Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

habari za ugaidi ndio zinapendwa sana na CHADEMA na ndio wamejaa huku kwenye mitandao wanazisambaza kwa kasi sana....leo Magufuli anaweka jiwe la msingi ujenzi wa reli hakuna anaejali....CHADEMA wako busy na habari za watu kutekwa! CHADEMA ni janga la Taifa

Sijawahi kuona umeandika kitu cha maana. Kwani uzinduzi wa ujenzi wa reli ndiyo dawa ya ugaidi unaoendelea..? unataka tujali reli badala ya usalama wetu? Shame on you...
 
Sasa gaid wakifanya tukio mkakaa kimyaa siwanafanya kubwa zaidii ili mzungumzee???
 
habari za ugaidi ndio zinapendwa sana na CHADEMA na ndio wamejaa huku kwenye mitandao wanazisambaza kwa kasi sana....leo Magufuli anaweka jiwe la msingi ujenzi wa reli hakuna anaejali....CHADEMA wako busy na habari za watu kutekwa! CHADEMA ni janga la Taifa

Ndugu yangu hata kama ugaidi unahusisha vyama , vya kisiasa au vya kijamii lakini matokeo au madhara yake ni mtambuka. Usishabikie upande wako ukidhani utakuwa salama.

ATHARI ZAKE ZINATUGUSA WATANZANIA WOTE
 
Lengo ni kupigana na ugaidi kwa kudhoofisha matakwa yao.
Dawa ya Ugaidi unaofanywa na wenye mamamlaka ni kuwanyanganya mamlaka walionayo na kuwafanya wachukuliwe hatua za kisheria kwa makosa yao...mfanoPol Pot wa Cambodia alinyang'anywa mamlaka na kuhukumiwa miaka kadhaa baadaye..
 
Huu ni ugaidi wa aina yake, ugaidi unaokuwa sponsored na government!!!! Pathetic
Common in Afrika..mfano Uganda ya Amin, Afrika ya kati ya Bokassa Zaire ya Mobotu na Majirani Zetu kaskazini magharibi
 
FaizaFoxy

Una pointi ya msingi kwamba sehemu kubwa ya lengo la ugaidi ni kuogopesha jamii na kuifanya ifuate matakwa ya magaidi.

Lengo hili linafanikishwa na kusambazwa kwa habari za ugaidi.

Hivyo, kwa upande mmoja, kukataa kuripoti habari hizi za ugaidi kunaweza kusaidia kudhoofisha kiasi cha lengo hili kufikiwa.

Vyombo vingi vya habari vimeshawahi kufanya namna ya jambo hili. Mfano mmoja ni vyombo kadhaa vya Marekani vilivyokataa kutaja jina au kutoa picha ya Adam Lanza aliyeua watu kwa kuwapiga risasi ovyo katika shule ya Sandy Hook Connecticut.

Lakini, tunapoangalia tija ya kufanya hivi, tupime kwa mizani itakayotuletea tija bila kuleta madhara mengine.

Nchi za kidemokrasia zinaendeshwa kwa misingi ya uwazi na uhuru wa habari. Wananchi wana haki ya kupewa habari. Wanahabari wana wajibu wa kutoa habari.

Zaidi, habari za ugaidi zinaweza kusambazwa katika lengo na minajili ya kumaliza ugaidi.

Mathalani, habari za ugaidi zinaweza kuenea, ikiwamo picha za magaidi, na kusaidia magaidi hao kukamatwa kwa msaada wa wananchi.

Pia, habari za ugaidi zinaweza kusambazwa na kuweza kuisaidia jamii kujihami. Mfano, kama eneo la Rufiji lina ugaidi, habari za kuwaasa wananchi kwamba wachukue tahadhari wanapotembelea eneo hilo, kwa sababu lina ugaidi, zitakuwa habari muhimu katika kuwatayarisha wananchi wajihami vizuri na kuchukua tahadhari zote kabla ya kutembelea eneo hilo.

Kwa kifupi, kwa upande mmoja kuna haja ya kuacha kuhamanika sana na kuandika habari za ugaidi ovyo kiasi cha kutisha wananchi na kuwasaidia magaidi. Kwa upande wa pili, kuacha kabisa kuandika habari za ugaidi kutaweza kusababisha matatizo vilevile.

