Inatamka '' Tanzania Bara maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika''
Kwa maana tunapoitaja Tanzania, lile eneo la Bara ndiyo ilikuwa Tanganyika. Huyu jamaa anayeitwa Tanganyika sijui alibatizwa au alisilimishwa lakini tunajua ni yule yule aliyeachwa na Mwingereza.
Tanganyika ipo midhali neno Bara lipo. Lakini Wazanzibar hawajiiti Tanzania visiwani tena, hili neno Bara ni Tanganyika. Ukiwa huna visiwani wapi utapata Bara? ni Tanganyika tu
Kwanini ni muhimu katika mjadala. Rais SSH alisaini MoU inayohusu Tanzania ( Zanzibar wakiwemo).
Katika kamati ya Bunge, kwa mujibu wa Mbunge Aida Kenani Wazanzibar walisema Bandari zao hazimo katika MoU. Hoja haijakanushwa na Bunge au Wazanzibar. Sasa kama Zanzibar haipo katika Tanzania tunabaki na Tanzania Bara ambayo ni eneo la iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika. Kwa maneno mengine MoU inahusu Tanganyika.
Kama Rais wa JMT anasaini suala la Tanzania Bara ambayo ni Tanganyika na kuiacha Zanzibar katika jambo la muungano (bandari kwa mujibu wa mkataba) kwa kutumia jina la Tanzania, huoni Tatizo hapo?
Mathalan DP wakitoa Dollar Bilioni 10 kwa Bandari, Zanzibar wanastahili kwasababu DP inatoa kwa Tanzania.
DP hao hao walileta ufanisi mapato ya Bandari ni ya JMT kwasababu yamesimamiwa na Rais wa JMT na kuandikwa kwa jina la JMT na Zanzibar watapewa ruzuku ya bajeti na 4.5% ya pato la bandari. Huoni tatizo hapo? Lakini DP wakitaifisha bandari au kudai malipo hilo litakuwa suala la Tanzania Bara ambayo ni Tanganyika, Zanzibar watatumia katiba yao. Huoni tatizo hapo?
Ni utaratibu ule ule mbovu wa gesi ya Tanganyika, Madini ya Tanganyika, utalii wa Tanganyika n.k. kuingiza pato la Taifa halafu Zanzibar wanapata mgao wa 4.5% kwasababu tu ya neno Tanzania. Lakini ukiwauliza gesi yao ipo wapi wanakwambia si jambo la muungano. Huoni tatizo hapo ? Huoni kwanini Tanganyika inahitajika kuwekwa wazi kwenye mambo mazito kama haya ya Bandari?
Ni utaratibu ule ule wa hovyo, kwamba, tunakopa kama Tanzania halafu wakati wa kulipa tunatumia hazina ya Tanzania Bara yaani Tanganyika. Huoni tatizo hapo?
Kama Tanganyika haipo , Hii Tanzania Bara iliyotajwa katika katiba ni kitu gani na kilianzia wapi?
The Boss JokaKuu Pascal Mayalla