mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
You are missing the point
Kama Magufuli alikosea na hawa kina Mwanakijiji walikuwa kimyaa kabisa hata watu walipokuwa wanapigwa risasi na kutekwa...hawana haki ya kuchonga midomo kisa Rais aliepo sie wanaomtaka....
Wale waliokuwa wanamkosoa Magufuli..sina shida nao kabisa kama wanamkosoa Samia...angalau wao wamesimamia principles... I hope umenielewa
Hoja yako inayohusisha Utawala uliopita na wa sasa ni nje ya mada kabisa.
Nami naungana na aliyekupinga kwa hoja kwamba utawala wa sasa haupaswi kurudia makosa ya uliopita, kufanya hivyo ni dalili za udhaifu. Wahenga walinena Kufanya kosa siyo kosa, kosa ni kurudia kosa.
Hivyo basi, wasiopenda mkataba wa IGA, kama mimi, tunauambia utawala wa sasa, KWA SAUTI KUBWA, watakosea sana kuipa DPW kuendesha bandari kwa mgongo wa nchi yake tofauti na makampuni ya nje yanayowekeza nchini kibiashara. Na ukiusoma huo mkataba (IGA), unaoiteua DPW, kwa umakini, unaipa mamlaka na madaraka makubwa.
Mkataba wa IGA utupiliwe mbali na DPW iwekeze bandari kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo za uwekezaji