Uganda yapitisha sheria mpya kukataza wanawake kuvaa nguo fupi

Uganda yapitisha sheria mpya kukataza wanawake kuvaa nguo fupi

Rais Yoweri Kaguta Mseveni wa Uganda ameusaini mswada wa sheria ambayo pamoja na mambo mengine inakataza ushoga, inakataza wanawake kuvaa nguo zinazobana, fupi juu ya Magoti na zinazoonesha kifua wazi na mavazi yote yatakayomfanya mtu wa jinsia nyingine kuwa na mhemuko wa mapenzi.

Mytake: Hapa kwetu tz napo inatufaa sana.

Rais kama huyu ndo anafaa kuitawala tanzania la sivyo kila siku tutaimba UKIMWI hali ya kuwa dawa yake inaeleweka. Au MSEVEN ni muislam nn???????? Coz hili ndo uislam linapigia kelele kila siku, hapo ndo penyewe!!!
 
Hiyo sheria ingefaa itumike hata Tanzania, lakini kwa sababu viongozi wenyewe ndio walewale, kwao hakuna shida, inaumiza sana, kuona wasomi wa vyuo vikuu ndio wanaongoza kwa utovu wa maadili, sijajua umuhimu wa elimu uko wapi hapo, maana tulitegemea msomi wa chuo kikuu angekuwa mfano wa kuigwa, lakini cha ajabu, watoto wanatoka nyumbani na maadili safi, wanavaa vizuri, wakifika chuo tu, wanaharibika, wanaanza kuvaa vimini, matiti njenje, visketi vifupi, harafu anaenda kuhudhuria lecture kwa profesor, hii hatari, tunatengeneza taifa la namna gani, ngono tu imetawala vyuoni, ndio maana wanachuo wengi wakirudi nyumbani, ni waathirika wa ukimwi, safi sana Mseveni.
 
Eti mini skirt zinachangia ngono?Upumbavu mtupu huu na hii inaonyesha jinsi waafrica na viongozi wao walivyo kuwa na akili za makamasi
 
nilidhani utapinga

Ukweli haupingiki kaka, tunachosha na vimini tunavyovaa wakat shapeless, miguu kama punda inagongana nyuma, makovu wengine tulijaliwa katiza kwenye mapori, wengine mikorogo iliyodunda bado tumo tu kuvaa vimini. Kisa kuwavutia wanaume!! hiyo sheria iwahi tu hapa uone KEKO inavyojaa wanawake tu
 
Safi sanaa,Kikwete nae aige basi hata kwa mbali navyomjua yeye ndio anapendea kuona manyonyo na mapaja yakiwa wazi moyo burudaniui
 
index.jpg
Ifike sasa tutunge sheria ya kurudia mavazi yetu ya zamani, mfano mzuri ni hawa watu wa asili ya namibia, wanatunza utamaduni wao
 
Ukweli haupingiki kaka, tunachosha na vimini tunavyovaa wakat shapeless, miguu kama punda inagongana nyuma, makovu wengine tulijaliwa katiza kwenye mapori, wengine mikorogo iliyodunda bado tumo tu kuvaa vimini. Kisa kuwavutia wanaume!! hiyo sheria iwahi tu hapa uone KEKO inavyojaa wanawake tu
wanawake wachache sana watakaokubaliana na haya uyasemayo, japo ndio ukweli
hata kama huna makovu, shape unayo na mengineyo, unatuonyesha ili nini?
 
Safi sanaa,Kikwete nae aige basi hata kwa mbali navyomjua yeye ndio anapendea kuona manyonyo na mapaja yakiwa wazi moyo burudaniui

hapa......mmmmh!!
😛eep: pigwa mawe mwenyewe
 
140219081848_africa_miniskirt_304x171_bbc_nocredit.jpg

Maandamano ya kkupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.

Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .

Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.

Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.

Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.

Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.

Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.

Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/02/140219_uganda_miniskirt.shtml
 
Itakuja lini huku kwetu hii sheria?

I can't wait kuona watu watakavyo babaika!!
 
tena alitakiwa kuweka kipengele cha kuwabaka kabisa...wanatufanya tushindwe kutembea kwa raha migegedo juu juu tuu.
 
Back
Top Bottom