Yaani mnataka kuua viwanda vya sukari vya ndani! kagera sugar na kilombero wana uwezo wa ku-saturate soko la sukari ingawaje kuna kipindi unaweza kutokea upungufu. Hivi viwanda vya sukari na mashamba ya miwa vimetoa ajira lukuki kwenye viwanda vyenyewe na wakulima wanaouza miwa. Utaratibu tunaokwenda nao ni kwamba ili kulinda viwanda vya ndani na ajira, serikali iwe inatoa vibali kuagiza bidhaa zinazozalishwa na kutumika kwa wingi nchini kama sukari endapo tu kutakuwa na upungufu.....chode chonde tusifanye nchi yetu gulio kwa kila kinachozalishwa huko nje, tutaua ajira za vijana wetu.