Ugomvi ndani ya CHADEMA – Viongozi walaumiana uchache wa watu Arusha

Ugomvi ndani ya CHADEMA – Viongozi walaumiana uchache wa watu Arusha

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
UGOMVI NDANI YA CHADEMA – VIONGOZI WALAUMIANA, UCHACHE WA WATU ARUSHA

Na Nulphin Charles (Jenerali)

Leo, tarehe 28 Mei 2025, jijini Arusha, ulifanyika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambao ulitarajiwa kuonesha nguvu ya chama hicho katika Kanda ya Kaskazini. Hata hivyo, kilichotokea kilikuwa kinyume kabisa na matarajio, eneo la mkutano lilikosa watu, hali iliyogeuka kuwa aibu ya kisiasa na kuzua mgawanyiko wa wazi miongoni mwa viongozi wa juu wa chama hicho.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya upinzani barani Afrika, chama cha siasa kimezuia matumizi ya drone kwa hofu ya ukweli kuonekana. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa hatua hiyo ilikuwa ni juhudi ya kuficha mwitikio mdogo wa wananchi hali ambayo sasa imetafsiriwa kuwa ni ishara ya chama kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi wa Kanda ya Kaskazini, ambako zamani ilikuwa ngome kuu ya Chadema.

Viongozi waanza kulaumiana
Katika mlolongo wa lawama, kidole kimeelekezwa kwa Godbless Lema, anayesemekana kuwa amekuwa akimweleza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, "hali iko sawa", ilhali ukweli ni tofauti kabisa. Lema anadaiwa kuficha mapungufu makubwa yaliyopo katika Kanda ya Kaskazini, ambako viongozi wengi wamehama na wengine kukata tamaa.

Swali gumu sasa ni: Je, Chadema bado kina mwelekeo, au kimegeuka kuwa genge la makundi yanayokomoana kwa maslahi binafsi?
Migogoro ya ndani, chuki na visasi vimeonekana kuwa chanzo kikuu cha kuyumba kwa Chadema. Kwa sasa, kuna baadhi ya mikoa ambayo haina kiongozi hata mmoja. Mfano hai ni Mkoa wa Kigoma ambako hakuna kiongozi yeyote wa Chadema kwa sasa.

Ndimi Jenerali,
Ninaondoka nikiwa na mshangao kama mpiganaji aliyeamriwa kupigana kivulini huku kambi ikiwa imetekwa. Chadema, hamjachelewa kurekebisha mwelekeo lakini muda hauwasubiri.

IMG-20250528-WA1614.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250528-WA1615.jpg
    IMG-20250528-WA1615.jpg
    93.6 KB · Views: 28
Back
Top Bottom