Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Kuna uwezekano pia ma don wa unga wanamgeuzia kibao?

Tutazame pande zote.
Kwanini wamgeuzie kibao? Kwani amewakamata au hata kuwasumbua ma don? Wahangaike naye kwanini na hajagusa maslahi ya don hata mmoja
 
Ugaidi wa ccm ni tofauti na wa ISSI, Al shabab , Boko Haram, kina Koni, IRA.... wakat huu unataka uhuru zaidi na matakwa yao yatekelezwe... wa CCM unataka watu wakae kimya tu wasiwakosoe.... ndo maana wa hao wengine publicity inaweza uondoa kama jamii itaweza kaa kimya (japo si rahisi), lakini wa ccm ukikaa kimya ina maana unakuwa umekubaliana nao na wao wanakuwa wameshinda.... tuseme hapana, tupige kelele na walioko ndani ya system wasio penda uonevu watupe habari sahihi ili tuwaumbue... ahsante Mange Kimambi kwa kuwa gwiji kwenye kuja na facts kwa haya majangiri (in Manges tone)
..
 
Mjadala maridhawa neno gaidi kwa tanzania yetu limekuwa rahisi ndio haya matokeo yake ndugu zetu wanaishia magerezani kisa tu walitoa mihadhara kwa sababu ya kulikuza hili neno gaidi,labda niseme magaidi wengi wafanyapo shughuli zao hutoa taarifa na kwa uwazi si uwazi wa mimi na wewe kuona isipokua hata kipande kidogo cha clip tutashuhudia sasa hapa kwetu tuna vikundi vya wahuni kama vile komando yosso panya road na kiboko msheli bado hatujakuwa na magaidi wa kututia hofu ila tunajitia hofu!
 

Unga robo na utumbo nusu kilo mtu SABA inakula tayari wewe unadai hapo kwa mjomba wako hakuna njaa.
 
A strong tiss will ensure there is no terrorism except when and where they are the terrorists themselves. Hivi kama utawala unadulterated katiba (pamoja na mapungufu ya hiyo katiba) kuna umuhimu na u lazima wa ku terrorise walipakodi? Kweli?
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
 
Swali ni kwamba nani anaefadhili hivi vikundi vya kigaidi duniani jibu ni baadhi ya Serikali duniani hivyo sishangai kuona hapa Tanzania mambo kama hayo yanaibuka kwani chokochoko huanza mdogo mdogo kama hivyo hatimae hukomaa na mambo kwenda mrama kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hujajibu swali langu. Kama wewe ndiyo ungekuwa umefanyiwa huo ugaidi ungependa wengine wakae kimya ili lengo la magaidi lisifanikiwe?

Ni mjadala mpana, si kila swali lazima nilijibu mimi, tujadiliane na wenye kujua jibu la swali lako watakupatia kwa mtazamo wao.

Hii mada haijalenga kwa fulani ila ipo "general" ili kila mmoja ajadili kwa mtazamo wake.

Jibu langu kwako; Ukimya saa nyingine ni silaha kubwa sana.
 
Hiv walio ua na kudhulu mapadri zenj ni kina nani? Hiv walio waumiza wale mabinti wa kizungu zenj ni kina nani? Kule Rufiji, Amboni na Kilindi je Tuwaiteje mkuu?
 


Kuna wenyeviti na viongozi wa CCM wameuliwa kigaidi kabisa huko kusini, kulikoni?
 
Nimekuelewa point yako mama mkwe, sema ngoja nipige kimya maana wanamatusi sana
 
Hiv walio ua na kudhulu mapadri zenj ni kina nani? Hiv walio waumiza wale mabinti wa kizungu zenj ni kina nani? Kule Rufiji, Amboni na Kilindi je Tuwaiteje mkuu?

= kudhuru

Kuna kila uwezekano wahusika wasiwe kama unavyofikiria.

Unaweza kufanya ugaidi na kupandikiza ili fulani aonekane gaidi. Intelijensia hufanya kazi kinyume na fikra za wengi.

Intelijensia imefanya kazi na imefanikiwa kukujaza ujinga (brainwashed) na kukuaminisha kuwa gaidi duniani ni Muislam tu, kinyume kabisa na ukweli na uhalisia hata tafiti za kisomi zinaonesha kuwa huko ni kujazana ujinga tu.
 
Umeandika sana Dada yangu,
Ila hujaandika hao magaidi hapa ni kina nani
 

=majangili

Ujangili na ugaidi ni vitu viwili tofauti kama ardhi na mbingu.


Kuna uwezekano mkubwa pia mahasimu wa CCM wakatumia njia za kigaidi ili kuipakazia CCM within and without.
 
Huo ndio ukweli tuwanyamazie magaidi wasiwe na misifa
 


Tukubali kuwa Tanzania kwa sasa tuna tatizo na tutafute njia za kulitatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…