Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sisi ma-air hostess itakuwaje sasa
Na wafanyakazi wa banks na kwenye mahotel ya kitalii, manake ndo mavazi yetu sie
Mh..hakuna sheria kama hiyo.airhostess ni zamani ram sasa hivi wanaitwa(cabin crew or flight attendant)kuvaa nguo fupi ram ni mtu mwenyewe anahamua maana sehemu nyingi ni chini ya goti..watu ndio wanavunja sheria wanavaa nusu uchi..
![]()
Taarifa ikufikie kwamba imepigwa marufuku kwa jinsia ya kike kuvaa nguo fupi (ki-mini) nchini Uganda na tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amesaini rasmi sheria hii.
Japokua baadhi ya Wabunge walipinga kwamba marufuku hii inaingilia uhuru wa mtu kuvaa, wabunge wengi wameunga mkono uamuzi huu.
Unaambiwa marufuku hii ambayo imelenga kuepusha vitendo vya ubakaji na ngono zembe kutokana na ushawishi unaotokana na uvaaji huu, inahusisha pia nguo nyingine fupi ambazo zinaacha sehemu kubwa ya mwili wazi kama vile kifuani.
Wanawake/Wasichana wataruhusiwa kuvaa mavazi mafupi kwenye matukio maalum tu yanayohusisha uvaaji huu kama vile michezo ambapo Waziri husika
Sheria hii pia inawabana Wanamuziki wa kike ambao wamekua wakivaa nguo fupi kwenye show zao pamoja na video ambapo Waziri Lokodo amesema hatutaki uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima
Vilevile vyombo vya habari yakiwemo Magazeti na TV, vimepigwa marufuku kuonyesha picha za watu wakipigana busu au picha zozote za Wanawake wakiwa nusu uchi.
Natamani na Hapa Tz ije hii sheria
Chanzo Hapa
kuvaa tuvae sie roho ziwaume nyie. mtuache tupumue, hips na manyonyo yetu nayo yahitaji kupunga upepo.
kuvaa tuvae sie roho ziwaume nyie. mtuache tupumue, hips na manyonyo yetu nayo yahitaji kupunga upepo.
hayo sio maadili ya mtanzania, ni maadili ya kwako mwenyewe
Aje na huku amuambukize presida wetu hiyo sera. Keros sana. Natamani niendelee kuleta watoto KIUME Tuuu.
Hata mimi naongelea mini sketi au gauni zinazoishia katikati ya goti au chini kidogo ya goti, sio mini za akina wema sepetu na akina aunt ezekiel, hata mimi sikubaliani na mini za hao wanaojiita mastaa. Vipi hawa vijana wanaovaa suruali chini ya makalio, sheria haijawatambua?
Habari zenu wana jf
raisi wa Uganda amepitisha sheria inayokataza uvaaji wa vimini na adhabu yake itakuwa kifungo cha miaka kumi jela
SOURCE BBC facebook page