Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,716
- 9,051
=======
Rais Samia Suluhu: Wote tunajua jinsi Rais Magufuli alivyounga mkono mradi huu hivyo kuahirisha zoezi hili ilikuwa katika heshima kutambua juhudi zake katika mradi huu.
Mradi huu utatoa mapato kwa nchi zote, ajira za muda mfupi na kudumu na kujibu tatizo la ajira. Mradi huu utakuza uhusiano kati ya nchi zetu pia muingiliano wa watu.
Rais Yoweri Museveni: Tena, salamu zetu za rambirambi kwa kifo cha kaka yetu, Magufuli na pia hongera kwako kwa kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania. Asante kwa kukubali mualiko wangu wa kuungana nasi kutia saini makubaliano ya bomba la Afrika mashariki kutoka Hoima kwenda Tanga.
Nchi ndugu ya Uganda iligundua mafuta na gesi mwaka 2006, imechukua hii miaka 15, mwanzo mimi sikuunga mkono wazo la bomba, swali langu lilikuwa, kwani tuuze nje mafuta, Afrika mashariki haiitaji mafuta?
Kwenye wazo hili, nilipendelea kusafisha mafuta pekee ili tutumie mafuta hayo kwa ajili ya Uganda, Kaskazini Maghribi ya Tanzania, Magharibi ya Kenya, Rwanda, Burundi nk