Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

I
habari za ugaidi ndio zinapendwa sana na CHADEMA na ndio wamejaa huku kwenye mitandao wanazisambaza kwa kasi sana....leo Magufuli anaweka jiwe la msingi ujenzi wa reli hakuna anaejali....CHADEMA wako busy na habari za watu kutekwa! CHADEMA ni janga la Taifa
Ila we ni mjinga kuliko mkeo
 
Ndugu yangu Faiza kwanza binafsi nashukuru kwa wewe pia kuliona hili, ya kuwa yanayofanyika tanzania ni ugaidi.

Laini acha tuongee huenda hawa Magaidi wataacha au wataona AIBU kwa vitendo vyao vya Kigaidi. Na hawa magaidi wanafahamika hata walipo, hawa ni magaidi tofauti na wale Alsha-ashab, Boko Haramu, Al-Qaeda, au IS; ambao matendo yao huyafanya kwa kujificha kiasi kwamba hata askari kupambana nao ni ngumu kiasi.

Lakini magaidi wa Tanzania ni kwamba asilimia kubwa wanafahamika.

NDUGU ZANGU HIVI KUNA TOFAUTI GANI KATI YA UTEKAJI UNAOFANYWA TANZANIA NA ULE WA BOKO HARAMU WA KUTEKA WASICHANA KULE NIGERIA??????

HIVYO NI JUHUDI ZINAHITAJIKA KATIKA KULIMALIZA HILI SUALA LA UGAIDI HAPA TANZANIA.

BINAFSI NAOMBA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUINGILIA KATI KAMA WANAVYOFANYA NCHI ZA SYRIA, MISRI, IRAQ, SOMALIA.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Hao wa nje uliowataja kuwa ni magaidi, kama ni magaidi kweli, huwa wanajitangaza ili walichokifanya kiwafikie wengi.

Huu wa kwetu mpaka leo sijaona aliyejitangaza, si kwa matukio ya Kusini ya kuuliwa wenyeviti wa CCM wala tukio la Roma au la Ben Saanane. Kwanini?

Nafikia kusema kuwa hawa magaidi wa kwetu wanataka wanatutumia sisi tuliojawa hofu tutangaze na hofu isambae zaidi na zaidi. Dawa yake nini?

Nionavyo, tukitangaza ndiyo furaha yao kwani malengo yao yametimia.

Tukikaa kimya lengo lao moja la kutangazwa litakuwa halijatimia. Hii itakuwa pigo kubwa kwao na itabidi tu wajitangaze, na hapo ndiyo tutawabaini kiulaini.
 
Tumekuelewa [HASHTAG]#Faizafoxy[/HASHTAG] siku ukitekwa tutanyaza ili lengo la magaidi lisifikiwe.

Hata Mandela aliitwa gaidi.

Hapa tunajadiliana kipi kifanyike ili kuukomesha huu ugaidi kwa faida ya Tanzania. Inabidi tuwe open minded na tusiwe biased kwani hata bungeni nimeona wabunge wa CCM na wa upinzani wote wakilalamikia hili.

Kwajinsi unavyojibu nna wasi wasi sana na uelewa wako wa kuweza ku "debate deliberately" kwa kutafuta ufumbuzi.

Critical thinking without prejudice is the key to achieve unbiased solution - FaizaFoxy
 
Lengo ni kupigana na ugaidi kwa kudhoofisha matakwa yao.
Sawa, lakini si kwa kiwango cha kukaa kimya wanapotoweka watu miongoni mwetu. Wakati mwingine ni vizuri kufikiria kwamba ingekuwa wewe ndiye ndugu, mume, mke au mtoto wa aliyetoweka ungefanya hicho unachoshauri. Anayejua maumivu ya kiatu ni mvaaji. Ninamwomba Mungu awape hekima na utu viongozi wetu wasilione jambo hili kuwa ni la kawaida na hivyo walipatie ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Inauma sana.

King Cobra
 
Majungu yapi,unadhani nani analipa kama siyo kodi yangu?Unadhani inalipwa na mshahara wake?Acho upumbavu?Mie siwangalii watu wanaosupport mauaji ya aina yeyote ya kiakili au kimwili
una roho mbaya sana
 
Hao wa nje uliowataja kuwa ni magaidi, kama ni magaidi kweli, huwa wanajitangaza ili walichokifanya kiwafikie wengi.

Huu wa kwetu mpaka leo sijaona aliyejitangaza, si kwa matukio ya Kusini ya kuuliwa wenyeviti wa CCM wala tukio la Roma au la Ben Saanane. Kwanini?

Nafikia kusema kuwa hawa magaidi wa kwetu wanataka wanatutumia sisi tuliojawa hofu tutangaze na hofu isambae zaidi na zaidi. Dawa yake nini?

Nionavyo, tukitangaza ndiyo furaha yao kwani malengo yao yametimia.

Tukikaa kimya lengo lao moja la kutangazwa litakuwa halijatimia. Hii itakuwa pigo kubwa kwao na itabidi tu wajitangaze, na hapo ndiyo tutawabaini kiulaini.

lakini tukikaa kimya wataendelea kututeka na kututia hofu, hata Jumuiya ya kimataifa haitafahamu kama Tanzania kuna ugaidi. Endapo tukikaa kimyana akatokea mmoja akasema "jamani Tanzania kuna tatizo hili la kutekwa wananchi...." hapo hakuna atakayeelewa kwani watashangaa mbona hawajasikia kilio chochote kuhusu jambo hilo??? Hivyo ataonekana aliyesema kuwa ni muongo.

