Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Sasa tutakula hewa.....unga wa dona hatari,soda hatari,Nyama ya ng'ombe hatari,Ya mbuzi et magoti yanapata hitirafu, bia hatari, kuku wa kisasa hawa hatari, mayai yao hatari,wali,viazi, ndizi etc...vina wanga sana navyo hatari,mafuta ya kupikia ya wanyama hatari.....kila kitu hatari....aiseee...
Uongo huu kwani nani kaja hapa kulinda dunia?? Hizi tafiti za kupatia pesa siyo CONSTRUCTIVE no DESTRUCTIVE
 
Tatizo si dona tatizo ni mbegu za mhindi yenyewe madawakibao utasikia hii ni mbegu ya Muda mfupi, mambo Lea ya kisasa kibao bora usile, madhara ya chakula ni mengi kuliko faida
 
Sasa tutakula hewa.....unga wa dona hatari,soda hatari,Nyama ya ng'ombe hatari,Ya mbuzi et magoti yanapata hitirafu, bia hatari, kuku wa kisasa hawa hatari, mayai yao hatari,wali,viazi, ndizi etc...vina wanga sana navyo hatari,mafuta ya kupikia ya wanyama hatari.....kila kitu hatari....aiseee...

Tunaelekea kula makofi tu sasa maana hakuna chakula[emoji28][emoji28][emoji28][emoji38]
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Siyo, afflatoxin tuu, wakulima wanatumia sumu kuvu kutunza mahindi yao, na mara nyingi watengenezaji unga wanasaga juu kwa juu
 
Papuchi yenyew ina sumu na bado watu wanazama ndani we kula unachoona kwako sawa ukienda usukumani huko ndani simiyu Wasukuma wanakula dona enzi na enzi hadi wamezeeka hiyo sumu haijawahi wadhuru
 
Aspergilus flavus ni fungus anayezalisha aflatoxin,sumu ambayo ni hatari,na huyo fungus anazaliana kwenye maeneo ya joto na unyevu nyevu,mazao hasa karanga ni sehemu ambayo huzaliana sana....utunzaji wa nafaka ni mhm sana ili kumzuia huyu mdudu.
 
Sasa tutakula hewa.....unga wa dona hatari,soda hatari,Nyama ya ng'ombe hatari,Ya mbuzi et magoti yanapata hitirafu, bia hatari, kuku wa kisasa hawa hatari, mayai yao hatari,wali,viazi, ndizi etc...vina wanga sana navyo hatari,mafuta ya kupikia ya wanyama hatari.....kila kitu hatari....aiseee...
Cha ajabu wazungu wanakula vyakula hivyo hivyo na bado wanatupita kwa life expectancy
 
Dona ndio ugali ulio nikuza mpaka siumwi,eti leo hii umekuwa hatari, shida sana
 
Papuchi yenyew ina sumu na bado watu wanazama ndani we kula unachoona kwako sawa ukienda usukumani huko ndani simiyu Wasukuma wanakula dona enzi na enzi hadi wamezeeka hiyo sumu haijawahi wadhuru
Naona akili yako haiwezi kukaa sawa mpaka uitaje papuchi kwenye mfano wako
 
Sio rahisi dunia ya sasa kuikwepa sumu,japo angalizo linahitajika walau usiingize kiasi kikubwa cha sumu mwilini,na hapa ndio tunashauriwa kufanya mazoezi ili kuondoa sumu.Nowdays kila kitu ni sumu kuanzia vyakula,maji,juisi,matunda,mboga mboga,hali ya hewa,maisha chini ya awamu ya jiwe,now hadi papuchi ni sumu.
God help us...
 
Mkuu wacha kupotosha umma si kila unga wa dona unakuwa na aflatoxin bali ungeelezea kiundani watu wakuelewe na sio kutaka watu wafuate unachotaka ipo hivi.
AFLATOXIN
hii ni sumu inayozalishwa na fungi wanaojulikana kama Aspergillus flavus na Aspergillus parasiticus fungi hawa hushambulia mazao hasa wakati wa kuhifadhiwa na kabla ya kuvuna .
Unaweza kugundua kuwa mazao yako yameathirika kwa fungi hawa kwa kuwa huwa wanaacha utandu kama wa rangi ya bluu mpauko au kijana inayoelekea buluu kwenye mazao yako .
So nimejaribu kuelezea kadiri ya ninavyofahamu na sio tu eti wanaathiri unga mahindi tu hapana !!!
Wanaathiri mazao yote KUWA MUWAZI MKUU
 
Ukweli uko hivi kama Mungu akiku-assemble vizuri mwili wako hautatikiswa na aina yoyote ya chakula hata kama umekula sembe au dona afya yako itakuwa ngangali tu. Bibi yangu hajawahi ktk maisha yake kula ugali wa mahindi. yeye ni mwendo wa wali tu, tena ule wali wa kupika mchele unachuja maji ndipo unapalia, saa hizi anagonga 90 hana kisukari wala beriberi. Kuna mzee wa kimasai anashangaa wanaokula samaki na kuku yeye ni nyama ya ng'ombe akibadirisha ni nyama ya mbuzi ana miaka 81 hana pressure wala gaut.
 
Hii habari niliibandika awali, lakini baadhi ya wanaJF wakachangia kwa kejeli, sasa imedhihirika kwamba unga wa dona ni hatari kama mahindi yaliyotumika kuutengeneza yatakuwa na sumukuvu.

Ni muhimu kwa watumiaji kujiridhisha na usafi na usalama wa unga/ugali wa dona kabla ya matumizi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Mahindi yalovunwa shambani na kwenda moja kwa moja kukobolewa kupata unga wa dona bila kukawizwa ni dona la chakula bora sana.

Ikiwa utavuna na kuhifadhi mahindi hayo kwa kutumia madawa halafu ndo uanze kukoboa kidogokidogo, hapo ndipo panaweza kuwa ni tatizo.

Lakini sehemu nyingi wanavuna mahindi na kukoboa papo kwa hapo kupata dona ambalo likipigwa na maharage ya kule Rukwa au Mbeya, basi hicho ni chakula bora kabisa.

Au dona hili linagongwa na samaki wa sato wa kule Mwanza au pweza aliekuwa amekaangwa au roasted na chuzi lake zito, 🙂🙂

Na hii ya kuvuna na kukoboa papo kwa hapo ndo njia sahihi na murua kabisa.
 
Unapopeleka mahindi yasagwe kwa ajili ya matumizi yako ya nyumbani ukakuta mashine imeharibika mhusika anakwambia ngoja mashine itengenezwe ktk kufungua mashine unashuhudia kuna machujio ya chuma yamelika yametoboka na mengine yaliungwa siku za nyuma yamelika.

Swali particles (chembechembe ) za hivi vyuma vilivyolika na kutoboka zinaenda wapi?
 
Back
Top Bottom