Kuna kanuni kadhaa nzuri na muhimu katika kuamua kutoa ama kutotoa habari ya kigaidi.Chache kati ya hizo ni:-

1. Habari itasaidia kuelimisha jamii kupambana/ kujihami na ugaidi?
2. Habari itamsaidia zaidi nani? Jamii au gaidi?
3. Kamahabari ikitolewa, itolewe kwa kiwango gani? Kutoa picha za watu waliouawa kinyama kutafaa au kutakosa staha kwa umuhimu wa maisha ya binadamu?
4. Habari zimethibitishwa au hazijathibitishwa na zinaweza kusababisha kashfa isiyo kweli (libel)?
5. Habari zinaandikwa kwa ukweli (facts) tu na si kwa ushabiki.
6. Gaidi hapewi uwanja wa kujitangaza zaidi ya inavyohitajika kuihami na kuifunza jamii.
7. Habari haiingilii wala kuharibu uchunguzi wa polisi na vyombo vya usalama.
8. Habari haihatarishi usalama wa raia wasio na hatia (kama kutaja vyanzo vinavyoweza kuumizwa na magaidi)
9. Habari haihatarishi usalama wa waandishi wa habari. Ikifikia sehemu ambayo waandishi wataanza kuhatarisha usalama wao,usalama wao uwe na kipaumbele kuliko habari.
10. Mizani mizuri itumike kati ya kuchapisha habari mapema na kuihakiki vya kutosha ili isiwe na au ipunguze makosa.

Safi sana.
 
tukae kimya ili watumalize. Kupiga kelele kunaweza saidia dunia kusaidia na kujua shida tupatazo refer USA alivyoingilia siria na kurusha mabom eiki iliyopita
 
tukae kimya ili watumalize. Kupiga kelele kunaweza saidia dunia kusaidia na kujua shida tupatazo refer USA alivyoingilia siria na kurusha mabom eiki iliyopita

Unakumbuka mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 yaliyobomoa majengo ya New York na kuyatandika makao makuu ya majeshi yote ya USA?

Waliotajwa kufanya mashambulizi hayo karibia wote ni Wasaudi lakini sijaona wala kusikia Saudi Arabia ikishutumiwa kwa ugaidi na USA.

Kwanini?

Kwa sababu tu wana maslahi yao Saudi Arabia.

Nchi za Magharibi hata uwe mbaya vipi kama wana maslahi yao kwako utakuwa ni mzuri tu kwao.
 
Na wakishawateka ndugu zetu wakawadhuru na kuwatia ulemavu tusiwapeleke hospitali wala kukaa nao karibu!!! pia wakiwaua tuwaachie wao wawazike wala tusiweke msiba!!!

Ama kitanda usichokilalia....

"Kutekwa" huwa ni vitani, hao waliotekwa walikuwa vitani?

Au unatekwa kwa watu kutaka "ransom", hao unaosema waliotekwa kuna "ransom" iliyokuwa "demanded"?

Hao unaosema walitekwa hao wala hawaingii katika kigezo cha ugaidi. Ugaidi ni kama matukio ya Kusini, ugaidi ni kama kutumia hao waliotekwa kusambaza habari za kutisha watu.

Tukio la Roma, hili baada ya kumsikiliza Ally leo nimeona kumbe ni mtu anaemtukana Rais, unamtukana Rais unategemea vijana wanaompenda wakuachie tu? Wacha Rais hebu mtu akutukane wewe tu mbele ya marafiki zako tuone kama utamuachia au marafiki zako watamuachia bila ya kumuadabisha.

Huo siyo ugaidi.
 
Sasa gaid wakifanya tukio mkakaa kimyaa siwanafanya kubwa zaidii ili mzungumzee???

Well, Kama inabidi tupige kelele mbona tumekaa kimya wakati wenyeviti wa mitaa wa CCM wanauliwa kigaidi huku Mkuranga na Rufiji?

Kuna matukio yanayoashiria ugaidi zaidi ya hayo kwa sasa?
 
Sijawahi kuona umeandika kitu cha maana. Kwani uzinduzi wa ujenzi wa reli ndiyo dawa ya ugaidi unaoendelea..? unataka tujali reli badala ya usalama wetu? Shame on you...

Sijaona kemeo lolote la matukio ya ugaidi ya hivi karibuni humu JF hadi sasa.

Wewe umeona?
 
Back
Top Bottom