SEMA USIKIKE.

Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994, endapo kama yasinge tangazwa, ni nani angejua kuwa kuna uasi mkubwa.

Hii ni faida ya utandawazi AMBAPO IKITUMIKA VIZURI PASIPO KUPOTOSHA UWEPO WA UTANDAWAZI. tusifananishe Ulimwengu wa sasa na ule wa miaka 60 iliyopita.

Kwa pamoja tusiangalie imani ya dini, siasa, taifa, au kabila; sote tukemee yanayoendelea nchini Tanzania kwani yanashika kasi siku hadi siku.

MIZAMBW
INANIUMA SANA!!!
 
Nashindwa kuelewa kwa nini serikali tukufu ya CCM iko kimya_ hata wabunge wake wanapokuwa wanakabiliwa na matishio ya kutekwa?

Watanzania hatuwezi tukakaa kimya eti tuwakomeshe magaidi kwa kimya chetu!!!.
FaizaFoxy Ndugu yangu nitaumia kiasi gani nikisikia umetekwa na kuteswa?
Je moyo Wangu utahimili kukaa kimya kweli?
Nitafanya niwezalo . Nikishindwa kulipa kisasi basi nitaandika.
Kamwe sitokaa kimya.
Kuna watekaji walitajwa kwa majina na miongoni mwao ni Ramadhan Igwondu, je alichukuliwa hatua gani?
Serikali yetu ya Leo imekuwa Crime Organiser ndio maana iko kimya na hata kwa maswali mazito inakuja na majibu mepesi.
Mzee Buji buji leo umenena
 
lakini tukikaa kimya wataendelea kututeka na kututia hofu, hata Jumuiya ya kimataifa haitafahamu kama Tanzania kuna ugaidi. Endapo tukikaa kimyana akatokea mmoja akasema "jamani Tanzania kuna tatizo hili la kutekwa wananchi...." hapo hakuna atakayeelewa kwani watashangaa mbona hawajasikia kilio chochote kuhusu jambo hilo??? Hivyo ataonekana aliyesema kuwa ni muongo.

SEMA USIKIKE.

Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994, endapo kama yasinge tangazwa, ni nani angejua kuwa kuna uasi mkubwa.

Hii ni faida ya utandawazi AMBAPO IKITUMIKA VIZURI PASIPO KUPOTOSHA UWEPO WA UTANDAWAZI. tusifananishe Ulimwengu wa sasa na ule wa miaka 60 iliyopita.

Kwa pamoja tusiangalie imani ya dini, siasa, taifa, au kabila; sote tukemee yanayoendelea nchini Tanzania kwani yanashika kasi siku hadi siku.

MIZAMBW
INANIUMA SANA!!!
Dhanna ya Mauaji ya kimbari na matukio ya kigaidi ni vitu viwili tofauti.
 
we mwanamke umenishinda tabia....mumeo ana kazi sana

Kwani unataka unioe??Kitu kikubwa mume wangu siyo mwanaume suruali anayesubiria kupewa tu anafanya kazi kulisha familia yake period.Na hatupo hapa kujadili familia zetu tupo kuinyoosha serikali,you either join us or kalale mbele
 
Sawa, lakini si kwa kiwango cha kukaa kimya wanapotoweka watu miongoni mwetu. Wakati mwingine ni vizuri kufikiria kwamba ingekuwa wewe ndiye ndugu, mume, mke au mtoto wa aliyetoweka ungefanya hicho unachoshauri. Anayejua maumivu ya kiatu ni mvaaji. Ninamwomba Mungu awape hekima na utu viongozi wetu wasilione jambo hili kuwa ni la kawaida na hivyo walipatie ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Inauma sana.

King Cobra

Ni njia mojawapo ya kupigana na ugaidi, Watanzania wote ni ndugu na yanayowafika hata mimi yananihusu na ndiyo maana nimeleta mjadala huu.
 
Kwani unataka unioe??Kitu kikubwa mume wangu siyo mwanaume suruali anayesubiria kupewa tu anafanya kazi kulisha familia yake period.Na hatupo hapa kujadili familia zetu tupo kuinyoosha serikali,you either join us or kalale mbele
mumeo anajua jinsi unavyoporomosha pumba huku jf?
 
Mtoa mada umekaaa upande gani WA lori mbele au ubavuni?Tutambuane me niko karibu na mlango nasikilizia kuruka Maana dereva kasema hasikilizi mambo ya nyuma huko yeye anajua tutafika tu.
 
Kama ugaidi haukufanikiwa awamu ya nne basi hauwezi awamu hii ya tano. Awamu ya nne watu wafitini walifugwa ili kumtawala vizuri mtanzania-divide and rule. Sasa hivi wafitini hawacheleweshwi-hata kama unajitungia tu kawimbo ka uchochezi kadogo, unashughulikiwa mpaka kuku unamuona kama mwewe.
 
Kwa namna nilivyowaona Bashe, Nkamia na Zitto jana bungeni na kwa kauli za Kessy leo bungeni sidhani kama kukaa kimya kutawezekana tena.Kama vifua vya wabunge vimeshindwa kuhimili itakuwaje kwa hawa walalahoi?!Tuache watu waseme na ktk kunena kwao suluhu itapatikana.FF wewe ulijua kama Roma aliimba wimbo wa kutukana?Binafsi sikujua lakini Kessy alijua na ametujulisha watanzania.
 
Back
Top Bottom